Waziri na Mbunge wa Rungwe Mashariki, Profsea Mark James Mwandosya akisalimiana na wanachama na wadhamini baada ya kutoka katika Ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Wilaya ya Iringa Vijijini leo.
Waziri na Mbunge wa Rungwe Mashariki, Profsea Mark James Mwandosya akiondoka kutoka katika Ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Wilaya ya Iringa Vijijini leo baada ya kupata wadhamini na kuelekea Uwanja wa ndege Nduli kwa ajili ya safari ya kwnda mkoani Tabora.
Katibu Msaidizi wa CCM Wilaya ya Iringa Vijijini, Hakimu Jackson (kushoto) akimkabidhi fomu ya majina ya wadhamini Waziri na Mbunge wa Rungwe Mashariki, Profsea Mark James Mwandosya katika Ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Wilaya ya Iringa Vijijini leo. (Picha Na Friday Simbaya)
Waziri na Mbunge wa Rungwe Mashariki, Profsea Mark James
Mwandosya aendelea kusaka wadhamini mkoani Iringa ili apewe ridhaa ya
kupeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka
huu.
Profesa Mwandosya alisema kuwa endapo atapata bahati ya kupeperusha
bendera ya chama chake katika mbio za kuwania urais mwaka huu na kufanyikiwa
kushinda urais, atahakikisha elimu afya, ajira kwa vjiana inaboreshwa pamoja na
kuboresha huduma za afya kwa wazee.
Profesa Mwanadosya ambaye aliongozana na mke wake Mama Lucy
Mwandosya wafika tangu juzi mjini Iringa kusaka wadhamini pamoja na kuongea
nao.
Wadhimini waliotoka sehemu mbalimbali walifika katika ofisi
kuu ya CCM Wilaya ya Iringa Vijijijni ambapo hata hivyo alipata wadhamini zaidi
ya 36 katika mbio za kusaka urais.
Profesa Mawandosya pamoja timu yake wameondoka nkoani Iringa
kuelekea mkoani Tabora kuenelea na kazi ya kutafuta wadhamini baada ya
kuzunguka zaidi ya mikoa mitano mpaka sasa.
Idadi ya wagombea urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
inazidi kuongezeka na kwa sasa kufikia wagombea 36.