DAUDI MASASI (KULIA)
Awali ya yote namshukuru mwenye enzi mungu kwakunijaali
kutangaza tena dhamira yangu ya dhati na ya siku nyingi .2005 Niligombea hivyo
sijakurupuka.
Mimi ni mzalendo wa iringa mjini nimezaliwa , nimesoma,
nimekulia , naishio na hasa , Iringa mjini ni nyumbani . Naijua iringa
ilipotoka inapostahili kwenda . Ninajitambua vyema kwa kipaji na ubunifu .
Heshima na adabu alivyo nijaalia mwenye enzi mungu na mafundisho niliyo lelewa
na wazee wa iringa mjini. Nikiwa jasilio mkubwa, natumai wazalendo wa iringa
mjini wataniamini kwasababu :-
Wengi wananifahamu kuwa mkweli na muaminifu . Sina kashfa
kijamii wala kisiasa.
Nina uchungu wa dhati na maendeleo ya iringa na wana Iringa.
Nina jawabu la ufumbuzi wa ajira hususani kwa vijana kwenye secta za ,
(i) Burudani na michezo. Mimi
ndiye mwenyekiti wa iringa movieclub, kwa hiyo nikipitishwa na chama changu cha
ACT wazalendo na kuchaguliwa kuwa mbunge tatizio la kurekodi filamu litakua
limekwisha ( ni BURE) nitanunua camera, Taa , boom ,computer MAC apple,
kwaajiri ya kueditia filamu na usafili wa kuendea location. Vifaa hivi
vitasimamiwa na iringa movie club, lakini vitatumiwa na wanamuziki wa kizazi
kipya , lakini pia Lipuli na timu yoyoyte ya iringa itakapo kua inahitaji
usafiri gari hilko litatuimika.
Nitaitumia vyema miongozo ya ACT-WAZALENDO, Ambayo
inapambanua vyema masuala yote muhimu ya kiuchumi kijamii na uongozi bora, Elimu
,afya n.k ilani ya ACT wazalendo , KATIBA
ya ACT wazalendo na AZIMIO LA
TABORA la ACT wazalendo.
Nikichaguliwa kuwa mbunge wa
jimbo la iringa mjini , nitafanya kazi kwa ushirikiano na wana Iringa
kuupa mji wa iringa sura inayostahili, kwa kupigania uwepo wa soko jipya la
kisasa ambalo hapana budi liendane na kasi ya mabailiko na ukuaji wa mji
kuelekea kuwa jiji. Soko hilo nitashauri
liwepo sehemu ambako hivi sasa panaitwa sabasaba.
Uwanja huu uilijengwa mwaka 1976 katika sherehe za miaka 22
tami ya kitaifa iliyofanyika mjini iringa .lakin waliojenga hapo ni taasisi
mbalimbali za serikali na mashirika ya umma nakamwe uwanja huo si halali ya
CCMsoko hili likijegwa litanyanyu a au kuchangia kwa kiasi kikubwa kukuza
uchumi wa iringa .
hata kama halitakuwa kama soko la kariakoo basi angalau liendane
na lile la mwanjelwa jijini mbeya .
lakini pia hata kama halitakuwa la kimataifa
,ni imani yangu litakuwa soko maarufu sawa kwa wafanyabiashara na wajasiriamali
mbalimbali ,kwani mwanza ,arusha ,kilimanjaro na hata nchi za jirani ,zitaingia
moja kwa moja katika biashara na iringa .
Jambo la tano ni uwanja wa kisasa wa maonesho ya biashara na
kilimo .iringa ninayoitazama mimi nikiwa mwana iringa halisi kwa wakati
tulionao na ujao ,inahitaji hiyo .nikichaguliwa kuwa mbunge ,ni jambo ambalo
nitalipigania ili wafanyabiashara wapate fursa ya kuonesha biashara zao lakini
pia kuona zawale watakao kuja kutoka sehemumbalimbali .
ni eneo ambalo wauza
vinyago pia wangepata nafasi nzuri ya kudumu ,na watalii wanaokuja ruaha
nationalpark watakuwa wakijipatia vituvya asili vyaaAfrica pahala apo.wauza
mitumba pia watapata nafasi hapo na biashara nyinginekwenye eneohil ipia
zitapata soko na hivyo kwa asilimia nyingi tatizo la ajira kwa wana iringa ,
kupungua ni aibu mkoa wa kilimo , wa kulima wake kwenda maonesho ya
nanenane mbeya au morogora.
SWALI….!
Pesa za kujengea soko la kisasa na uwanja wa maonesho zitatoka wapi .? JAWABU .zipo pesa nyingi kwaa jiri hiyo
katika bank mbalimbali ikiwemo bank ya Dunia . Lakini mifuko ya hifadhi ya
jamii pia inazopesa nyingikwa kazi kama hizo. M’bunge mzalendo mjanja ataweza kufanikisha haya mambo vizuri.
Ikiwa soko litajengwa uwanja wa sabasaba , uwanja wa maonesho
ya biashara na kilimo ningeshauri ujenge eneo lile lililokuwa hifadhi yam situ
kihesa kilolo. Ama la.! Maeneo yapo mengi kuelekea kiwele, njia panda ya
Tosamaganga n.k Iringa hakuna tatizo la ardhi , tatizo ni wabnifu na
wafuatiliaji, na nani katoa wazo? Kwa uzalendo na maslahi ya Iringa , tuache
mawazo mazuri yatumike, bila kujali aliyetoa ni DAUDI MASASI.!
Hakuna mtu duniani anae jua kila kitu , kwahiyo ata mimi sio
nina jua kila kitu , au kila au kilakitu nitafanya mimi tu.! Hapana nitatoa
fursa ya kukutana na wana iringa bila ubaguzi katika mpango maalum na nitapokea
ushauri , maoni na mawazo mazuri yote
nitafanyia kazi kwa faida ya Iringa na wana iringa.
Kwamfano tunalotatizo la barabara ya hospitali ya
rufaa inayo pita magereza , mimi nikiwaa m’bunge nitalishughulikia jambo hilo kwa kushauri
wizara ya mambo ya ndani iachie eneo hilo lote na hata Magereza ihame na kwenda
mlolo amako wao wanalo eneo la kutosha .
Likiwezekana hilo,
hospitali itapata eneo la kuongeza vyumba vya kulala wagonjwa na mambo mengine
kama vile chumba cha maiti cha kisasa ,zaidi ya kile alicho jenga mfanya
biashara marwaa kwa kumbukumbu ya marehemu bintiye kipenzi nina, marwaa na kushuhudia vile vyumba vya
zamani vikiwa na hali mbaya sana.
Lakini usafiri wa
basi za mjini zinazoegeshwa barabara ya mivinjeni (mashine tatu) tayari eneo
hilo halifai kabisa kwa shughuri hiyo ya kusafirisha abiria kwa usalama pia wa
watembea kwa miguu, wakati standi kuu ikiendelea kujengwa
huko kuliko kubalika ijengwe.? Ni vema kituohiki kihami kwa muda
makorongoni barabara mbili ,moja iwe yakuegesha nakuingilia , nay a pili iwe ya
kutokea. Bila shaka hata wajasiria mali watapata nafasi nzuri zaidi ya kutafuta
riziki yao kwa usalama.
Lakini stendi ya mkoa ikisha ni vema hii ya zamani ikawa sasa
ndo ya hiace kwa maeneo ya mjini nay ale ya nje ya mji.lakini eneo hili la
stend kuu ya sasa lilipo ni katikati ya mji ni jambo lakushangaza sana kuona
waliobomoa mabanda ya mbao,wamajenga
mabanda ya tofali. Tunaposema ubunifu ni
eneo kama hili halikuhitaji tena mabanda;
bila kujali eneo hilo linamilikiwa na nani; bali lilihitaji mchoro mzuri wa
ghorofa la kisasa la zaid ya ghorofa nne ,tano au zaid,kwasababu hili ndilo
eneo la sura ya mji.
Kwa hiyo tunaposema kipaji ni ubunifu; maana yake iwe ni pamoja
na kuona mbali.
Mimi kama mwanamichezo halisi siwezi kuacha kuona inahitaji uwanja wa mkoa. Uwanja
wa samora umemilikishwa na chama cha mapinduzi, hata kamaeneo hilo lilikuwa na
shule ya serikali (mshindo .p. school) bado wana iringa na watanzania tunayo
nafasi ya kuhojilakini wakati jawabu halijapatikana ni lazima tuwe na mbadala,
mji unapanuka vema, basi hili ni jambo muhimu kulifanyia kazi. Chama cha soka
cha mkoa IRFA tumeambiwa tayari wanao
uwanja bado kujengwa tuhuko kitwiru’ ni vema lakini uwanja wa mkoa muhimu .
Iringa inahitaji mbunge mzalendo mwenye uchungu na kujua nini
kifanyike ili iringa itajilike vizuri hata kwa watanzania wa maeneo mengine
.wacheza mpira waliotoka iringa na kucheza soka la kitaifa na kimataifa wakiwa
na vipaji vya ajabu ni weng lakini kwavile hatujapata bahati hiyo ya m’bunge
motto wa mjini mnyakuboma isipokuwa mwaka huu
2015 nitakapoingia mimi; inshaalla iringanitaisemea na watu wataona
tofauti.
Iringa iliyotoa wachezaji wenye vipaji na historia kama KESSY KIBUDA, SAAD ALLY, SHABANI
CHELULA, ABDALLAH MWANGAMILO< ABUU NELLY< ALLY KONDO mkubwa na
mdogo,SHAMTE, JUMAKALUNGWANA, AGUSTINO
MWAMNYALA, ALLY MWACHULA ,ABAS KANDOLO ,MICHAEL SOSO, MUSSA KISOKI SALIMU
k kiyendesa ,blastus mathias,
juma rajabu mdigo, said chalamila ,jamuhuli kikoti, super, steven mussa, faiya
said, daud kufa kunoga,hamad mbata,damkan butimu,costa magolosa,Joshua kilale,
kevin haule,,jastin mtekeve,david sawala, ally maliva, venaus
mwamoyo.,mohamadiy sigara, na wengine weng sana (siwezi kutaja wote)wachezaj
hawa kutoka iringa walikuwa viwango vya hali ya juu sana kiasi cha kuchezea
samba, yanga, na stars lakin lringa kwa kukosa mtu wa kuisemea, watanzania
hawajui thaman ya wachezaji hawa kwa mfano kessy na saad ni washambuliji hatari
zaid kuliko washambuliaji wote waliopata kutokea nchin Tanzania kama unabisha
uliza kwa wanaojua wakwambie.baadhi yao niliwataja ni marehemu,mungu awalaze
mahara pema peponi AMINIIIII
8 lakini hata
katika nyingine kama vile bongo freva na
muziki wa dansi, iringa imetoa vipaji vingine akina ally makungulu,john kitime
lakin nani anavisemea na kuwa njia kwa wengine; kwa mf ni wanairinga wangap
wanajua thamani ya mpiga solo mwandamizi wa msondo ngoma ridhiwan ,abdul
pangamawe,kuwa ni kijana wa iringa mshindo; ni wanairinga wangapi wanajua
hakuna wachoraj wa katuni mwenye kiwango kama ilivyokua kwa marehemu JOHN
MATHIAS KADUMA. ANTOFOGASTA; TANZANIA ONE. Mchoraji mkuu wagazeti langu la
TABASAMU enziyake?
Michoro mingi ya
wachoraji wa leo wanagandamizia michoro ya JOHN KADUMA. Lakini pia IRINGA
ilipata kutia wachezaji NETIBAL wazuri kiasi cha kuchukua ubingwa wa nchi na
kutamba sana kabla ya wengi wao kutimkia bora ya dar.
Baadhi yao ni DADA
MWAHIJA MASASI; SHUMBANA; HARUNI MSANGU; TWAHIYA; MAJALIWA; AMINA LUPEMBE;
SAIDA KATIUKO; MWANAIDI LUSASI; LENA NDAMBO; SEKELA NGOSI; MAIMUNA MASASI;
NASEKILE ANTONI; ASHA AYUBU na walimu wao
hodari mwalimu MARRY CHALAMILA[MAMA CHOOKI] na mwalimu mwamuzi [MAMA
BUTININI]. Kiasi hata timu ya taifa ya wanawake kusheheni nyota hao toka
iringa. Lakini challenge ya NETBALL ilipata kufanyika uwanja wa samora miaka ya
mwishoni ya sabini; na watoto wa iringa wa enzi hizo pamoja na wananchi wengine
wa iringa tuliweza kushuhudia michezo hiyo na kumuona live Ida musoke aliye kuwa akicheza nafasi ya
mfungaji akiwa anavaa G5 kutoka timu ya Uganda , sifa yake ni kwamba alikua
mrefu kupita kiasi, na kwamba akiupata mpira anautumbukiza kiurahisi tu. Lakini
hata hivyo Uganda hawakuchukua ubingwa na taarifa zisizo rasmi zilisema Iddi
amin alimpiga risasi mwanamke huyo mrefu.
Lakin I vipaji vya iringa havikuishia hapo, ni wana iringa wangapi
wanajua mastaa wa filamu , Halima
yahaya’Davina’ Shamsa ford ‘Chausiku’ ,Mohamed mwikongi Frank, Tausi mdgea,
William mtitu, na wengine kibao ni watoto wairinga.Nimewataja wahchache li wana
iringa msifanye makosa kwa kuacha kunichagua, ili iringa ikae pahala panapo
stahili, kwani hata laya na marekani , watu wanao ishi vizuri zaidi na pesa zao
, ni sekta za michezo na burudani.
Wachezaji kama Yaya Toure, Samwel Etoo, Drogba, pamoja na kuchoka ni
wachezaji ambao wametengeneza pesa nyingi ambazo bila shaka zitawasaidia ndugu
zao wengi, hata mishahara ya kina Samata , Ulimwengu hapojirani DRC unaona ina
wasaidia pia wanafamilia, lakini hata akina mrisho ngasa, na wachezaji wote
wanaosajiliwa azam,samba na yanga si haba kwa mishahara (kipato)
Lakini hata wanamuziki
,wale watakoa fanikiwa kama akina Diamond na Ally kiba , pia ndiyo iwe lengo,
kwani hiyo ndiyo njia ambayo hata akina , Chriss brown, Tiger , Lil wayne, Jay
z, Rick ross, Kid ink, Rihanna, Iggy azalea,Nick minaj , Yemi alade, nawengine
wengi, wanapiga pesa ndefu na kuishi maisha bora , ambapo na vijana toka iringa
wanaweza kufanikiwa kwa kiwango chao.
Lakini pia wachezaji
nyota wa soka kama vile , wayne rooney, Christian Ronaldo, Lionel messi,
Ibrahimovic, Benzema, Diago costa, Muller, Alex sanches, Kun aguero na wengine
wengi pesa wanayo piga ni ndefu mno. Sisi pia tunaweza kuwatengeneza vijana
wakafikia soka kuwa ni sehemu ya kuingiza kipto cha kutosha na hivyo kupunguza
tatizo la ajira. Naamini kwa haya machache wengi watakuwawamethibitisha sasa kuwa
Daidi Issa Masasi kitu cha ziada na ninastahili kukaliakiti cha ubunge iringe
mjini bila wasiwasi. Uvumi kwamba iringa kuna goliati, uta ishia kati ya
augusti na septemba kwa sababu hayupo huyo mtu , na kama kweli yupo ? Basi mimi
ndiye Daudi Issa Mohamedi Masasi
Asanteni..!
Tuzo ya nia yangu nampa marehemu mama wangu, Asha (paunu) salyuti
Goigoi Wapalila mjukuu wa sehongoli, maarufu sana mjini iringa enzi ya uhai
wake, Mama Mohammedi mwenye enzi mung ailaze pahala pema peponi aaamin.
No comments:
Post a Comment