Katibu wa CCM Wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama
MUFINDI: KATIBU wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mufindi Gimson Mhagama ametoa rai kwa vijana kuepuka kutumika katika kuvuruga amani na utulivu uliopo nchini Tanzania kwa kutumika na baadhi ya vyama vya siasa na kuhatarisha amani ya Taifa.
Alisema kuwa amani ambayo tunajivunia ipo siku itatoweka na iwapo vyama vya siasa vitaacha kufanya kazi yake ya kisiasa kwa kunadi sera za vyama vyao na kueneza chuki dhidi ya serikali kama ilivyo hivi sasa kwa baadhi ya vyama kuendesha siasa za chuki na kuwatumia vijana kuvuruga amani yetu.
Katibu hiyo ambayo alikuwa katibu msaidizi wa CCM Mkoa wa Iringa na kuteuliwa kushiki nafasi ya ukatibu Wilaya ya Mufindi alitoa rai hiyo wakati akikongea na vijana wa stendi ya mafinga pamoja na madereva taxi na bodaboda jana ikiwa ni kazi yake ya kwanza tangu kuteuliwa.
Alisema kuwa Tanzania ni nchi pekee yenye ustawi wa amani barani Afrika na kutoa mfano kwa nchi jirani zinazoonesha madhara ya kuichezea amani na kuongeza kuwa ni rahisi sana kupoteza amani na umoja lakini ni vigumu sana kuirejesha.
“Nawaomba vijana wenzangu kuacha kuandamana kwa kuiga tu kwa kuwa umeambiwa fanya jambo hilo, mbali mwe vijana bora katika kudumisha amani iliyopo na kamwe msije iga siasa vya vyama vya upinzani siasa ya kufanya vurugu,” alisema katibu.
Alisema kuwa moja ya changamoto kubwa inayowakabili vijana na ambayo kwa kushirikiana nao atahakikisha inafanyiwa kazi ni kwa kutumia fursa mbalimbali zinazowazunguka katika sekta ya biashara, kilimo kwa kupitia vikundi vya maendeleo.
Alisema Tanzania ina jumla ya vyama vya siasa 22 na lengo ya kila chama ni kushika dola na kuongeza kuwa vyama vya upinzani bado sana kushika dola na itachukuwa miaka 75 ijao.
Alisema kuwa vyama vya upinzani havina demokrasia ndani ya vyama vyao kwa sababu wenyeviti wa vyama hivyo ni wale wale tofauti na CCM ambapo tumeshuhudia upana wa demokrasia kwa watia nia kuvitokeza kwa wingi zaidi ya 35.
Pia aliwaomba vijana wajitokeze kupiga kura katika uchaguzi mkuu hapo tarehe 25.10.2015 na wasisahau kuipigia kura CCM kwa sababu ni chama pekee chenye uwezo wa kudumisha amani, upendo na mshakamano.
Wakati huohuo, Katibu CCM Wilaya Mufindi ametoa vifaa vya michezo kwa vijana stendi kama vile jezi na mipira kwa ajili ya kuwasaidia kuimarisha afya zao kupitia michezo.
No comments:
Post a Comment