Monday, 16 April 2018

LIPULI FC YATAMBA KUICHAPA SIMBA SC

Wachezaji wa wakigombania mpira wa kona katika lango la timu ya Lipuli wakati wa mechi dhidi ya Singida United (jezi la rangi ya kijani) ya mkoani Singida katika Uwanja wa CCM Samora mjini Iringa Jumapili. Timu ya Lipuli ilishinda 1-0. (Picha na Friday Simbaya)

Mshambuliaji wa Timu ya Singida United Deus Kaseke mwenye jezi namba saba (7) mgongoni akijaribu kumtoroka Beki wa timu ya Lipuli FC Daruwesh Saliboko katika mechi iliyopigwa Jumapili katika Uwanja wa CCM Samora mjini Iringa. Lipuli FC iliishinda Singida United 1-0. (Picha na Friday Simbaya)


Mshambuliaji machachari wa Timu ya Lipuli ya mjini Iringa Malimi Busungu akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza ndani ya dakika 17 kipindi cha kwanza ya mechi dhidi ya Singida United jana (Jumapili) katika uwanja wa CCM Samora mjini Iringa. Matokeo mechi hiyo Lipuli FC dhidi ya Singida United yalikuwa 1-0. (Picha na Friday Simbaya)



Mashabiki wa Timu ya Lipuli FC wakisangilia timu ya kwa mavuvuzela dhidi ya Singida United ambapo timu yao iliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika Uwanja wa CCM Samora mjini Iringa Jumapili. (Picha na Friday Simbaya) 





IRINGA: Timu ya Lipuli FC ya mjini Iringa imeomba mashabiki na wapenzi kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao itakaposhuka dimbani kuzichapa na Simba SC ya jijini Dar es Salaama Ijumaa wiki hii. 

Timu hiyo imetamba kuwa imejipanga kuibuka na ushindi katika mchezo wake wa Ijumaa dhidi ya Simba SC ya jijini Dar es Salaam unaotarajia kuchezwa katika uwanja wa Kumbukumbu ya Samora mjini hapa. 

Kocha msaidizi wa Timu hiyo Selemani Matola alisema katika mchezo wa Ijumaa wiki hii timu hiyo inatarajia kuifunga Simba, ambapo watakutana na mchezaji wao wazamani Asante Kwasi aliyetimkia Simba. 

"Sisi benchi la ufundi tumelifanyia kazi jambo hilo na sasa tunajipanga kuhakikisha tunaibuka na ushindi katika uwanja wetu wa nyumbani, "alisema Matola. 

Kwa upande wake, Ofisa Habari wa timu hiyo Clement Sanga alisema ushindi katika mechi hiyo ni muhimu kama sehemu ya kujiweka katika nafasi nzuri timu yake lakini pia kupunguza machungu yaliyotokana na kipigo cha Jumatano wiki iliyopita dhidi ya Mwadaui FC ya Shinyanga cha mabao 2-1. 

Timu ya Lipuli ya mkoani Iringa inatarajia kumenyana na kisiki cha mpingo Simba SC ya jijini Dar es Salaam tarehe 20 Aprili mwaka. 

Simba ambao wanaoongza Ligi Kuu msimu wa 2017/18 kwa kuwa na alama 55 wakifuatia na wapinzani wao Yanga waoshika nafasi ya pili kwa kuwa na alama 47, hawajawahi kufungwa hata mechi moja tangu kuanza kwa ligi. 

Hata hivyo, Timu ya Lipuli ya mkoani Iringa imejihakikishia kubaki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzabia Bara baada yakuibamiza Timu ya Singida United Jumapili wiki iliyopita katika mzunguko wa 25 kwa kupata alama 31 na kuendelea kushikilia nafasi ya saba (7) huku Singida United wakiwa na alama 37 nafasi ya tano (5). 

Jumapili iliyopita Lipuli FC walicheza na Singida United katika Uwanja wa kumbukumbu wa Samora mjini Iringa nakushinda 1-0, kupitia kwa mshambuliaji machachari Malimi Busungu dakika 17 ya kipindi cha kwanza cha mchezo. 

Uwanja wa Samora ulilipuka kwa shangwe kutoka kwa mashabiki baada ya mshambuliaji Busungu waliyevalia jezi namba 16 mgongoni kuitikisa nyavu ya Singida United. 

Timu ya Singida United inaoongezwa na Kocha Mkuu Mdachi Hans van der Pluijm aliyezaliwa tarehe 3 Januari mwaka 1949) ambaye pia ni golikipa mstaafu aliyewahi kuchezea timu ya Den Bosch FC katika ya mwaka 1967 na 1986, na baada ya kustaafu soka alikuwa meneja wa Timu ya Den Bosch mpaka 1995. 

Timu ya Lipuli ya mkoani Iringa imerejea ligi kuu Tanzania bara baada ya kupita miaka 17 tangu iliposhuka daraja na mkoa huo kukosa timu ya Ligi Kuu Vodacom kwa kipindi chote hicho. 

Kocha msaidizi wa zamani wa Simba raia wa Uganda Richard Amatre ndiye aliyeipandisha timu hiyo baada ya kusota nayo kwa miaka mitatu ikiishia katika nafasi za pili na tatu. 


WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...