mwakilishi wa Kampuni iliyoshinda zabuni hiyo Home Africa Investment Corporation ya jijini Dar es salaam |
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Ndugu, Omary Mkangama, |
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mheshimiwa Alex Kimbe, |
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imesaini mkataba wa ujenzi wa soko la kisasa katika Kata ya Mlandege wenye thamani ya shilingi Bilioni 3,725,236,998/= chini mradi wa kusaidia uendelezaji wa mji( Urban Local Government Support Programme unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.
Mkataba huo umesainiwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mheshimiwa Alex Kimbe, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa, Omary Mkangama, mwakilishi wa Kampuni iliyoshinda zabuni hiyo Home Africa Investment Corporation ya jijini Dar es salaam chini ya usimamizi wa Mwanasheria wa Manispaa ya Iringa Ndugu, Charles P. Lawisso , wakuu wa Idara na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali.
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ni miongoni mwa Mamlaka za Serikali za Mitaa( Miji& Manispaa zinazotekeleza mradi wa kusaidia uendelezaji wa Miji ( Urban Local Government Support Programme) unaofadhililiwa na Benki ya Dunia.
Soko hilo la kisasa linatarajiwa kuwa la ghorofa moja likiwa na maduka kuzunguka soko hilo na hudumu zote zitapatikana katika soko hilo. Mkataba huu ni wa muda wa miezi sita ya utekelezaji na unatarajiwa kuanza mapema wiki hii.