Thursday, 30 July 2015

DAUDI MASASI ATANGAZA NIA KUGOMBEA JIMBO LA IRINGA MJINI


DAUDI MASASI (KULIA)

Awali ya yote namshukuru mwenye enzi mungu kwakunijaali kutangaza tena dhamira yangu ya dhati na ya siku nyingi .2005 Niligombea hivyo sijakurupuka.

Mimi ni mzalendo wa iringa mjini nimezaliwa , nimesoma, nimekulia , naishio na hasa , Iringa mjini ni nyumbani . Naijua iringa ilipotoka inapostahili kwenda . Ninajitambua vyema kwa kipaji na ubunifu . Heshima na adabu alivyo nijaalia mwenye enzi mungu na mafundisho niliyo lelewa na wazee wa iringa mjini. Nikiwa jasilio mkubwa, natumai wazalendo wa iringa mjini wataniamini kwasababu :-

Wengi wananifahamu kuwa mkweli na muaminifu . Sina kashfa kijamii wala kisiasa.
Nina uchungu wa dhati na maendeleo ya iringa na wana Iringa. Nina jawabu la ufumbuzi wa ajira hususani kwa vijana  kwenye secta za ,

MMLIKI WA ST. MATHEW, ST. MARK ADAIWA TALAKA NA MGAWANYO WA MALI



Na Mwandishi Wetu

MDAI katika kesi ya madai ya talaka na mgawanyo wa mali Magreth Mwangu mkazi wa Mkoani Singida dhidi ya Mkurugenzi wa Shule za sekondari za St.Mathew na St Marks Thadei Mtembei amelalamikia kitendo cha Benki ya CRDB kutoa taarifa zake za benki bila idhini yake wala ya mahakama.

Pia ameilalamikia mahakama ya Mwanzo Kizuiani inayosikiliza kesi hiyo kwa kutumia Wakili wa kujitegemea licha ya kuwa mawakili hawaruhusiwi katika mahakama ya Mwanzo.

Kesi hiyo inasikilizwa na hakimu Rajab Tamaambele.

Wakili huyo amekuwa akimwakilisha mdaiwa ambaye amekuwa hafiki mahakamani tangu kesi hiyo ifunguliwe kwa kile kilichoelezwa wamepata kibali kutoka kwa mwanasheria mkuu wa serikali kinachoruhusu kesi hiyo kusikilizwa na wakili bila mdaiwa kuwepo.

Kwa mujibu wa Mwangu tangu kesi hiyo ianze kusikilizwa mahakamani hapo mdaiwa amekuwa hafiki mahakamani na badala yake amekuwa akiwakilishwa na mtoto wake,Peter Mtembei ambaye ni Wakili hali iliyofanya kesi hiyo mpaka inaisha na kufungwa ushahidi mdaiwa akiwa hajasikiliza shahidi hata mmoja.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...