Wednesday, 14 February 2018

Mama Samia aahidi kupunguza msongamano hospitali ya Mafinga








Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali imeanza kupanua vituo vya afya nchini pamoja na kuboresha huduma za matibabu ili kupunguza msongamano wa watu katika hospitali za wilaya. 

Mama Samia alitoa kauli hiyo hivi karibuni alipotembelea na kuweka jiwe la msingi na kukagua maendeleo ya upanuzi wa Kituo cha Afya Ihongole katika Kijiji cha Ihongole nje kidogo ya Mji wa Mafinga, wilayani Mufindi mkoani Iringa. 

Alisema kuwa Serikali itaendelea kutoa kipaumbele katika boresha utoaji wa huduma afya katika vituo vya afya katika wilaya ili kupunguza msongamano mkubwa uliopo kwenye hospitali za wilaya pamoja nza mikoa. 

“Tukishapunguza msongamano madaktari wetu watafanya kazi kwa uhakika zaidi na kwa umakini mkubwa,” aliongeza makamu wa rais. 

Hata hivyo, makamu wa rais halmashauri ya mji wa mafinga, wilayani Mufindi kwa kutumia fedha vizuri zilizotoalewa na serikali kwa ajili ya shughuli za upanuzi wa kituo cha Ihongole. 

Awali akitoa taarifa ya mradi wa upanuzi wa kituo cha afya Ihongole, Mkugurenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Saada Mwaluka, alisema Kituo cha Afya Ihongole kilianza kutoa huduma mwaka 2008 ambapo kilikuwa kinahudumia wastani wa watu 5,000 kwa mwaka. 

Kwa sasa kinahudumia wastani wa watu 26,032 kwa mwaka ikiwa ni ongezeko la wastani wa watu 21,032 kutoka katika kata ya Boma na kata jirani za Kinyanambo, Changarawe na Isalavanu. Mradi wa upanuzi wa Kituo ulianza mwezi Novemba 2017. 

Alisema kuwa Mradi huu ni juhudi za Serikali katika kuhakikisha inasogeza huduma za Afya kwa wananchi yanafikiwa. 

Mawluka alisema kuwa lengo la mradi huo ni kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa kuimarisha Miundombinu katika kituo ili kiweze kutoa huduma za upasuaji wa dharura na huduma ya kuongeza damu. 

Alisema kuwa ili kufanikisha hilo, mradi umelenga kuongeza majengo ya Upasuaji, Maabara, wodi ya Wazazi, nyumba ya Mtumishi na kuhifadhia Maiti pamoja na kufanya ukarabati wa majengo ya zamani. 

Mwaluka alisema upanuzi wa majengo ya kituo cha afya pia utasaidia kuboresha utoaji wa matibabu katika kituo hicho cha Ihongole na hatimaye kupunguza msongamano wa hospitali ya wilaya Mafinga. 

Alisema kuwa Ujenzi na ukarabati wa kituo hiki cha Afya, unaotarajiwa kukamilika wakati wowote kuanzia sasa, baada ya serikali kutoa kiasi cha Shilingi Milioni saba na ishirini (720) kwa lengo la kuimarisha miundombinu ya kituo hicho ili kiweze kukidhi haja ya kutoa huduma bora za Afya kwa zaidi ya Wananchi. 

Mwaluka alisema ujenzi na ukarabati wa kituo, utatekelezwa kwa mfumo wa (Force Account) ambapo, Halmashauri itatumia Mafundi wenyeji watakaothibitishwa kuwa na uwezo unaokubalika wa kutekeleza jukumu hilo. 

Halmashauri ya Mji Mafinga ina jumla ya wakazi 71,641 kati yao wanaume ni 34,522 na wanawake 37,119 (Sensa ya watu na makazi 2012). 

Halmashauri ina jumla ya vituo 21 vya kutolea huduma za Afya, ikiwemo Hospitali 1, vituo vya Afya 5 (2 vya serikli na 3 visivyo vya Serikali) na zahanati 15 (9 za 
serikali na 6 zisizo za Serikali). 


WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...