Monday, 10 August 2015

WILAYANI MUFINDI KUTEKELEZA MRADI WA VIAZI LISHE






Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi  mkoani Iringa ni miongoni mwa  wilaya saba nchini, zilizochaguliwa na shirika la kimataifa lianaloshughulikia mazao ya viazi (CIP)  kutekeleza mradi  wa uzalishaji wa viazi lishe vyenye asilimia kubwa ya vitamini “A” ukilinganisha na  aina nyingine ya vyakula kama Mboga, Matunda na Mizizi.

Kauli hiyo imetolewa Jana na Ofisa habari na Mawasiliano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi. Ndimmyake Mwakapiso, wakati akizungumza na Nipashe  ofisini kwake.

YALIYOJIRI LEO DAR WAKATI LOWASSA ANACHUKUA FOMU NEC

MWENYEKITI WA CCM ARUSHA ATIMKIA CHADEMA



Aliyekuwa Kigogo wa Chama cha Mapinduzi ambaye ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha, Mh Onesmo Nangole na Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Arusha, Isack Joseph wamejiuzulu nafasi zao zote na kujiunga na chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA).


Wakizungumza mara baada ya kutua Upinzani vigogo hao wamemtaka Katibu Mkuu wa CCM, Kinana kuacha mara moja siasa za matusi za kuwaita Makapi wanachama ambao wamekuwa wakijiunga na vyama vya upinzani.

MAADHIMISHO YA 23 YA WIKI YA UNYONYESHAJI MAZIWA YA MAMA KITAIFA YAFIKIA KILELE MJINI DODOMA MWISHONI MWA WIKI


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akitoa hotuba ya kuhitimisha Maadhimisho ya 23 ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kitaifa kwenye viwanja vya Nane Nane Nzuguni Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki.Picha na John Banda wa Pamoja Blog.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akimkabidhi zawadi Mwanafunzi Margreth Mussa wa shule ya msingi Maria de Matias baada ya kushinda shindano la kuandika insha ya lishe na unyonyeshaji wakati wa sherehe za kilele cha Maadhimisho ya 23 ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kitaifa zilizofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Nane Nane Nzuguni Mkoani Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akimkabidhi zawadi Bi. Lilian Simon mmoja ya wakina mama walionyonyesha watoto wao kwa kufuata maelekezo ya wataalamu na kuwezesha watoto wao kuwa na afya bora na kukua vizuri. 

Kikundi cha ngoma za asili ya kigogo cha zepisa Hombolo kikitumbuiza wakati wa sherehe za kilele cha Maadhimisho ya 23 ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kitaifa zilizofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Nane Nanne Nzuguni Mkoani Dodoma.

Vijana wa bendi ya muziki ya Winners ya Mjini Dodoma wakionesha ufundi wa kusakata muziki wakati wa sherehe za kilele cha Maadhimisho ya 23 ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kitaifa zilizofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Nane Nanne Nzuguni Mkoani Dodoma.

TAZAMA VIDEO MPYA YA FRED SWAGG FT BARAKA DA PRINCE - "KIKOMO"


IMG-20150721-WA0084




WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...