Na Friday Simbaya, Iringa
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu amewaasa wanafunzi wa kidato cha nne kuzingatia elimu na kusoma kwa bidii, kwa kuwa elimu ndiyo mkombozi wa maisha yao.
Rai hiyo aliitoa alipokuwa akitoa nasaha katika mahafali ya kidini kwa wanafunzi zaidi ya 50 wa umoja wa wakikristo wa wanafunzi Tanzania (UKWATA) yaliyofanyika jana katika Kanisa la KKKT Usharika wa Nyamhanga mjini Iringa.
Ibada maalum ya kuwaombea wanafunzi hao kutoka shule za sekondari za Efatha, Ipogolo, Tagamenda na Cagrielo katika Manispaa ya Iringa iliongozwa na Mchungaji Nuru Makweta kwa kushirikiana na Mchungaji Yekonia Koko ambaye pia mlezi wa UKWATA mkoa wa Iringa.
Mgeni rasmi Jesca Msambatavangu aliwataka wanafunzi hao wanapopata fursa ya kusoma waoneshe bidii darasani ili wajikomboe ili kutimiza malengo yao ya baadaye.
“Lazima muwe na maono ya mbali yakutaka kuwa kina nani hapo baadaye katika taifa hili,”alisisitiza Msambatavangu.
Mbali na kujikomboa, Msambatavangu alisema juhudi katika masomo yao zitasaidia kujiwekea misingi imara wa kujitegemea hapo baadae.
Katika hafla hiyo, mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Iringa wamekabidhiwa wanafunzi misaada shilingi laki nane pamoja vyeti vya uanacha wa UKWATA.
Aliwaasa wanafunzi wa kidato cha nne shule za sekondari za Efatha, Ipogolo, Tagamenda na Cagrielo ambao wapo kwenye umoja huo (UKWATA) kusoma kwa bidii ili kukabiliana na changamoto za maisha hapo baadaye.
Msambatavangu alikuwa alikuwa akiwapongeza kabla ya kuanza kwa mitihani yao hapo tarehe 02.11.2015.
No comments:
Post a Comment