Friday, 1 March 2013

MAJIMAJI SPORTS CLUB YAPIGWA JEKI



Waandishi wa habari wakifanya mahojiano na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Peramiho, Dkt. Venance Mushi katika viunga vya hospitali hiyo jana muda mfupi baada ya hafla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni mbili kwa Timu ya Majimaji kuiwezesha timu hiyo kufika malengo yake.






TIMU YA MAJIMAJI YAPIGWA JEKI




HOSPITALI ya Peramiho, Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma imetoa hundi ya shilingi milioni mbili kwa timu ya mpira ya Majimaji (Majimaji Sports Club) jana kwa lengo ya kuisaidia timu hiyo kufikia malengo yake ya kutafuta nafasi ya kucheza Ligi Kuu Bara mwakani.

Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt. Venance Mushi alisema kuwa hospitali yake kama sehemu kubwa ya jamii ya mkoa Ruvuma na mdau pia wa kuendeleza michezo yote, wameamua kuisaidia timu ya Majaimaji kiasi kidogo pesa, kwa lengo kuiwezasha timu hiyo kufanya vizuri mashindano ya ligi daraja la kwanza yanayoendelea hivi sasa iliweze kusonga mbele.


Alisema kuwa Peramiho ikiwa ni sehemu kubwa ya Mkoa wa Ruvuma hawanabudi kuisaidia timu yoyote ile kupanga ushindi na hatimaye kufikia malengo yake. 


Aidha, alisema kuwa Hospitali ya Peramiho imeamua kutoa msaada ya shilingi milioni mbili kwa timu ya mpira ya Majimaji ya ilikuwawezesha kutimishiza malengo yake pamoja na kutatua baadhi matatizo timu hiyo.


“ Hospitali ya Peramiho ikiwa sehemu kubwa ya Mkoa wetu wa Ruvuma na kama wadau wa michezo tumeamua kutoa kiasi kidogo kuisaidia timu yetu ya majaimaji ili iweze kujiandaa vizuri katika mechi za ligi ya daraja la kwanza zilizobaki na hatimaye kufikia malego yake,“ alisema Dkt. Mushi. 

Hata hivyo, Timu ya Majimaji ya songea, mkoani Ruvuma (Majimaji Sports Club) inayoendelea kushiriki Ligi ya Daraja ya Kwanza inayoendea nchini hivi sasa, kwa hiyo inahitaji msaada wa hali na mali iliweze kufanya vizuri katika mechi zilizobaki na hatimaye kupata nafasi ya kucheza Ligi Kuu Bara ya Vodacom (VPL) mwakani.

Naye Mwenyekiti wa Timu ya Mpira ya Majimaji mkoani Ruvuma, Humphrey Milanzi alitoa shukrani kwa hospitali ya Peramiho msaada wa pesa shilingi 2m/- na kuahidi kwa kwamba pesa hizo zitatumika vizuri kwa lengo la kusudio.


Alisema kuwa timu ya Majimaji kwa sasa inakabiliwa na ukata wa pesa pamoja na vifaa vya michezo, hivyo basi kwa wadau mbalimbali wa mkoa huu hawanabudi kuisaidia timu ili iweze kufanya vizuri pamoja na kuweze kutatua baadhi ya matatizo mbalimbali yanayoikabili klabu hiyo. 


Aliongeza kuwa pesa hiyo waliyopata kutoka Hospitali ya Peramiho wataitumia vizuri kwa kujiandaa na michezo iliyobaki na vilevile kutatatua matatizo mbalimbali ambayo timu hiyo ilikuwainabaliwa nayo wakati wa kiwa kambini.


“Tinaishukuru Hospitali ya Peramiho kwa msaada wao mkubwa na kugependa na wadau wengine pia waige mfano wa huu kwa kuisadia kwa vifaa na pesa ilituweze kuendelea klabu yetu majimaji iingie kwenye ‘Premier League’ ilikuwweza kuongoze kipato kwa Mkoa Ruvuma kwa ujumla,” aliseam mwenyekiti huyo wa timu ya majimaji.

“Ni jambo la busara sana kwa Hospitali ya Peramiho iliyofanya kusaidia timu yetu na tugeomba hata wadau wengi wa mkoa huu waweze kusaidia timu yetu, kwa sababu kufanya tuleta malengo kwa mkoa wetu ukizingatia kwamba timu inapofanya vizuri italeta maendeleo pia kwa mkoa.”


Mwenyekiti wa Majimaji alitoa mfano kwamba, timu yake itakaposhiriki Ligi Kuu bara, mechi nyingi zitachezwa hapa mkoani na wenye usafiri na hoteli mbalimali watafaidika kwa sababu wageni watafika kwa wingi na hatimaye kiongeza pato kwa mkoa.


Kwa upande wa Mwenyekiti FARU (Football Association of Ruvuma), Golden Sanga alimshukuru sana Mkuu wa Wilaya ya Songea , Joseph Mkilikiti kwa jitihada zake kuwaunganisha na Hospitali ya Peramiho na hatimaye kupata msaada huu wa pesa.



“Tunamshukuru sana mkuu wa wilaya, tuaishukuru Hospitali ya Peramiho na mimi kama mwenyekiti wa FARU na mimi pia katibu saidia timu ya majimaji…” aliongeza Sanga.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...