Na Vicky Macha,
Iringa.
MADEREVA wanatakiwa kuzingatia
alama za barabarani ili kukabiliana na ajali za mara kwa mara hasa
zinazojitokeza katika barabara kuu ya Tanzania na Zambia (TANZAM).
Rai hiyo ilitolewa jana na Mkandarasi wa Mradi wa ujenzi wa
barabara kutoka makao makuu (Tanroads) Kenfas Mahenge wakati wa
makabidhiano rasmi ya barabara hiyo na makandarasi wa kampuni ya Aarsleff-
Interbeton Denmark mara baada ya kumalizika kwa ujenzi wa barabara hiyo
mwishoni mwa wiki.
Mahenge alisema hali ya nchi ilivyo ambayo ni ya milima, miteremko
na kona nyingi hasa katika maeneo ya hifadhi ya wanyamaMikumi ni lazima kila
dereva kuzingatia alama hizo pindi apitapo katika barabara hiyo kwani kumekuwa
na ongezeko la ajali zinazoendelea kuwatafuna wananchi hasa abiria.
Alisema kwa kuliona hilo walilazimika kumtaka mkadarasi kuweka
kila eneo alama ikiwemo matuta, lakini kumeoneka madereva kuendesha
magari kwa uzoefu mbali na kupatiwa elimu ya udereva.
Hata hivyo alisema utaratibu wa kuwatoza fidia waharibifu wa
barabara pindi ajili inapotokea ni pamoja na kukamata bima zao ikiwa ni
harakati za kutokomeza ajali zisizo za lazima.
Naye Meneja wa wakala wa
barabara wa mkoa wa Morogoro (Tanroads) Charles Madinda alisema kumekuwa
na uzembe kwa baadhi ya madereva hasa nyakati za usiku na husababisha ajali
nyingi na wakati mwingine ajali hizo huwa ni za uzembe ikiwemo mwendo kasi.
Alisema sheria ya mwaka 2007/ 2009 kifungu cha 13 ya kulipa fidia
endapo ajali itatokea na kuharibu barabara na alama zilizowekwa inafuatwa bila
ya kumtazama ni mtu wa nafasi gani katika nchi kwani gharama za ujenzi ni
mkubwa hivyo ni lazima kuzingatia muda ulioweka kwa matumizi ya barabara hiyo.
“ Barabara hii ni lazima itunzwa kwa madereva na hata wananchi
waishio jirani na eneo lililopita barabara ili iweze kudumu kwa miaka zaidi ya
20 kama ambavyo imekusudiwa na ni wajibu wa kila mmoja,” alisema.
Kwa upande wake Meneja wa
wakala wa barabara mkaoni Iringa (Tanroads) Paul Lyakurwa alisema
wakandarasi hao wamejenga barabara hiyo kwa fedha ambzo walitakiwa kuzitumia
bila ya kupungua wala kuzidisha.
Alisema barabara ambayo wameitekeleza inaukubwa wa kilometa 150
ambayo ilikuwa na sehemu nne ambazo ni Iyovi – Ruaha Mbuyuni km 40, Ruaha
Mbuyuni – Kitonga km 47, Ikokoto – Iringa km 61 na Iringa Mjini km 2
iliyojengwa kwa fedha za US$ 110 milion / Euro 76.2 Milion.
Lyakurwa alisema kutokana na hali ya uwaminifu wao kwa kuzingatia
muda na kiasi cha fedha za makubaliana wamelazimika kuwapa sehemu nyingine ya
ujenzi wa barabara itokayo Iringa - Mafinga yenye urefu wa km 68
ambayo inatarajiwa kuanza rasmi mapema Septemba 18, 2011 na kumalizika July 9,
2013 kwa Euro 38.5m (us$ 46.2m).
Mradi huo wa awali ulianza rasmi September 19, 2008 kwa makubalina
ya miaka mitatu ambayo ni 18 Sept 2011 na imemalizika kwa kuzingatia makubalina
hayo.
Mwisho.
0713 654945
0713 654945