Friday, 9 June 2017

INTANETI INAVYOCHOCHEA UKUAJI WA UTALII BARANI AFRIKA


Na Jumia Travel Tanzania

Afrika ni bara la pili kwa kuwa na idadi kubwa ya watu ambapo inafikia takribani bilioni 1.2 (wengi wao wakiishi mijini) na inatarajiwa kongezeka mpaka bilioni 2.5 kufikia mwaka 2050 (25% ya watu wote duniani).




Kwa mujibu wa ripoti ya utalii kwa Afrika mwaka 2017 iliyofanywa na Jumia Travel imebainisha kwamba mtu mmoja kati ya watatu ni sehemu ya watu wa daraja la kati (watu wanaofanyakazi kwenye taaluma na biashara mbalimbali pamoja na familia zao) na wanatarajiwa kuongezeka mara mbili zaidi kufikia 2050. Watu wa daraja la kati ni muhimu katika uchangiaji wa ukuaji wa utalii wa ndani na ukanda mzima tuliopo.


Miongoni mwa mambo yanayochochea maendeleo na ukuaji wa sekta mbalimbali Afrika ikiwemo utalii ni pamoja na mtandao wa intaneti.


Mpaka hivi sasa, watumiaji wa mtandao wa intaneti barani Afrika wamefikia zaidi ya milioni 300, ambayo ni sawa na 9.3% ya waafrika wote na 27.7% ya ueneaji wake. Kwa kiasi kikubwa idadi hiyo imechangiwa na kuingia na kuongezeka kwa matumizi ya simu za mkononi.




Ripoti hiyo imeendelea kufafanua kuwa mnamo mwishoni mwa mwaka 2015, 46% ya waafrika walijiunga na huduma za simu za mkononi. Na idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka kufikia milioni 725 kufikia mwaka 2020. Na hiyo imetokana na upatikanaji wa mtandao wa intaneti wa 4G kwa zaidi ya nusu ya nchi za kiafrika, ambapo mpaka kufikia katikati ya mwaka 2016 takribani nchi 32 zilikuwa zimekwishaunganishwa na mitandao 72 ya LTE (Long-Term Evolution). 


Kutokana na maendeleo hayo ya matumizi ya intaneti, sekta ya utalii hususani huduma za hoteli na malazi kwa ujumla inanufaika kwa kiasi kikubwa. Na hii ni kutokana na wateja kuwezeshwa kufanya kila kitu wakiwa mtandaoni badala ya kutembelea moja kwa moja hotelini.


Jumia Travel kwenye ripoti yake imebainisha kwamba idadi kubwa ya wateja wanatafuta na kufanya huduma za hoteli mtandaoni kwani ni salama, haraka na uhakika zaidi. Ripoti inaonyesha kwamba wateja wengi hutafuta huduma mtandaoni kwa kutumia simu za mkononi (51%) zaidi ukilinganisha na kompyuta (49%). Vivyo hivyo pia kwenye kufanya huduma yenyewe wengi hupendelea zaidi simu za mkononi (68%) dhidi ya kompyuta (32%).


Takwimu hizo ni ishara nzuri kwamba waafrika wamekubali kuyapokea mabadiliko yaliyotokana na mtandao wa intaneti hususani kwa matumizi yenye faida kwao. Kwa hiyo ni fursa kwa wadau wa sekta ya utalii kujikita zaidi mitandaoni ili kuweza kuendana na kasi ya wateja wengi wanaohamia huko.




Ingawa bado tupo nyuma kwa kiasi fulani ukilinganisha na mabara mengine lakini hali imebadilika ukilinganisha na kipindi cha nyuma. Hivi sasa, wasafiri wengi kutokana na kurahisishiwa kila kitu mtandaoni imekuwa ni rahisi kwao kufanya huduma wakiwa mahali popote na muda wowote.


Kwa mfano, wateja wengi wanaitumia njia ya mtandao kufanya huduma zao za malazi tofauti na hapo awali ambapo ilibidi kupiga simu au kwenda moja kwa moja hotelini. Mtandaoni kuna orodha ya hoteli zote, zikiwa sehemu moja, zikionyesha mahali zilipo, bei za vyumba vyake, upatikanaji wake na pia namna ya kufanya malipo. Hivyo kumrahisishia mteja kwa kuokoa muda na gharama ambavyo vingepotea kwa kutembelea hoteli moja kwenda nyingine.


Mtandao wa intaneti si tu umewarahisishia wateja kupata huduma kwa urahisi na uhakika lakini pia hata mameneja wa hoteli na wapokea huduma. Kwa mfano, kwa sasa kuna mifumo ambayo inawawezesha kuratibu mwenendo na utaratibu wa shughuli zao mahali popote walipo na muda wowote wautakao.


Mfumo huo huwarahisishia kupokea na kuthibitisha upatikanaji wa huduma, kuwa na uhakika na idadi ya vyumba walivyonavyo, kujua idadi na aina ya wateja wanaopendelea huduma zao pamoja na kupokea maoni mbalimbali juu ya huduma wanazozitoa. 



Ripoti hiyo pia imebainisha kwamba orodha ya nchi nane ambazo ueneaji wake wa mtandao wa intaneti ni mkubwa barani Afrika ni kama vile; Kenya (74%), Mauritius (63%), Shelisheli (57.6%), Morocco (57.3%), Nigeria (52%), Afrika ya Kusini (51.6%), Tunisia (50.5%) na Cape Verde (44.1%). 






WAKINA BABA WATAKIWA KUTOA ELIMU YA AFYA YA UZAZI KWA WATOTO WAO




Ofisa Programu wa TGNP Mtandao, Anna Sangai (kushoto), akitoa mada katika kongamano la siku moja lililohusu elimu ya afya ya uzazi lililofanyika Makao Makuu ya TGNP Mabibo Dar es Salaam jana. Kongamano hilo liliandaliwa na TGNP.



Mwanafunzi Leila Kisinga kutoka Sekondari ya Mabibo akitoa mada kuhusu via vya uzazi vya mwanamke vinavyofanya kazi.



Kongamano likiendelea.



Mshiriki Idd Hamisi akichangia jambo katika kongamano hilo.



Usikivu katika kongamano hilo.



Aisha Kijavara akichangia.



Wakina mama wakiwa katika kongamano hilo. Wakina mama hao walitoa uzoefu wao kuhusu afya ya uzazi kwa watoto.



Mwanafunzi Juma Nasoro kutoka Sekondari ya Mabibo akitoa mada kuhusu via vya uzazi vya mwanaume vinavyofanya kazi.



Mdau Selemani Bishagazi akichangia kuhusu wanaume kuwasaidia watoto wao wa kike wanapokuwa katika hedhi.



Mary Mbarawa akichangia jambo.




Na Dotto Mwaibale


WAKINA Baba nchini wametakiwa kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa watoto wao badala ya kuwaachia kazi hiyo ifanywe na wakina mama pekee.


Mwito huo umetolewa na Selemani Bishagazi wakati akichangia mada katika kongamano la siku moja lililohusu elimu ya afya ya uzazi kwa watoto hasa wa kike lililoandaliwa na TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam jana.


"Suala la utoaji wa elimu ya afya ya uzazi kwa watoto wetu hasa wa kike ni letu sote kati ya baba na mama kwani baba ndie chanzo kikubwa cha mapato katika familia" alisema Bishagazi.


Bishagazi alisema suala la kutoa fedha za kunulia pedi wakati mtoto wa kike anapokuwa kwenye hedhi si la mama bali hata baba anawajibu wa kutoa fedha hizo na akaomba dhana hiyo potofu kuwa mama ndiye anawajibika katika suala hilo iachwe.


Alisema ni vizuri mtoto wa kike anapokuwa katika hedhi kuwajulisha wazazi wake ili aweze kusaidiwa kupata fedha za kununulia pedi badala ya kukaa kimya kwa hofu na kujikuta akishindwa kujistiri na kuchafuka.


Mshiriki mwingine katika kongamano hilo alisema usiri imekuwa ni changamoto kubwa katika kumsaidia mtoto kujua afya za uzazi kwani wazazi wengi wanashindwa kuwaweka wazi watoto wao kuhusu jambo hilo.


Alisema mtoto wa kike anapobalee na kuanza kuingia katika hedhi wazazi wanapaswa kumueleza kuwa amekuwa na hivyo iwapo atakutana na mwanaume atapata mimba hivyo kumpa elimu hiyo kwa wazi ataweza kujiepusha na kupata mimba badala ya kufanya siri.


Aisha Kijavara ambaye alishiriki katika kongamano hilo alisema ni vizuri elimu ya afya ya uzazi ikatolewa kwa uwazi na kutaja viungo vya uzazi bila ya kuona aibu ili watoto waweze kuelewa vizuri badala ya kufichaficha.


"Katika suala ili la utoaji wa elimu hii ya afya ya uzazi tunapaswa kuwa na muda wa kutosha na kutamka wazi viungo vya uzazi jinsi vinavyofanya kazi ili walengwa waweze kuelewa vizuri somo" alisema Kijavara.


Ofisa Programu wa TGNP Mtandao, Anna Sangai alisema wanapopigania bajeti zinazopitishwa na bunge ziwe na mlengo wa kutoa kipaumbele kijinsia zinamlenga zaidi mtoto wa kike ambao wanachangamoto nyingi hasa wale waliopo mashuleni kwani wengi wao hawana uwezo wa kununua pedi wanapokuwa katika hedhi.


Alisema baadhi yao wamejikuta wakiingia katika vishawishi vya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume ambao wamekuwa wakiwasaidia kuwanunulia bedi.


"Tumekuwa tukihimiza kutengwa kwa bajeti kubwa za wizara husika ili kuwasaidia watoto hawa ambao wapo katika changamoto hiyo" alisema Sangai.


Kongamano hilo lilihudhuriwa na Wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari ya Mabibo ambao baadhi yao walitoa mada kuhusu afya ya uzazi na matumizi ya via vya uzazi.

RC ANNA MNGWIRA ATEMBELEA FAMILIA YA DKT NDESAMBURO,AZUNGUMZA NA WANACCM



Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mngwira akizungumza na baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi alipotembelea ofisi za chama hicho kujitamburisha .kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro Idd Juma ,na anayefuatia ni Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi,Aisha Amour.


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Manispaa ya Moshi,Elizabeth Minde (katikati) akifurahia jambo wakati Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mngwira (hayupo pichani) alipokutana na uongozi wa chama hicho katika ofisi za CCM-Mkoa wa Kilimanjaro.



Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kilimanjaro ,Idd Juma akitoa neon la shukrani mara baada ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mngwira kutembelea ofisi za chama hicho.


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mngwira akitoka ofisi za Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro mara baada ya kuonana na viongozi wa chama hicho.


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna mngwira akisalimaiana na Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoa wa Kilimanjaro alipofika nyumbani kwa Marehemu Dkt Philemoni Ndesamburo kutoa pole kwa familia.


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mngwira akisalimiana na mtoto wa Marehemu Dkt Philemoni Ndesamburo ,Sindato Ndesamburo alipotembelea nyumbani kwa marehemu kutoa pole kwa familia.


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mngwira akitia saini katika kitabu cha waombolezaji mara baada ya kufika nyumbani kwa Marehemu Dkt Ndesamburo kutoa salamu za pole kwa familia.


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna mngwira akizungumza jambo na mjane wa Marehemu Dkt Ndesamburo ,Ndehorio Ndesamburo alipofika nyumbani kutoa salamu za pole kwa familia.



Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,akitembelea kaburi ulipolazwa mwili wa marehemu Dkt Philemoni Ndesamburo alipofika nyumbani kutoa salamu za pole kwa familia.


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mngwira akiongoza sala katika kaburi la marehemu Dkt Philemon Ndesamburo.


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mngwira akimpa mkono wa pole Mbunge wa viti maalumu na mtoto wa marehemu Dkt Ndesamburo ,Lucy Owenya alipofika kutoa salamu za pole kwa familia y marehemu.



Mbunge wa Viti Maalum Chadema mkoa wa Kilimanjaro,Lucy Owenya akizungumza jambo na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mngwira alipofika kutoa salamu za pole kwa familia.


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mngwira akisalimiana na wananchi katika neo la Kwa Alphonce wakati akiwa njiani akitoka kutoa salamu za pole kwa familia ya Dkt Ndesamburo.



Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mngwira akiwa katika picha ya pamoja na wananchi alipowasalimia katika eneo la Kwa Alphonce mjini Moshi.


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro akizungumza na mmoja wa wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro aliposhuka kwenye gari kuwasalimia.




Na Dixon Busagaga wa Busagaga's Orijino Blog.


WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...