Monday, 7 September 2015

MKUTANO WA KUJADILI UPANGAJI WA MIPANGO WA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA

Katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa, Martin Mlwafu akifungua mkutano wa kujadili upangaji wa mipango ili kuboresha upatikanaji wa huduma bora za afya katika halmashauri ya wilaya ya Iringa uliofanyika mjini Iringa leo.

Mkutano huo wenye madhumuni ya kushirikiana katika matokeo ya utekelezaji wa mradi wa CEGO (citizens engaging in government oversight in health service provision ) kwa kupitia mfumo wa ufuatiliaji wa uwajibikaji jamii (social accountability monitoring-SAM ).

Mradi huo unatekelezwa na TACOSODE kwa ufadhili wa watu wa marekani kupitia shirika la misaada ya maendeeleo ya kimataifa la (USAID).

Mkutano huo pia unatoa fursa ya kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya afya na kuadhiri kwa kiasi fulani upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi wa halmashauri hiyo.


Afisa Uchechemuzi (Advocacy Strategist) kutoka TACOSODE, Abraham Kimuli akifafanua jambo wakati mkutano.

Secretarieti kutoka TACOSODE wakifuatilia majadiliano.

washiriki

Makamu Mwenyekiti wa TACOSODE, Leonard Lugenge akitoa maneno ya utangulizi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi. 

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...