Tuesday, 5 September 2017

RITTA KABATI AIPONGEZA NURU FM RADIO KUANZISHA MASHINDANO YA MAMA MSOSI


Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiongea wakati wa kutambulisha shindano la mama msosi linalolaratibiwa na kituo cha radio Nuru FM 93.5 Iringa katika viwanja vya Kata ya Kihesa.

Msimamizi wa vipindi vya Nuru fm radio na ndio Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya mama msosi mkoani Gerald Malekela akiongea na hadhara iliyokuwa imejitokeza wakati wa utambulisho wa shindano hili.

Baadhi ya washiriki wa shindano la mama msosi wakiwa kwenye picha ya pamoja na mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Ritta Kabati


Na fredy Mgunda, Iringa.


Shindano la mama msosi linaloratibiwa na kituo cha radio cha Nuru fm mkoani Iringa limetambulishwa rasmi kwa wakazi wa manispaa ya Iringa likiwa na lengo la kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira kwa kina mama na jamii kwa ujumla,shindano hilo litawapa washindi kumi na nane kwa kila kata ya manispa ya Iringa ambapo kila mshindi atajinyakulia mtungi mmoja wa shirika la gesi la mihan.


Akizungumza wakati wa utambulisho wa shindano hilo mwenyekiti wa kamati ambaye pia ni msimamizi wa vipindi vya Nuru fm radio Gerald Malekela alisema kuwa wameamua kutoa elimu ya mazingira kwa kuifikia jamii moja kwa moja kwa njia ya kuandaa shindano ambalo limeanza kwa mafanikio makubwa.


“Kutoa elimu kuna njia nyingi sana hivyo nuru fm radio 93.5 Iringa tumeamua kutoa elimu ya utunzaji wa mazingiri kwa wakazi wa mkoa wa iringa kwa kutumia mashindano ya kupika na ndio maana unaona wananchi wamejitokeza kwa wingi sasa nauhakika elimu ya utunzaji wa mazingira imewafika na itaendelea kuwafikia” alisema Malekela.


Malekela aliwataka wakinamama ambao hawajachukua fomu za kushiriki shindano hili walizuate kwenye kata na hapa radio nuru fm ili kupata elimu bure ya mazingira ,ujasiliamali na kujua jinsi ya kutumia nishati mbadala ambayo haina madhara makubwa kwa jamii tofauti na ukataji miti hovyo.


“Mmekuwa mashaidi jinsi gani akinamama walivyokuwa wanapata tabu kuwasha moto hapa kwa kuwa walikuwa wanatumia mkaa,mmewaona walivyochafuka hivyo kama wangekuwa wanatumia gesi hawagepata shida yote hiyo wala wasingechukua muda wote huo kupika” alisema Malekela


Aidha Malekela alitaja maeneo ambayo shindano la mama msosi litafanyikia ambazo ni kata zote kumi na nane za manispaa ya Iringa hivyo wananchi wanaombwa kujitokeza katika maeneo ambayo shindano litakuwa linafanikia.


Akihudhuria utambulisho wa shindano mama msosi linaloendeshwa na kituo cha radio Nuru fm mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati aliipongeza radio hiyo kwa hatua waliyochukua kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira kwa njia ya mashindano ambayo yameanza kwa kuwa na mashabiki wengi.


“Leo ni utambulisho tu lakini watu ni wengi na hamasa imekuwa kubwa hivyo naamini kuwa elimu ya utunzaji wa mazingira kwa wakazi wa manispaa ya Iringa itawafikia vilivyo na kusaidia kupunguza uharibifu wa mazingira ambao umekuwa ukiathili mazingira kwa ujumla” alisema kabati


Kabati aliongeza kuwa ataendelea kuliunga mkono shindano hilo kwa kuwa linatija ya kimaendeleo kwa taifa la Tanzania narudia tena kuwapongeza Nuru fm kwa wazo lenu ambalo litaungwa mkono na watu wengine wadau wa mazingira.


Kwa upande wake meneja wa kituo cha radio Nuru fm Victor Chakudika alimshukuru mbunge huyo kwa kuthamini kitu kinachofanywa na rado kwa maendeleo ya wakazi wa mkoa wa Iringa na mikoa yote inayoizunguka mkoa wa Iringa na kuwaomba wananchi kuendelea kusikiliza radio Nuru fm kwa habari za uhakika,matukio mbalimbali na kwa burudani nzuri.


“Radio yetu inavijana wengi wenye kuhitaji mafanikio na kuisadia jamii na ndio maana wamekuwa wakibuni vitu mbalimbali vinavyoleta tija kwa maendeleo ya taifa hata ukikumbuka hivi karibu tuliendelesha mashindano ya mpira wa miguu yaliyokuwa yanaitwa Ritta kabati challenge cup na yalikuwa na mafanikio makubwa hivyo narudia tena kumshukuru mbunge huyu” alisema chakudika

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...