Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Iringa Mhe. Amina J Masenza (kuume) na Mshauri wa Mgambo Mkoa Meja Akili katika Maadhimisho ya Kumbukumbu ya siku ya Mashujaa Mkoani Iringa.
Saturday, 25 July 2015
Hepautwa:nafahamu maumivu yaliyotokea kwa wana CCM baada ya kuichagua Chadema uchaguzi wa mwaka 2010
Nuru Hepautwa
Na Friday Simbaya, Iringa
KADA maarufu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa mjini Iringa, Nuru Hepautwa amesema anafahamu maumivu yaliyotokea kwa wana CCM baada ya kuachia jimbo hilo mikononi mwa Chadema katika uchaguzi wa mwaka 2010 lakini akaahidi kuyamaliza endapo atapewa ridhaa hiyo.
Hepautwa ambaye pia ni mfadhili wa mashindano ya soka yaliyojizolea umaarufu mjini Iringa ya Hepautwa Cup alitoa mchango huo jana wakati akijinadi kwa wanachama katika Kata ya Kitwiru Jimbo la Iringa mjini.
MFANYABIASHARA huyo alitangaza nia ya kuwania ubunge wa jimbo la Iringa Mjini hivi karibuni katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu kwa kupitia tiketi ya chama chake, Chama cha Mapinduzi (CCM).
Hepautwa ambaye pia ni Naibu Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Iringa Mjini alisema anafahamu maumivu yaliyotokea kwa wana CCM baada ya kuachia jimbo hilo mikononi mwa Chadema katika uchaguzi lakini akaahidi kuyamaliza endapo atapewa ridhaa hiyo.
Kwa mwaka wa tano sasa, jimbo la Iringa Mjini limeendelea kuongozwa na Mchungaji Peter Msigwa aliyechaguliwa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika Uchaguzi Mkuu wa 2010.
Akizungumzia vipaumbele vyake endapo atapewa ridhaa hiyo, Hepautwa alivitaja kuwa ni pamoja na kubuni vyanzo vipya vya ajira kwa vijana na kuboresha huduma katika sekta mbalimbali zikiwemo za afya, maji, elimu, miundombinu ya barabara na biashara.
Kwa upande wa sekta ya biashara alisema mpango wake ni kuwashawishi wafanyabiashara wenye uwezo mkubwa kujenga viwanda vya mazao ya kilimo, kutenga maeneo ya wafanyabiashara wadogo na kuufanya mji wa Iringa kuwa mji wa kibiashara.
“Nataka kuona Iringa unakuwa mji wa biashara za aina zote, magari, vipuri, mitambo, nguo, vyakula na nyinginezo ili waliojirani na CCM wasiende tena Dar es Salaam ili sehemu ya kununua mali wanazohitaji kwa jumla iwe Iringa,” alisema.
Alitaja biashara nyingine zinazoweza kufanywa na wakazi wa Iringa Mjini kuwa ni pamoja na ya kuongoza na kusafirisha watalii ili kuiongezea msukumo wa kutosha.
“Kule kaskazini, vijana wengi kama sisi wamenufaika na mapato yatokanayo na utalii kwasababu wamethubutu kuwekeza katika sekta hiyo. Nataka kuona na sisi wa Iringa tunatumia ujirani wetu na hifadhi ya Taifa ya Ruaha kuchangamkia fursa hiyo,” alisema.
Katika afya alizungumzia namna atakavyosaidia kuboresha huduma hasa za mama na mtoto, mapambano ya virusi vya Ukimwi na upatikanaji wa vifaa tiba na dawa katika vituo vyote vya kutolea huduma.
Katika Jimbo la Iringa mjini, mkoani Iringa chama hicho kimeandaa mikutano kwa wagombea ubunge wote ya kuwatambulisha kwa wanachama ikiwa sehemu ya pili ya mchakato ya kumpata mgombea pekee atakaye peperusha bendera ya chama hicho kwa kushindana na vyama vya upinzani katika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu.
Jumla ya wagombea ubunge 13 Iringa mjini waliochua na kurudisha fomu na wameanza safari ya kuwatambulisha kwa wanachama katika matawi 81 ya CCM Jimbo la Iringa Mjini.
Wana CCM hao wanaoomba nafasi ya ubunge ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu, Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe Frederick Mwakalebala na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mahamudu Madenge.
Katika orodha hiyo yupo pia Dk Yahaya Msigwa, Nuru Hepautwa, Addo November Mwasongwe, Adestino Mwilinge, Frank Kibiki, Aidani Kiponda, Peter Mwanilwa, Fales Kibasa, Michael Mlowe na Balozi mstaafu Dk. Augustine Mahiga.
UWT CCM MKOA WA IRINGA WACHAGUANA
Rose Tweve
Ritta Kabati
Lediana Mng'ong'o
wajumbe
Zainabu Mwamwindi
wagombea
UMOJA wa Wanawake wa Tanzania (UWT) mkoa wa Iringa umekataa kumuongezea kipindi kingine cha miaka mitano bungeni, Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Lediana Mng’ong’o (58) katika mkutano wake wa kura za maoni uliofanyika juzi, mjini Iringa.
Mng’ong’o ambaye pia alikuwa mmoja wa wenyeviti wa bunge la 10 linalomazima muda wake amekuwa mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa kwa miaka 15.
Subscribe to:
Posts (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
Habari ndugu msomaji wetu wa blog, Natumaini unaendelea vyema. Leo tutaanza kujifunza kilimo cha bora cha nyanya, na tutaanza kufahamu vit...