Thursday, 8 October 2015

MAGAZETI LEO IJUMAA







MRADI WA UENDELEZAJI SEKTA YA MAZIWA AFRIKA YA MASHARIKI (EADD II)

Mkurugenzi wa Asas Dairies Ltd, Salim Asas Abri (aliyesimama) akitoa maelezo ya kiwanda cha kuzalisha maziwa na bidhaa zake kilichopo mkoani Iringa kwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Titus Kamani wakati ya ziara ya kutembelea nyanda za juu kusini kupitia mradi wa uendelezaji sekta ya maziwa afrika ya mashariki awamu ya pili.

Mradi wa uendelezaji sekta ya maziwa afrika mashariki (East Africa Dairy Development) ni mradi wa miaka mitano (2013-2018) unatekelezwa kwa awamu ya pili katika nchi za Kenya, Uganda na tanzania kwa mfumo wa kitovu cha maziwa (dairy hub).

Nchini tanzania mradi huu unatekelezwa katika mikoa ya Mbeya, Iringa na Njombe, ambao unatekelezwa kwa ubia-kongano (consortium partnership) kati yaa Heifer International (msimamizi mkuu wa mradi na kuongoza uzalishaji maziwa) kwa kushirikiana na Technoserve (biashara na masoko ya maziwa).







Mitamba katika shamba la Kibebe linalomilikiwa na Richard Phillips  lillilopo karibu na kijiji cha Tagamenda wilayani iringa.

Nyati maji (water buffaloes) katika shamba la Asas Dairy Ltd lililopo karibu na kijiji cha Igingilani wilaya ya Iringa Waziri wa maenedeleo ya mifugo pia alitembelea katika ziara yake.

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Titus Kamani (kushoto) akibalishana mawazo na Afisa mifugo Manispaa ya Iringa Dr. Augustino Nyenza.

Afisa mifugo Manispaa ya Iringa Dr. Augustino Nyenza (wa pili kushoto) akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi machinjio ya kisasa yalipo Ngelewale kwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Titus Kamani wakati ya ziara ya kutembelea Nyanda za Juu Kusini (southern highlands) kupitia mradi wa uendelezaji sekta ya maziwa afrika ya mashariki awamu ya pili.

Mkurugenzi wa Kibebe Farms Richard Phillips (katikati)akitoa salamu kwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi  Dkt Titus Kamani wakati ya ziara ya waziri huyo.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa (katikati) Amina Masenza akitoa taarifa ya maendeleo ya sekta ya mifugo kwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt Titus Kamani (wa pili kushoto) wakati ya ziara yake iliyoratibiwa na shirika la Heifer International kupitia Mradi wa Uendelezaji Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki (East Africa Dairy Development). (PICHA ZOTE NA FRIDAY SIMBAYA)

MPIGIE KURA MO DEWJI KUSHINDA TUZO YA HESHIMA BARANI AFRIKA #FAPOY2015



“NINAFURAHA KUKUARIFU KUWA NIMETEULIWA KUWANIA TUZO YA “ FORBES PERSON OF THE YEAR 2015” #FAPOY2015

KWA HESHIMA NA TAADHIMA NINAOMBA KURA YAKO; Bonyeza Link hii: [ ttp://t.co/8mPEDbghsB] KUNIPIGIA KURA ILI TUIPEPERUSHE BENDERA YA TANZANIA JUU ZAIDI NA KUIWAKILISHA VYEMA AFRIKA MASHARIKI.”


"I am humbled to be one of the nominees for Forbes Person of the Year and i hope to make Tanzania/East Africa & Africa Proud. Please share with your friends and cast your votes here: http://t.co/8mPEDbghsB 


IPC CHA ANDAA MDAHALO KWA WAGOMBEA



Mwenyekiti wa chama cha wanahabari mkoani Iringa (IPC) Frank Leonard ameongea na waandishi wa habari kuhusiana na maadalizi ya mdahalo kwa wagombea wote wa vyama vya siasa sita katika jimbo la iringa mjini.  (Picha na Friday Simbaya)

Hata hivyo amesema kwamba wagombea wote wa ngazi za ubunge watashiriki mdahalo utakaofanyika siku ya jumapili katika ukumbi wa highlands hall kuanzia saa sita mchana hadi saa tisa alasiri . 

Amesema kuwa vyama vya siasa vilivyothibitisha kushiriki ni pamoja na CCM, CHADEMA, ADC, ACT,DP NA CHAUSTA na katika vyama hivyo wabunge wameruhusiwa kuja na wanachama 50 kwa kila chama.

Aidha ametoa wito kwa wanachama wote ambao watafika katika ukumbi huo wasiwe na wasiwasi kutakuwa na ulinzi wa kutosha na kila mgombea ataweza kutoa sera zake.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...