Monday, 19 December 2016

KAIMU KATIBU MKUU UVCCM TAIFA SHAKA AFANYA ZIARA WILAYANI NGARA



Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (MNEC)akizungumza na ajumbe wa Baraza la UVCCM pamoja na Wajumbe wa Sekretariet ya CCM Wilayani Ngara Katika Kikao Cha Ndani Kilicho Fanyika katika Ukumbi wa Engubenako Wilayani Ngara.

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akiwasili katika Kijiji Cha BENACO Wilayani Ngara, Shaka yupo kwa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM 2015-2020



Mwenyekiti wa uvccm Mkoa wa Kagera Bw. Yahya Kateme akizungumza kumkaribisha Ndg: Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka Kuzungumza na Wajumbe wa Baraza la UVCCM pamoja na Wajumbe wa Sekretariet ya CCM Wilayani Ngara



Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (MNEC)akizungumza na Wajumbe wa Baraza la UVCCM pamoja na Wajumbe wa Sekretariet ya CCM Wilayani Ngara Katika Kikao Cha Ndani Kilicho Fanyika katika Ukumbi wa Engubenako Wilayani Ngara


Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akizindua Mradi wa kikundi cha Vijana wajasiliamali cha Ufugaji wa Nyuki na Shamba la Upandaji wa Miti katika kijiji cha Nyaruku Wilayani Ngara.



Mwandishi wa Gazeti la Uhuru Bw. Antari Sangali pamoja na wazee wa kijiji cha Mumilamila Wilayani Ngara wakimsikiliza kwa makini Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (MNEC)alipo kua akigawa Vyeti kwaajili ya Matibabu ya Bure kwa wazee.


MTOTO AWAKIMBIA WAZAZI WAKEKUKWEPA KUKEKETWA


Kamanda wa Polisi Ilala, Salum Hamdun 









Na Dotto Mwaibale


MTOTO mwenye umri wa miaka 12 ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kivule Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam jina lake linahifadhiwa ameelezea jinsi alivyofanikiwa kuwatoroka wazazi wake ili asikeketwe.


Mtoto huyo hivi sasa analelewa na msamaria mwema baada kufungua kesi Kituo cha Polisi cha Stakishari Ukonga kufuatia kufikishwa kituoni hapo kwa ajili ya kujisalimisha na kuelezea madhila aliyotaka kufanyiwa.

Wakati mtoto huyo akijisalimisha katika kituo hicho kuna taarifa za ndani kuwa kuna mpango wa kuwakeketa watoto 85 wenye umri kuanzia miaka 12 hadi 15 katika manispaa hiyo ambapo watoto zaidi ya 30 wanadaiwa kukeketwa.


Akizungumza na mtandao wa www.habari za jamii.com mtoto huyo alisema hawezi kurudi tena nyumbani kwao kwa kuhofia kupigwa na kukeketwa ambapo ameomba msaada wa hifadhi kutoka kwa watanzania.


"Baada ya baba yangu kufariki nyumbani kwetu Tarime tulikuja na mama hapa Dar es Salaam kwa kaka yake Chacha Nyanchiri anayeishi Kitunda Kivule karibu na Shule ya Msingi Misitu" alisema mtoto huyo.


Alisema katikati ya wiki iliyopita alifika bibi yake mzaa baba yake aliyemtaja kwa jina la Boke na kuwaambia yeye na wenzake wajiandaa kwenda kukeketwa.


Mtoto huyo alisema kwamba siku ya alhamisi majira ya saa mbili usiku wakiwa nyumbani kwa mjomba wao anakoishi na mama yake alifika bibi mzaa mama yake aliyemtaja kwa jina moja la Debora huku akiwa ameongozana na mama yake Happyness na kuwaambia yeye na watoto wengine wawili wa mama yake mkubwa wakaoge ili waende kukeketwa.


Alisema ili kukwepa kukeketwa alipokwenda bafuni alifanikiwa kutoka na kupita njia nyingine na kufanikiwa kuwatoroka wazazi wake na kwenda kujificha kwenye pagala na ilipofika saa tatu usiku alifika eneo la kwa Mpemba akielekea darajani ambapo alikutana na dada mmoja aliyemsimulia mkasa huo.


Alisema dada huyo alimchukua hadi nyumbani kwake ambako alilala na siku iliyofuata alimpeleka kituo cha Polisi cha Stakishari kwa ajili ya usalama wake.


Mmoja wa wakazi wa eneo hilo ambaye alikataa kutaja jina lake alisema kuna mpango wa kuwakeketa watoto 85 kabla ya kuisha kwa mwaka huu wa 2016 na kuwa karibu watoto 30 wamekwisha keketwa.


Alisema shughuli hiyo inasimamiwa na wazee wa kimila wa kabila la kikurya na kuwa ngariba mkuu wa kazi hiyo ya kukeketa watoto hao yupo eneo la Nyamuhanga na kuwa baada ya kukeketwa ufanyiwa sherehe kwa siri katika baadhi ya nyumba zilizopo jirani na ngariba huyo.

Mwenyekiti wa Serikali wa mtaa anaoishi mtoto huyo, Dominick Mlimi alisema hana taarifa ya mtoto huyo kutoweka nyumbani kwao.

"Jana niliwaona baadhi ya watoto wa kike wa familia ya Nyanchiri wakiwa hapo barabarani lakini kuhusu kutoweka kwa mtoto huyo kwa kuhifia kukeketwa sijazipata" alisema Mlimi.

Mke wa Chacha Nyanchiri ambaye anaishi na mtoto huyo Regina Wilison alikiri mtoto huyo kuondoka usiku baada ya kufika nyumbani hapo bibi yake na mama yake ingawa alisema hawakutoa taarifa kwa mtu yeyote ya kutoweka kwake.

"Mwenye mamlaka ya mtoto huyo ni mama yake ambaye ametoka asubuhi kwenda kumtafuta mtaani mimi sihusiki naye na wala sijui walichomuambia ingawa siku zote tulipokuwa tukizungumzia kuhusu kukeketwa mtoto huyo alikuwa akionesha hofu" alisema Wilison.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Salum Hamdun alisema hakuwa na taarifa kuhusu tukio hilo ingawa aliahidi kuwasiliana na wasaidizi wake ili kulifuatilia na kutoa taarifa kamili.

Mtoto huo alisema watoto wenzake waliofanyiwa vitendo hivyo bado wapo majumbani mwao wakijiuguza majeraha na kama vyombo vya usalama vitahitaji kwenda kuwaonyesha walipo yupo tayari. 

Taarifa ambazo tumezipata jana kutoka kwa baadhi ya wananchi wanaoishi jirani na nyumba aliyokuwa akiishi mtoto huyo na mama yake zimeeleza kuwa polisi walifika katika nyumba hiyo na kumkamata Regina Wilson, mama ya mtoto huyo Happyness na watu wengine wawili na kupelekwa kituo cha polisi Stakishari Ukonga jijini Dar es Salaam kwa mahojiano.

RC MASENZA TELLS OFF RAPE AND SODOMY CULPRITS





By Friday Simbaya, Iringa

Iringa Regional Commissioner (RC), Amina Masenza has told off rape and sodomy persistently arises in society and warned that such acts should not happen again in 2017. 

Masenza made the statement on Monday while speaking to journalists at her office, where she also used the opportunity to wish the citizens of Iringa region blessed Christmas and New Year in 2017. 

RC has also directed the security organs to work and identify the perpetrators and bring them to the course of justice. 

She also asked the citizens of Iringa Region to protect children against rape to young children. 

"It is our duty to ensure we are all completely eradicating all actions that contributes to breach of peace in our region of Iringa and the country in general," Masenza said. 

In addition, she asked the citizens of Iringa Region to ensure they maintain peace and unity to the region continue to have peace and calm. 

"I would like to wish you a good feast of Christmas and New Year 2017 with abundant prosperity. I beg you to make sure you celebrate these holidays in peace, security and stability, "she said. 

She said the government would ensure the protection and safety are made available throughout the festival because experience shows that in the holiday season people do not like to see peace and stability of the region by using this period to commit a crime. 

Amina Maenza is the 21st Iringa Regional Commissioner since the introduction of this region in 1964, where the 1st Iringa Regional Commissioner was Philemon Muro (1964-1968). 

Meanwhile, the governor has called on citizens to make better use of rain to grow crops to ensure food security. 

She said that in areas that receive very little rainfall particularly in Mahenge and Isimani areas to plant crops that are drought resistance. 


In addition, RC has reminded citizens to plant trees in the rainy season in that region have good weather for growing trees.

RC MASENZA: VITENDO VYA UBAKAJI VISITOKEE TENA 2017








Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amani Juma Masenza akiongea na wananchi wa Mkoa wa Iringa kupitia vyombo vya habari kwa kuwatakia heri katika sherehe za Noeli na Mwaka Mpya 2017 leo ofisini kwake. (Picha na Friday Simbaya)




IRINGA: Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza amekemea vitendo vya ubakaji na ulawiti vinavyoendelea kujitokeza katika jamii na kuonya kwamba vitendo hivyo visitokee tena mwaka 2017. 


Mkuu mkoa huyo alisema hayo leo (Jumatatu) wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake, ambapo alitumia pia fursa ya kuwatakia wananchi wa Mkoa wa Iringa heri katika Noeli na Mwaka Mpya 2017.


Masenza ameviagiza vyombo vya dola vifanye kazi ya kuwabaini wahusika na kuwafikisha kwenye mkondo wa sheria.


Pia, mkuu huyo aliwaomba wananchi wa Mkoa wa Iringa kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vya ubakaji kwa watoto wadogo.


“Ni wajibu wetu sote kuhakikisha tunatokomeza kabisa vitendo vyote vinavyopelekea uvunjifu wa amani katika mkoa wetu wa Iringa na nchi kwa ujumla,” alisema Masenza.


Aidha, mkuu huyo aliwaomba wananchi wa Mkoa wa Iringa kwa umoja wahakikishe wanasimamia na kudumisha ulinzi na usalama ili mkoa uendelee kuwa na amani na utulivu.


“Napenda kuwatakia sikukuu njema ya Noeli na Mwaka Mpya 2017 wenye mafanikio tele. Ninawasihi kuhakikisha mnasherehekea sikukuu hizi kwa amani, usalama na utulivu,” alisema.


Alisema kuwa serikali itahakikisha ulinzi na usalama vinakuwepo kipindi chote cha sikukuu kwa sababu uzoefu unaonesha kuwa katika majira ya sikukuu watu wasiopenda kuona amani na utulivu wa mkoa hutumia majira haya kufanya uhalifu.


Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza ni wa 21, tangu kuanzishwa kwa mkoa huu mwaka 1964, ambapo Mkuu wa Mkoa wa Iringa alikuwa Philemon Muro (1964-1968).


Wakati huohuo, mkuu wa mkoa ametoa wito kwa wananchi kutumia vizuri mvua zinazoendelea kunyesha kwa kuhakikisha wanapanda mazao ili kujihakiishia uhakika wa chakula.


Alisema kuwa katika maeneo yanayopata mvua chache hususan Mahenge na Isimani wapande mazao yanayovumilia ukame.


Aidha, mkuu wa mkoa huyo aliwakumbusha wananchi kupanda miti katika msimu huu wa mvua kwa kuwa mkoa una hali ya hewa nzuri inayostawisha miti.

KIKAO CHA TATHMINI YA MAONESHO YA UTALII KARIBU KUSINI KINAENDELEA...



Mjumbe na Mmliki wa Hilltop Lodge iliyopo karibu na Hifadhi ya Wanyampori Ruaha (RNP), Alban Lutambi akichangia mada wakati wa Kikao cha Tathmini Ya Maadhimisho Ya Kitaifa Ya Siku Ya Utalii Duniani Pamoja Na Maadhimisho Ya Utalii Karibu Kusini kulichofanyika mjini Iringa Leo. (Picha Na Friday Simbaya)









Wajumbe wakifuatilia kikao cha tathmini ya maonesho ya utalii karibu kusini kinachofanyika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mjini Iringa.

Researchers, Scientists and Developers Urged To Invest In Climate Data


WWF Tanzania’s Country Director Dr. Amani Ngusaru  is making a speech on Friday last week during the WWF - Ruaha Water Program-SWAUM exit workshop held in Njombe Region. (PHOTO: FRIDAY SIMBAYA)






 NjombeWWF Tanzania’s Country Director Dr. Amani Ngusaru is calling on researchers, scientists and developers to create data-driven simulations to help plan for the future and to educate the public about the vulnerability of climate change, hence help farmers to plan for their future.

Dr. Ngusaru made the disclosure on Friday last week during the WWF - Ruaha Water Program-SWAUM exit workshop held in Njombe Region.

He said that this effort will help give communities across the country the information and tools they need to plan for current and future climate impacts.

He said that farmers need to have right information about weather and climate so that they can know when to plant their fields because at the moment farmers in the country don’t know exactly what to do.

He said farmers are confused because they don’t when the rains are coming, they don't know when to cultivate and to plant but with the investment in climate data initiative (CDI) it will help them to plan for current and future climate impacts. 

WWF in collaboration with Care International are intending to implement Intensive Farming (IF) project in the Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania (SAGCOT).

SAGCOT’s objective is to foster inclusive, commercially successful agribusinesses that will benefit the region’s small-scale farmers, and in so doing, improve food security, reduce rural poverty and ensure environmental sustainability.

So, agricultural intensification and mechanization system is aimed to maximize yields from available land through various means, such as heavy use of pesticides and chemical fertilizers. 

Intensive farming practices produce more and cheaper food per acre and animal, which has helped feed a booming human population and may prevent surrounding land from being converted into agricultural land.

However, WWF Tanzania has been working in the Great Ruaha River catchment with a focus on promoting and improving integrated water resources management since 2002. 

Throughout the intervening period however the once perennial Great Ruaha River (GRR) has run dry in the dry season for progressively longer periods.

Throughout the period 2011-2016 WWF Tanzania has been piloting the SWAUM programme – Sustainable Water Access, Use and Management. 

SWAUM was explicitly framed and designed to address a situation – shortfalls in water governance in the GRR catchment – that was understood to be ‘complex’ (i.e. widespread conflicts and disagreements, knowledge gaps and uncertainties, and weak organizational capacity).

And has sought to identify and address the institutional constraints, within and between both formal organizations and local communities. 

Lack of awareness or acknowledgment of these strategic constraints, and of any commensurate response, considerably weakened or undermined the effectiveness and potential sustainability of earlier management and technical initiatives.

SWAUM’s empirical findings are that there are systemic shortcomings in aspects of integration critical to the governance system – the ‘critical dimensions of integration’ (CDIs) – and given the continuing deference to IWRM as the governance model in the Rufiji Basin IWRMD Plan. 

It is said that unless these shortcomings are addressed, the pattern of governance failure will not be broken, nor the associated drying of the GRR reversed.

RC IRINGA AWATAKIA WANANCHI HERI YA NOELI NA MWAKA MPYA 2017


Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amani Juma Masenza akiongea na wananchi wa Mkoa wa Iringa kupitia vyombo vya habari kwa kuwatakia heri katika sherehe za Noeli na Mwaka Mpya 2017 leo ofisini kwake. (Picha na Friday Simbaya)




WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...