Walimu wa shule ya Msingi JJ Mungai Manispaa ya Iringa mkoani Iringa wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wao baada ya kupewa mgao wa maziwa na Kampuni ya Asas Dairies Ltd ya mjini Iringa jana. |
Watanzania waliungana na wenzao katika kuadhimisha Wiki ya Unywaji Maziwa ambapo kilele cha maadhimisho kilikuwa juni mosi mwaka huu.
Katika maadhimisho hayo, imebainika kuwa Watanzania bado wako nyuma katika unywaji wa maziwa ikilinganishwa na nchi nyingine kama vile Kenya.
Meneja wa miradi wa Asas Group of Companies Ltd Hassan Swedi kwa upande amewataka wananchi kujenga utamaduni wa kupenda kunywa maziwa kila siku badala ya kusubiri wang’atwe na nyoka au wadudu kutoa sumu mwiilini ama washauriwe na madaktari.
alisema kuwa watu wengi wamekuwa wavivu katika suala la unywaji wa maziwa ikilinganishwa na kasi wanayoitumia kwenye unywaji wa pombe ambapo baadhi yao wamekuwa mabingwa wa kushinda au kukesha baa.
Akaongeza kuwa viwango vinavyopendekezwa kimataifa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) ni lita 200 kwa mtu kwa mwaka wakati unyanji wa maziwa kwa mtu ni lita 47 kwa mwaka kitaifa.
Swedi aliwataka wananchi wa mkoani Iringa kuyatumia maadhimisho hayo kama darasa katika kujifunza mbinu bora za ufugaji wa ng’ombe wa maziwa na usindikaji wa maziwa kwa ajili ya kuinua kiwango cha upatikanaji wa maziwa hayo.
Kampuni ya Asas Dairies Ltd ilitumia maadhisho hayo kwa pakiti za 4,000 (sawa na lita 1,000) kwa wanafunzi wa shule mbali mbali za Manispaa ya Iringa, mkoani Iringa .
Meneja wa miradi huyo alisema kuwa maadhimisha ya mwaka huu yamelenga zaidi vijana hasa wanafunzi wa shule za msingi mjini Iringa na ndio sababu kampuni yake imelazimika kutoa msaada wa maziwa kwa wanafunzi.
Alisema kuwa kampuni hiyo inaamini kuwa iwapo shule zitaweka utaratibu wa kuhamsisha unyanji wa maziwa kupitia kamati za lishe bora kwa wanafunzi afya za wanafunzi hao zitakuwa bora na kiwango cha elimu kinaweza kuongezeka zaidi mashuleni.
Mbali ya unywaji wa maziwa kuhamasishwa zaidi mashuleni bado viongozi wa serikali wanapaswa kuanza kuhamasha unywaji wa maziwa katika ofisi hizo za umma badala ya kutumia maziwa kutoka nje ya nchi .
Hata hivyo, mkoa wa Iringa unashika nafasi ya tatu kwa kuwa na watoto wenye utapiamlo kwa kuwa na asilimia 51.3 baada ya mikoa ya kagera (51.9)na Njombe wenye asilimia 51.5.
Maadhimisho ya Wiki ya Maziwa inayoadhimishwa Kitaifa katika Mkoa wa Kagera katika Uwanja wa Kyakailabwa nje kidogo ya mji wa Bukoba kuanzia tarehe 28 Mei, 2017 hadi tarehe 1Juni, 2017.
Malengo ya Maadhimisho ya Wiki ya Maziwa Kitaifa inalenga kuelimisha wananchi na umma juu ya matumizi ya maziwa kama chakula bora kwa watu wa rika zote na faida za maziwa katika kujenga afya ya binadamu.
Kaulimbiu ya Maadhimisho hayo ni “Kunywa Maziwa Furahia Maisha“. Maadhimisho haya yatakuwa ya 20 mfululizo kuadhimishwa nchini ambapo yalianza kuadhimishwa kuanzia mwaka 1998 na mwaka jana yaliadhimishwa Mkoani Njombe.