Thursday, 9 February 2017

BARAZA LA VIONGOZI WA DINI LAUNGA MKONO JITIHADA ZA MAKONDA ...




Mwenyekiti wa Baraza la Viongozi wa Dini la Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania, Sheikh Alhad Mussa Salum.



Mwenyekiti wa Baraza la Viongozi wa Dini la Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania, Sheikh Alhad Mussa Salum (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu baraza hilo kuunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda za kupambana na wanaojihusisha na dawa za kulevya. Kulia ni Katibu wa Baraza hilo, Padre John Solomon.



Baadhi ya viongozi wa dini (waliokaa), wakiwa kwenye mkutano huo. Wengine ni wanahabari.



Mkutano na wanahabari ukiendelea.










Na Dotto Mwaibale






BARAZA la Viongozi wa dini la kupambana na dawa za kulevya Tanzania ambalo liko chini ya Tume ya kupambana na dawa za kulevya limeunga mkono jitihada zinazofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda za kupambana na watu mbalimbali wanaotumia dawa za kulevya.






Katika hatua nyingine baraza hilo limeiomba serikali kumuongezea ulinzi Makonda kwa kuthubutu kutaja watu wanaojihusisha kwa namna moja au nyingine na dawa hizo.






Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum ,alisema Makonda anapaswa kuongezewa ulinzi kutokana na ujasiri aliouonesha wa kuthubutu kuwataja kwa majina watu hao.






"Sisi kama baraza tunapinga vita na kulaani hatua yoyote ya kushiriki katika biashra au utimiaji wa dawa za kulevya kwa kuwa matumizi ya dawa hizo yamekuwa ni kikwazo kikubwa cha maendeleo katika nchi yetu na yanapotokea nguvu kazi ya Taifa kwa vile wahanga wakubwa wa matumizi ya dawa hizi ni vijana"alisema.






Alisema kutokana na ugumu wa kazi hiyo aliyoianzisha baraza hilo linamuombea kwa mwenyezi mungu ili ampe ulinzi wake na kinga yake na azidi kumpa moyo wa ujasiri wa kupambana na maovu yote yanayo haribu sifa ya Taifa letu na vijana kwa ujumla.






Salum alisema hivi sasa Makonda ameshanza kutengenezewa majungu, fitina na uzushi mbalimbali ili kumkatisha tamaa na aonekane mbaya kwa watanzania lakini hawatafanikiwa endapo atamtanguliza mwenyezi mungu katika mapambano hayo.






Alisema inawezekana wanaopinga au kubeza juhudi hizo ni kwa sababu tu madhara ya dawa za kulevya hayajawagusa wao na familia zao hivyo hawana uchungu na watanzania wenzao walioathirika hivyo wapuuzwe badala yake wasimame pamoja kama watanzania dhidi ya vita hiyo.









Mwenyekiti huyo wa baraza hilo alitumia fursa hiyo kuwaomba viongozi wengine waige mfano wa Makonda wa kupambana na uovu huo mkubwa ambao ni janga kwa Taifa kwani Tanzania bila dawa za kulevya inawezekana.












LADY IN RED 2017 KUTIKISA JIJI LA DAR




Ni siku chache tu! zimesalia kuikamata Tarehe 11 mwizi huu 2017, kumbuka siku hiyo ni siku pendwa ya Wanamitindo wa hapa Tz, coz wanategemea kukutatishwa kwenye Big Fashion Show ambayo hufanyika kila mwaka yaani hapa naizungumzia “Lady In Red”. 






Muandaaji wa show hiyo Mama wa mitindo maarufu kama Asya Idarous Khamsin, akizungmza na wabahabari Jana Tarehe 8/2/2017 huku akiwa ameambatana na wanamitindo wengine amesema kuwa, 


“Kwanza Show hii ni yakipekee pia inafaida kubwa sana kwa upcoming Designers, Lady in red huwa inatoa kipaumbele kwa upcoming Designers kuweza kuonesha kazi zao jukwaani, hivyo mwaka huu 11/2/2017 mambo yatakuwa mazuri sana ndani ya King Solomoni Hall”. 






Hivyo kwa wadau wote wapenzi wa mitindo mnaombwa kuhudhuria usiku huo ili sanaa ya mitindo iweze kukua zaidi Asante.


Wanamitindo wakiwa kwenye Press ya Lady In Red 2017 



















Asya Idarous 





Picha ya pamoja ya wanamitindo baada ya Press ya Lady In Red 2017 


































RC MTAKA AKABIDHI NG'OMBE KWA AJILI YA AROBAINI YA KIFO CHA MZEE KAYOMBO







Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kijiji cha Misasi


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (kushoto)


Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo



Ng'ombe aiyetolewa na Rc Mtaka kwa ajili ya Arobaini ya Mzee Kayombo


Mwenyekiti wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA) Chief Mrindoko Babu Mwidadi akisaini kitabu cha wageni ishara ya ushiriki wa asasi hiyo katika msiba wa Mzee Kayombo



Mazungumzo yamenoga mara baada ya makabidhiano ya Ng'ombe


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka (katikati) na Mkewe wakifanya maombi katika kaburi la marehemu Mzee Kayombo, Kulia kwao ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Kayombo ambaye ni mjukuu wa Marehemu Mzee Kayombo



Rc Antony Mtaka Mtaka



Rc Mtaka akiwasalimu ndugu wa marehemu Mzee Kayombo mara baada ya kukabidhi Ng'ombe 



Rc Mtaka (kulia) akisisitiza jambo, kulia MD Kayombo na katikati ni Mathias Canal Mhariri wa Tovuti ya (www.wazo-huru.blogspot.com) wakisikiliza kwa makini busara za mkuu huyo wa Mkoa wa Simiyu



MD Kayombo akiwa na ndugu na jamaa katika mazungumzo ya jioni 


Na Mathias Canal, Mwanza 

Ikiwa ni siku tatu zimepita tangu Marehemu Mzee Antony Raphael Kayombo kuhifadhiwa katika nyumba yake ya milele (kaburini) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka amezuru kijijini Misasi, Wilayani Misungwi kwa ajili ya kutoa pole kwa familia ya Mzee huyo.

Rc Mtaka aliyeambatana na Mkewe wamefanya sala ya kumuombea mapumziko mema Mzee Kayombo ikiwa ni ishara ya ukamilifu wake wa haki na kheri hapa Duniani.


Pamoja na mkono wa pole kama mila za kiafrika zinavyoarifu Rc Mtaka pia ameikabidhi familia hiyo Ng'ombe kwa ajili ya Arobaini itakayofanyika kijijini hapo ikiwa ni ishara ya ukamilisho wa Msiba huo (HITMA)).


"Binafsi naamini katika matendo mema hapa Duniani, Mzee wetu ametutoka ni pigo kwa familia na kwetu sote lakini hakuna namna tuna kila sababu ya kulipokea jambo hili kama jambo la kila mmoja wetu japo halizoeleki" Aliongeza RC Mtaka

Akipokea Ng'ombe huyo na kuzungumza kwa niaba ya familia Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo ambaye ni mjukuu wa marehemu Mzee Kayombo amesema kuwa kwa kuwa safari ya kifo ni ya kila mmoja hivyo familia imepokea kifo hicho kama safari ya mwisho kwa Mzee wao lakini inaendelea kumuombea ili aishi maisha ya amani huko alipo.

MD Kayombo amemshukuru Mkuu huyo wa Mkoa wa Simiyu kwa kufika na kuwasalimu waombolezaji ambao bado wapo kijijini hapo sawia na kumtakia majukumu mema katika utendaji wake ili kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo kote nchini.


Marehemu Mzee Kayombo aliugua ugonjwa wa kibofu cha mkojo ambao ulianza ghafla tarehe 29/1/2017 na kupelekwa katika hospitali ya Misasi, Baadae hospitali ya Sekou Ture na mwishowe Hospitali ya Bugando ambapo alifanyiwa upasuaji ambapo hata hivyo hali yake iliendelea kudhoofika mpaka mauti ilipomkuta tarehe 4/2/2017 majira ya saa mbili usiku.


MUNGU AILAZE MAHALA PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU MZEE ANTONY RAFAEL KAYOMBO. AMENI 


RAS MKOA WA IRINGA AZITAKA KAMATI ZA SHULE KUSIMAMIA MAENDELEO YA SHULE



Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu akizungumza na wajumbe wa kamati za shule kutoka shule za serikali wakati akifunga mafunzo ya kuzijengea uwezo kamati za shule yafanyika kimkoa katika Kata ya Makungu, Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa jana. (Picha na Friday Simbaya)

Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu akifuatilia risala kutoka kaimu afisa elimu taaluma (msingi) wa wilaya ya mufindi, Onesmo Kikoti (hayupo pichani) kabla ya kufunga mafunzo ya kuzijengea uwezo kamati za shule yafanyika kimkoa katika Kata ya Makungu, Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa jana. (Picha na Friday Simbaya)


Kaimu Ofisa Elimu Mkoa wa Iringa, Nasibu Mengele (kulia) akitoa utambulisho kwa wajumbe wa kamati za shule kutoka shule za serikali wakati wa ufungaji wa mafunzo ya kuzijengea uwezo kamati hizo yaliyofanyika kimkoa katika Kata ya Makungu, Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa jana. Kulia kwake ni Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu, Afisa Elimu ya Wazima- Mufindi, Faustine Mhapa, Afisa Mtendaji wa kata ya Makungu, Markus Makweta na Afisa Habari wa Mkoa Dennis Gondwe. (Picha na Friday Simbaya)






Kaimu Afisa Elimu Taaluma (msingi) Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa, akitoa utangulizi kwa Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Wamoja kabla ya kufunga mafunzo ya kuzijengea uwezo kamati za shule yafanyika kimkoa katika Kata ya Makungu, Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa jana. (Picha na Friday Simbaya)



Baadhi ya wajumbe wa kamati za shule kutoka shule za serikali wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi ambaye ni Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu (hayupo picha) wakati akifunga mafunzo ya kuzijengea uwezo kamati za shule yafanyika kimkoa katika Kata ya Makungu, Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa jana. (Picha na Friday Simbaya)

Na Friday Simbaya, Mufindi

Maendeleo ya Taifa lolote yanategemea kwa kiasi kikubwa ubora wa elimu ya watu wake. 

Mahitaji ya utoaji elimu bora na usimamizi unahitaji uwajibikaji wa karibu kutoka ngazi ya taifa, mkoa, halmashauri na serikali ya kijiji/mtaa.

Hayo yalisema jana na Katibu Tawala Mkoa wa Iringa (RAS), Wamoja Ayubu wakati akifunga mafunzo ya wajumbe wa kamati za shule kimkoa katika Kata ya Makungu wilayani Mufindi, mkoani Iringa.

Mafunzo kwa wajumbe wa kamati za shule za msingi za serikali hayo yalianza tarehe 13/01/2017 katika Mkoa wa Iringa na kumalizika jana tarehe 07/02/2017.

RAS aliwataka wajumbe wa kamati hizo kusimamia kikamilifu shughuli zote za maendeleo ya shule za msingi.

Alisema kuwa kamati za shule ni chombo cha usimamizi, uendeshaji na uongozi wa shule ambacho kinasimamia shughuli zote za shule kwa niaba ya wenye shule.

Alisema kuwa mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka kwa sababu kumekuwa na changamoto nyingi katika sekta ya elimu, hasa katika uendeshaji wa shughuli za maendeleo shuleni.

RAS huyo pia alitumia fursa kuwapongeza kwa matokeo mazuri ya kidato cha nne mwaka 2016, kwa mkoa kushika nafasi ya pili (2) kitaifa.

“Haya ni mafanikio makubwa kwa sababu mwaka 2015 Mkoa wa Iringa ulishika nafasi ya tano (5) kitaifa,” alisema Ayubu.

Aliongeza kuwa lengo la kuundwa kwa kamati za shule ni kukuza dhana ya uongozi na ushirikishaji ili kuleta ufanisi katika uendeshaji wa shule kwa ujumla.

Naye, Kaimu Ofisa Elimu Mkoa wa Iringa, Nasibu Mengele alisema kuwa elimu msingi ni kiungo muhimu cha kuandaa wataalam mbalimbali ambacho mchango wa ni mkubwa katika kuendeleza uchumi, sayansi na teknolojia katika jamii na maisha bora kwa watanzania.

Alisema kuwa ili kufikia malengo tarajiwa ni vizuri wajumbe wa kamati za shule wakatambua masuala mbalimbali na kupata stadi mahiri za uongozi na usimamizi wa shule, ili ziweze kutoa elimu bora kwa watoto wote nchini.

“Kamati ya shule imepewa uwezo kisheria chini ya ibara ya 3 ya kifungu cha 39 cha Sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978, na marekebisho yake ya mwaka 1995,” alisema Mengele.

Alisema kuwa kifungu hicho kinataka kuundwa kwa kamati ya shule kwa kila shule ya awali na msingi ambayo itakuwa na jukumu la kusimamia uendeshaji wa shule husika.

Mafunzo hayo kwa wajumbe wa kamati za shule za serikali walikuwa na mada kuu nne zilizotelewa kwao.

1. Uongozi,mundo wa majukumu ya kamati za shule.

2. Usimamizi wa sera na sheria za uendeshaji wa elimu.

3. Usimamizi wa rasilimali za shule.

4. Uandaji wa mpango wa jumla wa maendeleo ya shule.

Mafunzo hayo ambayo yalifanyika katika kila halmashauri yalihudhuriwa na jumla ya washiriki 5,750 (wanaume 3,470 na wanawake 2,280) kutoka shule zote za serikali zilizopo katika Mkoa wa Iringa.

Aidha, kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, jumla ya washirika 1,792 walipaswa kushiriki (wanawake 701 na wanaume 1,091), lakini waliyofanyikiwa kushiriki mafunzo hayonni washiriki 1,642.



Mwisho

DC WASHUKIA VIJANA WANAOCHEZA KAMARI ‘KUBETI’

DC KASESELA

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amewata vijana nchini kuachana na tabia ya kucheza kamari yaani ‘kubeti’ kwa kutabiri mambo kadhaa.

Hapa Tanzania mchezo maarufu ni soka, hivyo mashabiki wa mchezo huo utabiri mambo kadhaa katika mchezo husika, ikiwemo wafungaji wa magoli, idadi ya magoli kwenye mechi husika, magoli yakufungwa kipindi kipi cha mchezo na ukuisha matokeo yatakuwaje.

Kasesela alisema kuwa vijana watakiwa kujishughulisha na shughuli za kiuchumi na kuachana mazoea kutengenza pesa kwa njia mikato kama kucheza kamari.

Akizungumza wakati wa kufunga mashindano ya Kombe la J.Msofu na kukabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza na wa pili, Kasesela alizipongeza timu hizo kwa kucheza mchezo mzuri huku akiwataka wachezaji kucheza mpira kwa kuwa mpira ni ajira.

Timu ya Itengulinyi FC iliyopo kwenye kata ya Maboga ilitwaa ubingwa baada yakuichakaza timu ya Kiponzelo FC kwa mabao 4-3 kwa mikwaju ya penalti kwenye mashindano ya kombe la Msofu Cup yaliyomalizika hivi karibuni.

Mechi hiyo ya fainali kati ya timu hizo mbili uliyochezwa katika uwanja wa shule ya sekondari kiponzelo, kata ya maboga na tarafa ya kipozelo, wilayani Iringa.

Mechi hiyo ya fainali kati ya timu hizo mbili uliyochezwa katika uwanja wa shule ya sekondari kiponzelo, kata ya maboga na tarafa ya kipozelo, wilayani Iringa.

Kwa upande wake, mdhamini wa mashindano hayo Jeremia Msofu alisema kuwa lengo la mashidano hayo nikuibua vipaji vitakavyoweza kuunda timu ya Jimbo la Kalenga, itakayoweza kucheza kuanzia Ligi ya daraja la nne la hadi Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara.

Mashindano hayo yalianza rasmi decemba 11 mwaka jana na kumalizika Februari 5 mwaka 2017.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza na wa pili mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alizipongeza timu hizo kwa kucheza mchezo mzuri huku akiwataka wachezaji kucheza mpira kwa kuwa mpira ni ajira.

Mshindi wa kwanza alizawadiwa ng’ombe mmoja mwenye thamani ya 500,000 na mshindi wa pili mbuzi wawili wenye thamani ya 150,000/-.

Hata Golikipa bora katika mashindano hayo Adam Jaffari alizawadiwa fedha taslim 50,000/-, mfungaji bora akizawadiwa 50,000/- huku timu yenye nidhamu katika mashindano hayo yaani Usengelindete ikiondoka na zawadi ya 50,000/-.

Mashindano hayo yalizinduliwa rasmi na Katibu wa Chama cha Mpira Iringa Vijijini ,Juma Lalika, ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya uchaguzi wa Chama cha Mpira Tanzania (TFF).

MWISHO



WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...