Friday, 26 February 2016

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI

TAMWA YASIKITISHWA KESI ZA UBAKAJI/ULAWITI KWA WATOTO KUTOHUKUMIWA



Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Edda Sanga(katikati) akizungumzia mbele ya waandish wa habari (hawapo pichani) ni kwa jinsi gani wamepata malalamiko kutoka kwa familia zinazofanyiwa unyanyasaji wa kijinsia hasa ubakaji na ulawiti katika ngazi za mahakama, polisi na baadhi ya hospitali hapa nchini.





Mratibu wa Kituo cha Usuluishi cha TAMWA, Bi. Gladness Hemedi Munuo akizungumza mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati walipokuwa wakilaani vikali ucheleweshwaji na upotoshaji wa kesi za vitendo vya ukatili.




Mtoto akitoa ushaidi ni kwa jinsi gani alivyofanyiwa kitendo cha ukatili wa kijinsia.





Mwanasheria wa TAWLA, Mary Richard (wa kwanza kulia) akizungumza ni kwa jinsi gani wanavyowasaidia wanawake wanaofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia leo katika mkutano na waandishi wa habari leo.





Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini.





Chama cha Wanahabari wanawake nchini Tanzania(TAMWA) kimelaani vikali ucheleweshwaji na upotoshwaji ushahidi wa kesi za vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa ubakaji na ulawiti katika ngazi ya mahakama, polisi na baadhi ya madaktari hospitalini. Hali hiyo imekuja baada ya TAMWA kubaini kesi sitini na mbili (62) za ubakaji zimeshindwa kutolewa hukumu au uamuzi na mahakama mbalimbali jijini Dar es Salaam katika kipindi cha mwaka 2014 hadi 2015. 


Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Edda Sanga amesema kati ya kesi 63 za ubakaji, ni kesi moja tu mtuhumiwa amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, kesi arobaini na tatu (43) bado ziko mahakamani, kesi kumi na saba (17) zimeshindwa kufika mahakamani ambapo kesi mbili zimefutwa kwa kukosa ushahidi. 


Pia aliongezea kwa kusema kuwa uongozi wa TAMWA umesikitishwa kuona kesi hizo zikicheleweshwa na vyombo mbalimbali vya serikali ikiwemo jeshi la polisi na mahakama.

Na kuna baadhi ya viongozi wanapokea rushwa ili kuzima kesi za watoto wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia, pia baadhi ya polisi wamekuwa wakishindwa kutoa ushirikiano kwa mlalamikaji ambapo wanatoa maneno ya vitisho na kupelekea mlalamikaji kukosa ujasiri wa kuhifadhi na kutetea kesi yake na wakati mwingine mama mzazi anaandikwa kama mlalamikaji badala ya mtoto mwenyewe aliyefanyiwa ukatili huo. 


Pia wameunga mkono tamko la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliposema wakati wa siku ya sheria duniani kuwa "Kila Hakimu wa Mahakama anapaswa kuhukumu kesi si chini ya 260 kwa kila mwaka na kwa haki", Hivyo basi wao kama TAMWA wanaamini ndani ya mwaka huu Mahakama hapa nchini zitafanya kazi yao kiweledi ili kuweza kupunguza ukatili wanaofanyiwa watoto wa kike.





MTAMBUE KIJANA WA KITANZANIA DESMOND ANDREW ALIYEANZISHA KAMPUNI YA MAWASILIANO YA CW NET




Kijana wa Kitanzania Desmond Andrew alimeanzisha kampuni ya Mawasiliano ya CW Net ambayo inatengeneza Power Bank, Smart Bracelet na Modem. Hakika Tanzania kuna vijana wengi kama Desmond Andrew lakini tatizo kubwa linalowakabili ni upatikanaji wa mtaji wa kuendeleaza vipaji vyao.



Mwanzilishi na mmiliki wa Kampuni ya Mawasiliano
ya CW Net akimtoa ufafanuzi Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Geoffrey Simbeye (aliyevaa suti) kuhusu Smart Bracelet na kazi zake katika maonesho yaliyoandaliwa na shirika la
Viwango nchini Tanzania(TBS) yanayoendelea katika ukumbi wa Mlimani Cityjijini
Dar es Salaam.



Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Geoffrey Simbeye (aliyevaa suti) akiuliza swali mara alipotembelea banda la CW Net maonesho ya Makampuni ya Kitanzania yanayotoa bidhaa yenye viwango vya kutosha hapa nchini.



Smart Bracelet hiki ni kifaa mojawapo kinachotengenezwa na kampuni ya Mawasiliano ya CW Net ambacho kifaa hicho kinahesabu hatua ambazo mtu ametembea nani kwa kiasi gani nguvu uliyoitumia pamoja na kukontrol muda unaolala na unaoamka, pia pia kifaa hicho kinaweza kuunganishwa na simu ya smartphone yako na kutambua simu ikiwa inaita kwa umbali wa mita kumi(10)



Hakika penda cha nyumbani





ACTION AID NA NORAD WAZINDUA MRADI WA KUSAIDIA UBORESHWAJI ELIMU NCHINI



Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Kimataifa la ActionAid nchini, Dkt. Azaveli Lwaitama akitoa neno la ufunguzi wakati wa warsha ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization).(Picha na Modewjiblog).

Katika kusaidia uboreshwaji wa elimu ya Tanzania, Shirika la Kimataifa la ActionAid kwa kushirikiana na serikali ya Norway kupitia Wakala wa Maendeleo na Ushirikiano (NORAD) wamezindua mradi kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization).

Akielezea kuhusu mradi huo, Makamu Mwenyekiti wa ActionAid nchini, Dkt. Azaveli Lwaitama alisema mradi huo unataraji kusaidia uboreshwa wa elimu nchini na zaidi maeneo ya vijijini sehemu ambapo zimekuwa zikionekana kuwa nyuma kielemu.

Alisema ili kupatikana kwa elimu bora kunahitajika uwekezaji wa kuboresha elimu kwa maeneo yote yanayohusika na elimu na inatakiwa kuanza na elimu ya shule ya msingi ili kuweza kumwandaa mwanafunzi kuanzia akiwa mdogo kwa kupata elimu bora inayokidhi viwango vya kimataifa.

“Elimu bora inataka kuwepo kwa uwekezaji kuanzia kwenye shule za msingi kwa kila jambo kama ni uniform, kalamu, uji, walimu kupatiwa stahiki zao na mengine yote yatimizwe,

“Ukitaka elimu bora lazima ujue inahitaji uwekezaji na mradi huu unataka kuongeza fursa kwa wanafunzi kwa kuanzia shule za msingi na zaidi tunaangalia vijijini,” alisema Dkt. Lwaitama.

Nae mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi huo, Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marie Kaarstad alisema Norway na Tanzania wamekuwa wakishirikiana katika shughuli mbalimbali za maendeleo na ana furaha kuona mradi huo unafanyika kwa maendeleo ya baadae ya Tanzania.

Alisema Norway itaendelea kusaidia miradi mbalimbali ya elimu nchini katika kusaidia vijana kupata elimu kuanzia ngazi ya msingi hadi vyuo vya ufundi ili kuweza kuongeza wasomi ambao watasaidia ukuaji wa uchumi nchini.

“Nina furaha kuona mradi ambao utakuwa na mambo muhimu kwa ajili ya maendeleo ya sasa na baadae kwa Tanzania ninataraji kuona miradi inafanikiwa na ushirikiano wa Norway na Tanzania kwa miaka 50 sasa unazidi kuimarika na Tanzania inaushirikiano mzuri na Norway,” alisema Kaarstad.

Kwa upande wa Paul Mikongoti kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu alisema kupitia Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977, ibara ya 11 (2) inaeleza kuwa kila Mtanzania anayo haki ya kujielimisha na kusoma ngazi zote za elimu hadi anapoamua kuacha kuendelea kusoma na hivyo mradi huo utasaidia watanzania kupata haki yao ya kikatiba.

Mradi huo unataraji kufanyika katika wilaya za Kilwa na Singida na utakuwa wa miaka mitatu ambao unataraji kuzifikia shule 60, 30 kwa kila wilaya.

Aidha unataraji kuwafikia wanafunzi wa kiume 7,758 na wakike 8,474 kwa wilaya ya Singida na Kilwa kuwafikia wanafunzi wa kiume 6,607 na wakike 6,546 lakini pia walimu 287 kwa Singida na 290 kwa Kilwa.


Baadhi ya wadau wa sekta ya elimu walioshiriki katika warsha ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization).


Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la ActionAid, Josaphat Mshighati akitoa maelezo kuhusu mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization).

Baadhi ya wadau wa sekta ya elimu walioshiriki katika warsha ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization).


Mshereheshaji wa warsha ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization), Jovina Nawenzake akisherehesha wadau wa sekta ya elimu waliohudhuria uzinduzi huo.


Kalistus Chonya kutoka Ofisi ya Sera katika Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi akielezea kuhusu sera ya elimu inayotumika nchini na mipango waliyonayo ili kuiboresha zaidi.


Paul Mikongoti kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu akielezea kuhusu haki ya elimu kwa watanzania.


Samwely Mkwatwa kwa niaba ya AAT akielezea kuhusu jinsi kodi inavyoweza kusaidia ukujuaji wa elimu Tanzania.


Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marie Kaarstad akifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa mradi kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization).Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Kimataifa la ActionAid nchini, Dkt. Azaveli Lwaitama.


Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marie Kaarstad akisoma hotuba wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization). Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Kimataifa la ActionAid nchini, Dkt. Azaveli Lwaitama.


Baadhi ya wahuzuriaji waliohudhuria katika warsha ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization) iliyoandaliwa na Shirika la ActionAid.


Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marie Kaarstad akizindua taarifa kuhusu mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization).


Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marie Kaarstad akimkabidhi taarifa ya mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization), Kalistus Chonya kutoka Ofisi ya Sera katika Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.


Kwa pamoja wakionyesha taarifa hiyo kwa wahudhuriaji wa warsha hiyo.


Watekelezaji wa mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization), wakisaini mikataba na mwongozaji wa mradi huo.


Mkuu wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Patrick Ezekiel akielezea kuhusu jinsi kodi inavyoweza kusaidia kuinua elimu nchini.


Mratibu Mkuu wa TEN/MET nchini, Cathlee Sakwambo akitoa neno la ufungaji wa warsha ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization).


Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.


WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...