Monday, 24 August 2015

Wanafunzi waaswa kuzingatia elimu






Na Friday Simbaya, Iringa

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu amewaasa wanafunzi wa kidato cha nne kuzingatia elimu na kusoma kwa bidii, kwa kuwa elimu ndiyo mkombozi wa maisha yao.



Rai hiyo aliitoa alipokuwa akitoa nasaha katika mahafali ya kidini kwa wanafunzi zaidi ya 50 wa umoja wa wakikristo wa wanafunzi Tanzania (UKWATA) yaliyofanyika jana katika Kanisa la KKKT Usharika wa Nyamhanga mjini Iringa.

Ibada maalum ya kuwaombea wanafunzi hao kutoka shule za sekondari za Efatha, Ipogolo, Tagamenda na Cagrielo katika Manispaa ya Iringa iliongozwa na Mchungaji Nuru Makweta kwa kushirikiana na Mchungaji Yekonia Koko ambaye pia mlezi wa UKWATA mkoa wa Iringa.

Mgeni rasmi Jesca Msambatavangu aliwataka wanafunzi hao wanapopata fursa ya kusoma waoneshe bidii darasani ili wajikomboe ili kutimiza malengo yao ya baadaye.

“Lazima muwe na maono ya mbali yakutaka kuwa kina nani hapo baadaye katika taifa hili,”alisisitiza Msambatavangu.

Mbali na kujikomboa, Msambatavangu alisema juhudi katika masomo yao zitasaidia kujiwekea misingi imara wa kujitegemea hapo baadae.

Katika hafla hiyo, mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Iringa wamekabidhiwa wanafunzi misaada shilingi laki nane pamoja vyeti vya uanacha wa UKWATA. 

Aliwaasa wanafunzi wa kidato cha nne shule za sekondari za Efatha, Ipogolo, Tagamenda na Cagrielo ambao wapo kwenye umoja huo (UKWATA) kusoma kwa bidii ili kukabiliana na changamoto za maisha hapo baadaye.

Msambatavangu alikuwa alikuwa akiwapongeza kabla ya kuanza kwa mitihani yao hapo tarehe 02.11.2015.



MSINDAI KUGOMBEA UBUNGE SINGIDA MJINI KWA TIKETI YA CHADEMA



Aliyekuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida na Mwenyekiti wa wenyeviti CCM mikoa ya Tanzania, Mgana Izumbe Msindai, akikabidhiwa fomu na msimamizi wa uchaguzi halmashauri ya manispaa ya Singida, Joseph Mchina ya kugombea ubunge jimbo la Singida mjini kupitia tiketi ya Chadema.

LOWASSA NDANI YA DALADALA

Mgombea Urais wa Chadema kupitia UKAWA, Edward Lowassa akiwa kwenye daladala asubuhi hii kuangalia kero za wananchi maeneo ya Gongo la mboto kuelekea Chanika.

UN KUBORESHA VYOO VYA SHULE 10 KILIMANJARO



Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisalimiana na walimu mara baada ya kuwasili katika shule ya msingi Kiboriloni kwa ajili ya kushiriki zoezi la kuweka msingi kwenye ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule hiyo. Kulia kwake ni Afisa Tawala Mkuu katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Omari Msuya. (Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)

Na Mwandishi Wetu, Moshi

MASHIRIKA ya Umoja wa Mataifa nchini, yatasaidia kuboresha vyoo katika shule 10 zilizopo katika manispaa ya Moshi na wilaya ya Moshi vijijini.

Hayo yalisemwa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, kwenye hafla ya kuweka msingi kwa ajili ya ujenzi wa matundu 18 ya choo katika shule ya msingi Kiboriloni.

Alisema pamoja na mashirika hayo kusaidia uboreshaji huo kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa, amewataka watoto kukumbuka kutunza mazingira na miili yao kama sehemu ya mazingira hayo.

MAMIA WAJITOKEZA KATIKA UFUNGUZI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU ZA CCM


Wiliam ngereja ajitokeza katika kumunga mkono Magufuli katika ufunguzi wa Kampeni leo jijini Dar es Salaam.
Vijana wakiwa wamebebana ili waweze kuona mbele katika ufunguzi wa kampeni za chama cha mapinduzi leo katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam.


Furaha imetawala kwenye mioyo ya wanaCCM kama inavyoonekana kwenye taswira yetu hapo katika ufunguzi wa kampeni za chama cha Mapinduzi CCM kwenye viwanja vya jangwani leo jijini Dar es Salaam.
Mzee akiwa amevaa Picha ya Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,John Magufuli leo katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam.
Vijana wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali.

Wananchi waliojitokeza katika ufunguzi wa kampeni za Chama cha Mapinduzi (CCM) katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam leo. Picha na Avila Kakingo na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.

MAALIM SEIF SHARIF HAMAD, ACHUKUA FOMU KUWANIA URAIS WA ZANZIBAR


Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akionyesha mkoba wenye Fomu za kuwania nafasi hiyo, leo Agosti 24, 2015, baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, (ZEC), kwenye Ukumbi wa Salama, Bwawani, Zanzibar.


Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha akimkabidhi Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, Fomu za kuwania nafasi hiyo, leo Agosti 24, 2015, kwenye Ukumbi wa Salama, Bwawani, Zanzibar.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimpongeza Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, baada ya kuchukua Fomu za kuwania nafasi hiyo, leo Agosti 24, 2015, kwenye Ukumbi wa Salama, Bwawani, Zanzibar.

Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Agosti 24, 2015, kwenye Ukumbi wa Salama, Bwawani, Zanzibar. Kulia kwake ni Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha akisoma taarifa ya muongozo kwa Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, wakati wa kuchukua Fomu ya kuwania nafasi hiyo, leo Agosti 24, 2015, kwenye Ukumbi wa Salama, Bwawani, Zanzibar. Maalim Seif alisindikizwa na Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa,Mgombea Mweza, Dkt. Juma Haji Duni pamoja na viongozi wengine wanaounda UKAWA

MFUKO WA PENSHENI WA PSPF WAFUNGUA RASMI MASHINDANO YA MPIRA WA MIGUU


Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Delphin Richard akizungumza na madereva bodaboda wa Kipunguni 'B' kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko wa Pensheni wa PSPF hasa katika uchangiaji wa hiari ambapo mtu yeyote anaweza kujiunga

Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Josephat Sylvery Tirumanywa akizungumza na wananchi mbalimbali waliofanikiwa kuhudhuria ufunguzi wa mashindano ya mpira wa miguu kwa madereva bodaboda wakiume maeneo ya Kipunguni 'B' katika manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam

Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Ismail Juma akitoa maelezo ya kina kuhusu faida na huduma zitolewazo na Mfuko wa Pensheni wa PSPF hasa katika uchangiaji wa hiari, ambapo mtu yeyote anaweza kujiunga na kunufaika na huduma mbalimbali zilizo katika hifadhi ya jamii ya (PSPF), akiongea na madereva wa bodaboda wa Kipungunu 'B' wakati wa ufunguzi wa mashindano ya mpira wa miguu kwa madereva hao.

Delphin Richard Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akisalimiana na muamuzi wa mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Madereva wa Bodaboda wa Kipunguni 'B' ambapo mfuko wa PSPF imedhamini mashindano hayo. Katikati ni Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Josephat Sylvery Tirumanywa.



Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Josephat Sylvery Tirumanywa akitambulishwa wachezaji

Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Eliachi Remmy akisalimiana na wachezaji katika ufunguzi wa ligi ya madereva bodaboda.

Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Delphin Richard akizungumza mmoja wa wazee kuhusu Mfuko wa Pensheni wa PSPF hasa katika uchangiaji wa hiari, ambapo mtu yeyote anaweza kujiunga na kunufaika na huduma mbalimbali zilizo katika hifadhi ya jamii ya (PSPF)

Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Ismail Juma akimjazia fomu ya Uchangiaji wa Hiari mmoja wa madereva wa Bodaboda wa Kipunguni B wilaya ya Ilala jijini Dar mara baaada ya kupata elimu na kuridhia na huduma za mfuko huo.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...