KUMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imekabidhi kompyuta kumi (10) pamoja na kifurushi cha intaneti ya bure yenye kasi ya 2Mbps kwa muda wa miezi sita vyote vikiwa na thamani ya 20,197,600/- kwa ajili ya Iringa Secondary School Internet Library (ISSIL).
Kampuni ya simu hiyo ya
kizalendo ambayo inatoa huduma mbalimbali
za mawasiliano nchi imetoa misaada hiyo Global Outreach Tanzania ili
kuunga mkono mradi wa maktaba mtandao (intaneti) katika kuboresha mfumo wa
elimu nchini.