Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amewata vijana nchini kuachana na tabia ya kucheza kamari yaani ‘kubeti’ kwa kutabiri mambo kadhaa.
Hapa Tanzania mchezo maarufu ni soka, hivyo mashabiki wa mchezo huo utabiri mambo kadhaa katika mchezo husika, ikiwemo wafungaji wa magoli, idadi ya magoli kwenye mechi husika, magoli yakufungwa kipindi kipi cha mchezo na ukuisha matokeo yatakuwaje.
Kasesela alisema kuwa vijana watakiwa kujishughulisha na shughuli za kiuchumi na kuachana mazoea kutengenza pesa kwa njia mikato kama kucheza kamari.
Akizungumza wakati wa kufunga mashindano ya Kombe la J.Msofu na kukabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza na wa pili, Kasesela alizipongeza timu hizo kwa kucheza mchezo mzuri huku akiwataka wachezaji kucheza mpira kwa kuwa mpira ni ajira.
Timu ya Itengulinyi FC iliyopo kwenye kata ya Maboga ilitwaa ubingwa baada yakuichakaza timu ya Kiponzelo FC kwa mabao 4-3 kwa mikwaju ya penalti kwenye mashindano ya kombe la Msofu Cup yaliyomalizika hivi karibuni.
Mechi hiyo ya fainali kati ya timu hizo mbili uliyochezwa katika uwanja wa shule ya sekondari kiponzelo, kata ya maboga na tarafa ya kipozelo, wilayani Iringa.
Mechi hiyo ya fainali kati ya timu hizo mbili uliyochezwa katika uwanja wa shule ya sekondari kiponzelo, kata ya maboga na tarafa ya kipozelo, wilayani Iringa.
Kwa upande wake, mdhamini wa mashindano hayo Jeremia Msofu alisema kuwa lengo la mashidano hayo nikuibua vipaji vitakavyoweza kuunda timu ya Jimbo la Kalenga, itakayoweza kucheza kuanzia Ligi ya daraja la nne la hadi Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Mashindano hayo yalianza rasmi decemba 11 mwaka jana na kumalizika Februari 5 mwaka 2017.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza na wa pili mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alizipongeza timu hizo kwa kucheza mchezo mzuri huku akiwataka wachezaji kucheza mpira kwa kuwa mpira ni ajira.
Mshindi wa kwanza alizawadiwa ng’ombe mmoja mwenye thamani ya 500,000 na mshindi wa pili mbuzi wawili wenye thamani ya 150,000/-.
Hata Golikipa bora katika mashindano hayo Adam Jaffari alizawadiwa fedha taslim 50,000/-, mfungaji bora akizawadiwa 50,000/- huku timu yenye nidhamu katika mashindano hayo yaani Usengelindete ikiondoka na zawadi ya 50,000/-.
Mashindano hayo yalizinduliwa rasmi na Katibu wa Chama cha Mpira Iringa Vijijini ,Juma Lalika, ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya uchaguzi wa Chama cha Mpira Tanzania (TFF).
MWISHO
No comments:
Post a Comment