Wanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Peramiho 'A' wilayani Songea, Mkoa wa Ruvuma wakiwa katika darasa lao na Mwalimu Katona wakiimba wimbo wa shule ikiwa ni siku ya pili tangu kuanza kwa muhula mwaka 2013.
Tuesday, 8 January 2013
WANACHAMA 150 WA CCM PERAMIHO WATIMKIA CHADEMA
Na
Friday Simbaya, Songea
Jumla
ya wanachama 150 wa Chama cha Mapinduzi (CCM), vijana kwa wazee wa Kata ya
Peramiho wamekata shauri na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) na kati yao 130 wamerudisha kadi za CCM na wengine 20 ni wanachama
wapya, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Namihoro sokoni, Wilaya ya
Songea (V) mkoani Ruvuma juzi.
Kada na mpigadebe wa CCM maarufu, Margret Ndomba (kushoto) akipeana mkono na Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa (NEC CHADEMA), Edson Mbogolo baada aliyakurudisha kadi tatu za CCM, yaani kadi ya UVCCM, kadi ya UWT na CCM wakati wa mkutano wa hadahra wa chama hicho uliyofanyika Namihoro katika Kata ya Peramiho Wilaya Songea, Mkoani Ruvuma juzi.
Miongoni mwa wanachama waliorudisha kadi za CCM na kuamua kujiunga na Chadema ni Mwenyekiti mstaafu wa CCM wa Tawi la Peramiho, Bruno Mwitumba pamoja na kada wa CCM Margret Ndomba aliyerudisha kadi tatu; kadi ya UVCCM, kadi ya UWT na CCM.
Akiwakabidhi
na kuwapokea wanachama hao, Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa (CHADEMA), Edson Oswald
Mbogolo alisema kuwa wanachama hao waliohamia Chadema wamefanya hivyo kwa
maamuzi sahihi kwa kuchagua maendeleo, na kuongeza kuwa wameamua kutoka ‘analojia
kwenda digitali.’
“Wananchi
hawa waliojiunga na Chadema kwenda ‘digitali kutoka analojia’ kwa maana ya
kutoka CCM kwenda Chadema kama nchi yetu na nchi
za Afrika Mashariki mzima ilivyoamia digitali wanajitambua…”, aliongeza Edson Mbogoro.
Alisema
kuwa mwaka 2014 utachukuliwa kama ni mwaka wa
Chadema na kipimo tosha cha kuchukua dola katika chaguzi za serikali za mitaa
kwa nafasi mbalimbali katika ngazi zote na hatimaye Uchaguzi Mkuu 2015.
Alidai
kuwa wananchi wa Kata ya Peramiho wameamua kujiunga na Chadema kwa sababu
Mbunge wao wa Jimbo la Peramiho, Jenister Mhagama amewatelekeza.
Aliwambia
wakazi wa Jimbo la Peramiho kujiunga na Chadema ili waweze kuunganisha nguvu kwa
pamoja kuondoa watawala pamoja na mbunge wa jimbo hilo .
“Ndugu
zangu wanaPeramiho siasa sio usanii kama
wanavyofanya kina Majuto kumbe siasa ni uhai wetu, siasa ni maisha yetu…”
alisisitiza mjumbe huyo wa kamati kuu taifa.
Naye
Katibu waChadema Wilaya ya Songea Mjini, Masumbuko Mbogolo alisema kuwa
wananchi wake kwa wanaume wa Jimbo la
Peramiho kuwa wanabudi ya kuchagua
upinzani kwa maendeleo ya jimbo lao, kwa sababu kwa muda mrefu jimbo hilo liko nyuma
kimaendeleo.
Alisisitiza
kuwa mahala ambapo wananchi wamechagua upinzani pana maendeleo kwa kutoa mifano
michache ya Moshi mjini, Karatu na
Kijiji cha Liweta ambacho kipo kilometa chache kutoka Peramiho, ambacho kina
maendeleo kwa sasa baada ya kuchagua upinzani na mwenyekiti wa serikali ya
kijiji hicho ni wa Chadema.
“Kijiji
cha Liweta ambacho kipo kilometa chache kutoa hapa Peramiho waliamua kuchagua
upinzani baada ya miaka mingi ya kutawaliwa na CCM, kwa sasa wananchi wa kijiji
hicho wana maendeleo, wamepata maji safi
na salama baada ya kuchimbiwa visima, wamechongewa barabara na wanasubiri
kujengewa zahanati kutokana na kelele za Chadema,” alisema Masumbuko Mbogolo.
Kuhusu
mbolea, Katibu wa Wilaya ya Songea Mjini alisema kuwa wananchi wa Jimbo la
Peramiho na kwingineko hawawezi kuwa na kilimo chenye tija kwa sababu gharama
za pembejeo na mbolea ziko juu ukilinganisha na Malawi na Zambia wakati wote
wanaagiza mbolea hizo kutoka China na Japan.
Alitoa
mfano kuwa, kule Malawi
mfuko moja wa mbolea unauzwa shilingi elfu nane tu wakati Tanzania mfuko mmoja wa mbolea unauzwa kati ya
shilingi elfu 65 hadi 70, wakati Malawi
na Zambia wanapitisha mbolea
kupitia Tanzania na wanalipa
kodi kwa Tanzania kwa
kupitisha mizigo yao .
Katika
hatua nyingine, Katibu huyo wa Wilaya ya Songea Mjini alipata nafasi ya
kufafanua maana ya rangi nne za bendera ya chama hicho (Chadema) kwa wananchi
wa Jimbo la Peramiho.
Alifafanua kuwa rangi nyeupe kwenye bendera ya
chama hicho ni alama na ishara ya amani, rangi nyeusi katika bendera hiyo ni
alama ya watu, rangi ya Bluu inaonyesha alama ya utajiri wa asili wa nchi ya
Tanzania na rangi nyekundu ni alama ya
damu iliomwagika kutoka kwa baadhi ya wapigania Uhuru wa nchi hii kama vile
Mkwawa na wengineo.
Mwisho
Subscribe to:
Posts (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
The most deadly form of tuberculosis is one that lies in wait inside the body for years, attacking at the first sign of weakness. Abou...