Friday, 21 August 2015
NEC YAMTEUA LOWASSA NA MGOMBEA MWENZA WAKE, JUMA DUNI HAJI, KUWA WAGOMBEA RASMI WA URAIS WA TANZANIA
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva akimkabidhi, Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, nyaraka mbalimbali zitakazotumika wakati wa Kampeni, kwenye Ofisi za Tume hiyo, Jijini Dar es salaam leo Agosti 21, 2015. Kushoto ni Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva akizungumza mara baada ya kupokea Fomu zilizorudishwa na Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni baada ya kukamilisha mchakato wa kutafuta wadhamini katika Mikoa 10 ya Tanzania na kutimiza masharti yote ya Uchaguzi, leo Agosti 21, 2015 kwenye Ofisi za Tume hiyo, Jijini Dar es salaam.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutangazwa rasmi na Tume ya Uchaguzi kuwania nafasi hiyo, leo Agosti 21, 2015 kwenye Ofisi za Tume hiyo, Jijini Dar es salaam. Pembeni yake ni Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni
Mh. Lowassa na ujumbe wake wakiondoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Subscribe to:
Posts (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
The most deadly form of tuberculosis is one that lies in wait inside the body for years, attacking at the first sign of weakness. Abou...