Saturday, 19 December 2015
KIJIJI CHA LYAMKO CHA PATIWA HAKIMILIKI ZA KIMILA 350 KUTOKA TAASISI YA HAKIARDHI
Afisa Ardhi Mteule, Elinaza Kiswaga
Mkurugenzi Mtendaji wa HakiArdhi, Yefred Myenzi...
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilolo, Mejuzi Mgeveke,akigawa hati miliki za kimila.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilolo, Mejuzi Mgeveke, ambaye alikuwa mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja baada yakugawa hati miliki za kimila. (Picha zote Friday Simbaya)
KILOLO: Shirika linalojishughulisha na masuala ya ardhi nchini, HakiArdhi, limetoa hatimiliki za kimila 350 kwa wananchi wa kijiji cha Lyamko baada ya kupimiwa mashamba yao.
Akitoa taarifa fupi ya mradi wa hakiardhi, utawala na mabadiliko ya tabianchi jana Afisa Ardhi Mteule, Elinaza Kiswaga kuwa kijiji cha lyamko kimekuwa ni kijiji cha nane katika wilaya kilolo kupatiwa hati miliki za kimila tangu zoezi la upamaji mwaka 2013.
Alisema kuwa taasis ya HAKIARDHI ilianza kufanya kazi za utafiti wa awali mwaka 2012, na mwanzoni mwa mwaka 2013 taasisi hiyo kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya ya kilolo, ilianza rasmi kutoa mafunzo ya sheria ya ardhi na utawala vijijini.
Alisema kuwa lengo la mradi ulikuwa kutoa uelewa kwa jamii juu ya sheria ya ardhi, utawala vijijini na mabadiliko ya tabianchi hususani kwa wazalishaji wadogo.
Afisa ardhi mteule wa wilaya alifafanua kuwa taasisi hiyo ya HAKIARDHI ilitoa mafunzo ya sheria ya ardhi na utawala vijijini pamoja na na mabadiliko ya tabia nchi katika vijiji 55, kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi kwa vijiji 11 ambavyo ni Kihesamgagao, Kidabaga, Kiwalamo, Kitelewasi, Kipaduka, Uhambingeto na Lugalo, Lyamko, Ibofwe, Itonya na Ilamba.
Naye mgeni rasmi wakati wa hafla ya ugawaji wa hati miliki za kimila Mejuzi Mgeveke, ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa halmashauri ya kilolo aliishukuri taasisi ya HAKIARDHI kwa kuendesha shughuli hizo katika wilaya ambazo zimeleta mafanikio makubwa.
Alisema kuwa ni dhahiri kuwa mafunzo hayo yamesaidia kuleta chachu ya mabadiliko kwa jamii ya wanakilolo katika ngazi zote hasa juu ya uelewa wa masuala ya ardhi, utawala bora na mabadiliko ya tabia nchi.
Nao wanakijiji cha Lyamko wamefurahi kwa kupimiwa mashamba yao ambapo wasaidia kupunguza migogoro ardhi.
Walisema haki ya kumiliki ardhi kwa wanawake imetambuliwa na imeanza kutekelzwa kwa vitendo.
Mkurugenzi Mtendaji wa HakiArdhi, Yefred Myenzi, alisema kuwa katika utekelezaji wa shughuli hizo kumekuwepo na mafanikio makubwa ambyo ameshuhudia vijiji 11 kuanadaliwa mipango ya matumizi bora ya ardhi, kiasi ambacho kimesadia kupunguza migogoro ya ardhi.
Alisema kuwa migogoro hiyo ni pamoja na inayotokana na mwingiliano wa matumizi na uhifadhi wa misitu asilia.
Taasisi ya HAKIARDHI imefanyikwa kufika vijiji 55 kati ya zaidi ya vijiji 106 vya wilaya ya kilolo na bado mwamko ni mkubwa kwa wananchi wa wialya hiyo kutakifiwa zoezi la upimaji mashamba.
Kwa mfano, katika kijiji cha Lyamko ililengwa kupima mashamba 350 lakini wananchi waliojitokeza kwa wingi kiasi cha kufikia wananchi 351 na wengine ilishindikana kupimiwa.
Subscribe to:
Posts (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
The most deadly form of tuberculosis is one that lies in wait inside the body for years, attacking at the first sign of weakness. Abou...