Meya wa Manispaa ya Iringa Mstahiki Amani Mwamwindi akufafanua jambo wakati wa kikao cha mwisho cha baraza hilo jana. Kulia kwake walioketi ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza, Mkuu wa Wilaya ya Iringa Andelina Mabula akifuatia na Naibu Meya Gervas Ndaki.
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kupitia Idara ya Fedha na Biashara imekusanya jumla ya 5,357,849,597/- kati ya hizo 1,010,046,997/- in mapato ya ndani katika kipindi cha kuanzia mwezi Aprili hadi Julai 2014/2015.
Akisoma taarifa ya kazi zilizotekelezwa na kamati ya fedha na uongozi kwa baraza la madiwani lililovunjwa jana, Naibu Meya Gerevas Ndaki kwa niaba ya mwenyekiti wa kamati hiyo, alisema kuwa 4,347,802,600/- ni ruzuku toka serikali kuu kwa ajili ya mishahara, matumizi mengineyo na miradi ya maendeleo.
Alisema kuwa kamati ya fedha na uongozi hiyo iliongozwa na mwenyekiti wake Amani Mwamwindi ambaye pia kulikuwa ni Meya wa Manispaa ya Iringa katika kipindi cha robo ya nne.
Alisema kuwa lengo la mwaka la kukusanya mapato ya ndani ya halmashauri ili kuwa ni kukusanya jumla ya 3,344,443,084/- kati ya 3,873,388,024/= sawa na asilimia 86.
Kwa upande wa ruzuku toka serikali kuu halmashauri ilipokea jumla ya shilingi 24,290,898,004.70 kati ya lengo la shilingi 26,607,093,100/- sawa na asilimia 91.
Aidha, alisema kuwa katika kipindi cha robo ya nne halmashauri ilitumia pia jumla shilingi 5,487,339,738.70 kati ya hizo Tshs. 4,825,568,215/- ni mishahara ya watumishi na Tshs. 661,771,523.70 ni matumizi mwengineyo na miradi ya maendeleo.
“Kwa lengo la mwaka 2014/2015 halmashauri imetumia jumla ya Tshs. 25,005,282,271.80 kati ya shilingi 31,258,652,999.93 sawa na asilimia 80. Kati ya matumizi hayo zaidi ya shilingi bilioni 19 ni matumizi ya mishahara, Tshs. 1,337,837,004.3 ni matumizi menegineyo na Tshs. 4,334,302,931.5 ni miradi ya maendeleo,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Kwa upande wa uwekezaji, kamati hiyo ilishughulikia masuala ya uwekezaji kwa kufanya uthamini wa eneo la mradi wa upimaji viwanja Igumbilo kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo na Uwekezaji (TIB).
Alisema jumla ya wananchi 232 walithaminiwa ardhi yao ambapo fidia ya mali ni Tshs. 1,579,681,809/-.
Mwisho
No comments:
Post a Comment