Wednesday, 7 September 2016

UZINDUZI WA KONDOM MPYA YA ZANA WAFANYIKA MKOANI MWANZA



Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dr.Leonard Subi (kushoto) akizindua Kondom mpya ya Zana inayotolewa na Serikali bure kwa wananchi kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Mpango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi.


Kondom ya Zana ni mbadala wa kondom iliyokuwa ikitolewa pia bure na serikali na kusambazwa na Bohari ya Dawa nchini MSD ambapo kondom hiyo haikuwa na jina, rangi na kifungashio chenye kuvutia hali ambayo ilisababisha wananchi kudhania kwamba haina ubora jambo ambalo hata hivyo halikuwa sahihi kwani ilikuwa na ubora kama aina nyingine za kondom.




Uzinduzi wa Zana Kondom mkoani Mwanza






Kaimu Mkuu wa kitengo cha habari, elimu na mawasiliano kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Mpango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi, Eddah Katikiro, amesema kumekuwa na dhana potofu kwa wananchi kuhusu kondom zinazotolewa bure na serikali kwamba hazina ubora jambo ambalo siyo sahihi ambapo amewahahikikishia kwamba kondom ya Zana ina ubora wa hali ya juu hivyo ni vyema wakazingatia matumizi sahihi na endelevu ya kondom hiyo ili kuondokana na magonjwa ya zinaa na mimba zisizotarajiwa. 


Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dr.Leonard Subi, amebainisha kwamba serikali imekuwa ikitumia kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kuwahudumia wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi hivyo ni vyema wakazingatia matumizi ya kondom ili kujikinga na maambukizi hayo.


Dr.Pius Masele ambaye ni Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Mwanza, akizungumza na wanahabari ambapo amesema hali ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi ni asilimia 4.2 na kwamba serikali inaendelea kuhakikisha kwamba inatomeza mambukizi hayo pamoja na magonjwa mengine ya ngono kwa kuhamasisha wananchi kuzingatia matumizi sahihi na endelevu ya kondom


Kutoka kushoto ni Dr.Pius Masele, Mratibu wa Ukimwi mkoani Mwanza, Kaimu Mkuu wa kitengo cha habari, elimu na mawasiliano Mpango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi, Eddah Katikiro, Mganga Mkuu mkoani Mwanza, Dr.Leonard Subi, Mratibu wa TACAIDS mkoani Mwanza, na Mratibu PSI mkoani Mwanza, Clement Mbogo.


Kaimu Mkuu wa kitengo cha habari, elimu na mawasiliano kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Mpango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi, Eddah Katikiro, akizungumza kwenye uzinduzi huo.


Dr.Pius Masele, Mratibu wa Ukimwi mkoani Mwanza, akizungumza kwenye uzinduzi huo


Mratibu PSI mkoani Mwanza, Clement Mbogo, akizungumza kwenye uzinduzi huo wa Zana Kondom mkoani Mwanza


Mganga Mkuu mkoani Mwanza, Dr.Leonard Subi, akizungumza kwenye uzinduzi wa Zana kondom mkoani Mwanza


Taswira Ukumbini


Wadau mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi wa kondom ya Zana mkoani Mwanza



Wadau mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi wa kondom ya Zana mkoani Mwanza



Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dr.Leonard Subi, amebainisha kwamba serikali imekuwa ikitumia kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kuwahudumia wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi hivyo ni vyema wakazingatia matumizi ya kondom ili kujikinga na maambukizi hayo.


Amesema ili kuondokana na matumizi hayo ya fedha, Serikali inawahimiza wananchi kuzingatia matumizi sahihi na endelevu ya kondom, ili kuondokana na maambukizi ya virusi hivyo pamoja na maambukizi mengine ya magonjwa zinaa ikiwemo kaswende.


Dr.Subi ameyasema hayo hii leo kwenye uzinduzi wa kondom mpya ya Zana uliofanyika mkoani Mwanza, ambayo itakuwa ikisambazwa bure kwa wananchi na serikali ili kusaidia wananchi kuondokana na magonjwa ya zinaa pamoja na kimba zisizotarajiwa.

Amesema ni vyema wananchi wakaendelea kuhimizwa kuwa na matumizi sahihi na endelevu ya kondom ya Zana, hatua itakayosaidia kupunga ongezeko la waathirika wa magonjwa ya zinaa ikiwemo virusi vya Ukimwi na hivyo kuipunguzia serikali matumizi makubwa ya fedha kwa ajili ya kuwahudumia wenye maambukizi hayo.

Naye Kaimu Mkuu wa kitengo cha habari, elimu na mawasiliano kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Mpango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi, Eddah Katikiro, amesema kumekuwa na dhana potofu kwa wananchi kuhusu kondom zinazotolewa bure na serikali kwamba hazina ubora jambo ambalo siyo sahihi ambapo amewahahikikishia kwamba kondom ya Zana ina ubora wa hali ya juu hivyo ni vyema wakazingatia matumizi sahihi na endelevu ya kondom hiyo ili kuondokana na magonjwa ya zinaa na mimba zisizotarajiwa.

Uzinduzi wa kondom mpya ya Zana inayotolewa bure na serikali kwa wananchi, ulifanyika Kitaifa Agosti 30,2016 mkoani Mbeya ambapo kwa mkoa wa Mwanza umefanyika hii leo Jijini Mwanza ambapo wahamasishaji rika watakuwa wakipita mitaani kuwahamasisha wananchi juu ya matumizi sahihi ya kondom hiyo na baadae uzinduzi kama huo utaendelea katika mikoa mingine nchini lengo likiwa ni kuwahamasisha wananchi kutumia kondom hiyo ili kusaidia mapambano dhidi ya magonjwa ya zinaa ikiwemo virusi vya Ukimwi na mimba zisizotarajiwa.


MUWSA YAKABIDHI MADAWATI KWA SHULE YA MSINGI MANDELA MJINI MOSHI


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.Said Mecky Saidiq akiwasili katika shule ya msingi Mandela iliyopo kata ya Bomabuzi wilaya ya Moshi kwa ajili ya kupokea msaada wa Madawati yaliyotolewa na Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA). 

Wanafunzi katika shule ya Msingi Mandela wakiimba nyimbo wakati wakipokea wageni waliofika katika tukio la kukabidhi madawati. 

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi(MUWSA) Joyce Msiru akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadiq alipowasili katika shule ya msingi Mandela kwa ajili ya kukabidhiwa Madawati. 

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Saidiq akiwa na Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba (kushoto) pamoja na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi,Raymond Mboya (kulia) wakati wa makabidhiano ya Madawati kwa ajili ya shule ya msingi Mandela. 

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) ,Joyce Msiru akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi madawati kwa ajili ya shule ya msing Mandela. 

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi(MUWSA) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadiq Madawati kwa ajili ya shule ya Msingi Mandela iliyopo Manispaa ya Moshi. 

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadiq (katikati) akiwa ameketi kwenye Dawati na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru pamoja na mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Mandela. 

Wanafunzi katika shule ya Msingi Mandea wakiwa wameketi katika madawti yaliyotolewa na Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira mjini Moshi(MUWSA). 

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Saidiq akikabidhi madawati kwa mkuu wa shule ya msingi Mandela ,Pegi Michael.

MNASI ATOA ONYO KALI KWA WASIMAMIZI WA MITIHANI YA DARASA LA SABA




Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi akiandika baadhi ya hoja kutoka kwa baadhi ya wasimamizi wa mitihani ya darasa la saba inayotarajiwa kufanyika siku ya jumatano tarehe 07 /09 /2016 na alhamisi tarehe 08 /09 /2016.


baadhi ya wasimamizi wa mitihani ya darasa la saba wakimsikiliza Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi.





Na fredy mgunda,ileje


Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi, amewaasa wasimamizi wa mitihani ya kumaliza elimu ya msingi kutofanya kazi kwa mazoea ili kutoruhusu mianya itakayowafanya wanafunzi wasiokuwa na uelewa kufaulu mitihani hiyo.


Alisema kumekuwa na baadhi ya wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika wanafaulu mithani hiyo kitendo kinachotia mashaka kwa wasimamizi hao kushindwa kunyakazi waliyopewa kwa makini.






Mnasi aliyasema hayo jana, wakati akitoa semina ya mafunzo kwa wasimamizi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje ambapo alisema usimamizi hafifu wa mitihani umesababisha kuwepo kwa watumishi wasiokuwa na uwezo kitaaluma.






Aidha kabla ya uteuzi wa Rais wa jamhuri ya muungazo wa tanzania Dr John Pombe Magufuli mkurugenzi huyo ambaye kitaaluma ni mwalimu alikuwa afisa elimu shule ya msingi manispaa ya iringa alisema iwapo ikibainika kufaulu kwa wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika mtuhumiwa wa kwanza kwenye uzembe huo atakuwa msimamizi wa mitihani na hatua kali zitachukuliwa zidi yake.


“Nawatahadharisha kwamba mnaweza mkarubuniwa kuwawezesha wanafunzi wasiokuwa na sifa wafaulu mitihani hiyo,kufanya hivyo ni kukiuka kanuni za usimamizi na uendeshaji wa mtihani na kuwaambia hayupo tayari kutumbuliwa na rais kwasababu za wasimamizi”alisisitiza Mnasi.


Hata hivyo Mnasi aliwataka wasimamizi hao kuwa makini katika kufanyakazi hiyo na kama kuna jambo lolote ambalo hawajalielewa kuhusu kazi hiyo ni vyema wakauliza ili kupewa majibu.


“hakikisheni kuwa taratibu zote za mitihani zinazingatiwa ipasavyo na kuwataka wasimamizi wote kufanya kazi yao kwa umakini na uadilifu wa hali ya juu.“Nawaasa wasimamizi wa mitihani kujiepusha na vitendo vya udanganyifu kwani serikali itachukua hatua kali kwa yeyote atakayebainika kukiuka taratibu za mitihani,” alisema Mnasi.






Mnasi alibainisha kuwa, serikali imezingatia uwezo wa kitaaluma, uadilifu na uaminifu hivyo wasimamizi hao kupewa jukumu la kusimamia mitihani hiyo muhimu ya kitaifa.






Aliongeza kuwa mitihani hiyo ni muhimu ili kuliwezesha taifa kupima kiwango cha elimu kilichpo nchini na kuwapata wasomi wa kiwango cha juu.






Nao wasimamizi wa mitihani hiyo wamemuahidi mkurugenzi huyo kuwa watasimamia mitihani hiyo kwa kufuata sheria na kanuni za usimamizi wa mitihani walizopewa.


Lakini mitihani hiyo ya kuhitimu darasa la saba inatarajiwa kufanyika siku ya jumatano tarehe 07 /09 /2016 na alhamisi tarehe 08 /09 /2016.


WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...