Meneja wa Takwimu za Watu na Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Sylvia Meku (katikati) akiwa na wadau wakionesha kitabu cha uwiano wa takwimu za wanawake na wanaume wakati wa hafla ya kuzindua kitabu hicho iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Habari na Ulaghibishi wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids), Jumanne Issango, Ofisa wa Takwimu kutoka nchini Sweden, Cath Craiger, Mtakwimu kutoka Sweden, Ana Morkuda na Mwanahabari Philip..Kitabu hicho kimeandikwa na wanafunzi watano kutoka Tanzania waliopata mafunzo ya miezi 11 nchini Sweden.
Mada kuhusu mafunzo hayo zikitolewa kabla ya uzinduzi.
Wafadhili wa mafunzo hayo kutoka nchini Sweden wakifuatilia mada kuhusu mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa Habari na Ulaghibishi wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids), Jumanne Issango (kushoto) na Meneja wa Takwimu za Watu na Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Sylvia Meku ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo wakifuatilia kwa karibu hafla hiyo.
Mtakwimu kutoka nchini Sweden, Cath Craiger akizungumza kwenye mkutano huo.
Mtakwimu kutoka Sweden, Ana Morkuda akichangia jambo
Mada zikiendelea kutolewa.
Mhadhiri kutoka Chuo cha Takwimu cha Afrika Mashairiki, Chisker Masaki (kushoto), akizungumzia mafunzo ya takwimu waliopata nchini Sweden.
Mratibu wa masuala ya Jinsia wa Tacaids, Jacob Kayombo akichangia jambo katika mkutano huo.
Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Tacaids, Jerome Kamwela akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Ofisa kutoka HakiElimu, Joyce Mkina akichangia.
Washiriki wa mafunzo hayo (walioketi) wakiwa katika picha ya pamoja na wageni waalikwa. Kutoka kulia Ofisa kutoka HakiElimu, Joyce Mkina, Mhadhiri kutoka Chuo cha Takwimu cha Afrika Mashairiki, Chisker Masaki, Ofisa wa Jinsia wa Tacaids, Judith Luande, Philbert Mrema kutoka NBS na Mariam Kitembe kutoka NBS.
Picha ya pamoja
Na Dotto Mwaibale
WANAUME wameonekana kuwa wengi katika nafasi mbalimbali ukilinganisha na wanawake.
Hayo yamebainishwa na Mhadhiri wa Chuo cha Takwimu Afrika Mashariki, Chisker Masaki wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo katika hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha Uwiano wa Taarifa za Takwimu kwa Wanawake na Wanaume Tanzania.
Alisema kitabu hicho kimeandaliwa na washiriki wa mafunzo ya ukusanyaji wa taarifa za takwimu kutoka Tume ya kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Hakielimu , Ofisi yaTaifa ya Takwimu (NBS) na Chuo cha Takwimu cha AfrikaMashariki, chini ya wakufunzi wa masuala ya ukusanyaji wa taarifa kutoka nchini Sweden.
Masaki alisema utafiti unaonesha kuwa kuna tofauti kubwa za uwiano kati ya mwanamke na mwaume katika nyanja za kimaendeleo na kijamii, ambapo maeneo mengi yanaonekana kutwaliwa na wanaume kuliko wanawake.
Akitolea mfano upande wa elimu kuanzia shule za msingi hadi chuo kikuu wasichana wanaoandikishwa hadi kufikia chuo kikuu ni wachache ukilinganisha na wavulana,watu wenye nafasi nzuri maofisini hasa ngazi za Ukurugenzi na mameneja wengi ni wanaume ukilinganisha na wanawake,viongozi wa kisiasa mfano mawaziri na wabunge wanawake ni wachache ukilinganisha na wanaume.
Alisema pamoja na uwiano huo wa wanaume kuwa kiwango kikubwa katika masuala ya maendeleo wanawake wamekuwa wakichukua nafasi kubwa katika kuathirika na maambukizi ya VVU na UKIMWI.
Mafunzo hayo ya ukusanyaji wa taarifa yalianza tangu mwaka 2016 mwezi Mei hadi Machi 2017 ambapo mafunzo yalifanyika nchini Sweden ni ukusanyaji wa taarifa pamoja na uandaaji wake kitabu ukafanyika Tanzania.