Wednesday, 8 July 2015

MO, DIAMOND PLATNUMZ KUTIKISA SINGIDA MJINI MCHANA HUU



Mbunge wa Singida mjini, Mh. Mohammed Dewji akishuka kwenye ndege mara tu baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Singida.


Mh. Mohammed Dewji akilakiwa na Mjumbe wa halmashauri kuu CCM (NEC) taifa manispaa ya Singida, Hassan Mazala mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Singida mjini kwa ajili kuhutubia Mkutano mkubwa ambao atawasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya mwaka 2005/2010 na 2010/2015 ambapo Mwanamuziki wa kimataifa Nassib Abdul almaarufu kama Diamond Platnumz atatumbuiza wanaSingida. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya Singida, Jumanne Hamis Nguli.


Mh. Mohammed Dewji akisalimiana na Katibu wa CCM wilaya ya Singida mjini, Magdalena Ndweta.


Mh. Mohammed Dewji akisalimiana na Katibu ambaye pia ni Mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya Singida mjini, Duda Juma.


Mwanamuziki wa kimataifa nchini, Diamond Platnumz akilakiwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya Singida, Jumanne Hamis Nguli.


Mh. Mohammed Dewji akionekana mwenye furaha na tabasamu bashasha akiongoza na Mwenyekiti wa CCM wilaya Singida, Jumanne Hamis Nguli kusalimiana watoto na wananchi waliojitokeza kumlaki katika uwanja wa ndege wa Singida mjini.

Katibu wa CCM Mufindi:Vijana tuepuke kutumika katika kuvuruga amani na utulivu iliopo nchini




 
Katibu wa CCM Wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama

MUFINDI: KATIBU wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mufindi Gimson Mhagama ametoa rai kwa vijana kuepuka kutumika katika kuvuruga amani na utulivu uliopo nchini Tanzania kwa kutumika na baadhi ya vyama vya siasa na kuhatarisha amani ya Taifa. 

Alisema kuwa amani ambayo tunajivunia ipo siku itatoweka na iwapo vyama vya siasa vitaacha kufanya kazi yake ya kisiasa kwa kunadi sera za vyama vyao na kueneza chuki dhidi ya serikali kama ilivyo hivi sasa kwa baadhi ya vyama kuendesha siasa za chuki na kuwatumia vijana kuvuruga amani yetu.

BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA IRINGA LAVUNJWA RASMI...!

Meya wa Manispaa ya Iringa Mstahiki Amani Mwamwindi akufafanua jambo wakati wa kikao cha mwisho cha baraza hilo jana. Kulia kwake walioketi ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza, Mkuu wa Wilaya ya Iringa Andelina Mabula akifuatia na Naibu Meya Gervas Ndaki.

Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kupitia Idara ya Fedha na Biashara imekusanya jumla ya 5,357,849,597/- kati ya hizo 1,010,046,997/- in mapato ya ndani katika kipindi cha kuanzia mwezi Aprili hadi Julai 2014/2015.

Akisoma taarifa ya kazi zilizotekelezwa na kamati ya fedha na uongozi kwa baraza la madiwani lililovunjwa jana, Naibu Meya Gerevas Ndaki kwa niaba ya mwenyekiti wa kamati hiyo, alisema kuwa 4,347,802,600/- ni ruzuku toka serikali kuu kwa ajili ya mishahara, matumizi mengineyo na miradi ya maendeleo.

CCM kuanza kusuka na kunyoa Urais hii leo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dkt. Jakaya Kikwete akifafanua jambo katika moja ya vikao vya kamati kuu.


Chama tawala nchini Tanzania CCM, leo kinaanza mchakato wa kumtafuta mgombea wake kwa ajili ya uchaguzi wa rais wa taifa hilo utakaofanyika mwezi Oktoba.

Mwenyekiti wa chama hicho Rais Jakaya Kikwete atastaafu baada ya uchaguzi huo akiwa amemaliza muhula wake wa pili na wa mwisho madarakani, kwa mujibu wa Katiba.

Wakazi wa Manispaa ya Iringa wa mchangia Mwanahabari Kibiki kuchukuwa fomu ya Ubunge




na fredy mgunda, iringa 

WAKATI joto la uchaguzi nlikiendelea kupanda katika jimbo la Iringa mjini, mamia ya vijana, wanawake, walemavu na wazee katika jimbo hilo wanaendelea kuchangishana fedha ili kumuwezesha mwanahabari Frank Kibiki kuchukua fomu ya kuomba ateuliwe kupeperusha bendera ya CCM, kwenye jimbo hilo.

Zoezi hilo linaloendeshwa na baadhi ya vijana waliomtaka Kibiki ambaye ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM taifa, kutotoa rushwa badala yake atumie hoja kuelezea sera zake, walisema wameamua kuchangishana fedha ili kumuwezesha kijana huyo kuchukua fomu.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...