Friday, 14 April 2017
ASKOFU DK.ALEX MALASUSA AONGOZA IBADA YA IJUMAA KUU KATIKA KANISA LA KKKT
Muumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Azania Front, Moses Kombe (katikati) na wenzake wakiigiza igizo la kumbukumbu ya kuambwa msalabani kwa Yesu Kristo miaka 2000 iliyopita katika ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika kanisa hilo jijini Dar es Salaam leo jioni.
Igizo likiendelea.
Askofu mstaafu Dk. Alex Malasusa akisalimiana na waumini wa kanisa hilo baada ya ibada ya Ijumaa Kuu.
Muonekano wa waumini wakati wa ibada hiyo.
Kwaya Kuu ya Ushairika huo ikitoa burudani ya nyimbo za kifo chake Yesu Kristo wakati wa kuhitimisha ibada hiyo.
Waumini wa kanisa hilo wakiwa nje kwa kuhitimisha ibada hiyo.
Waumini wakitakiana kheri ya Ijumaa Kuu baada ya ibada hiyo.
VIJANA WASHAURIWA KUUNGA MKONO MABADILIKO NDANI YA CHAMA
Katibu wa masuala ya kisiasa na mahusiano ya kimataifa Kanal mstaafu Ngemela Lubinga akizungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo mkoani Iringa juzi. (Picha na Friday Simbaya)
|
CHAMA Cha mapinduzi (CCM )kimewataka vijana kuunga mkono mabadiliko yanayofanywa na chama hicho ka kuwa yanalnga kuleta ufanisi ya chama.
Kauli hiyo na katibu wa masuala ya kisiasa na mahusiano ya kimataifa Kanal mstaafu Ngemela Lubinga juzi kwenye mkutano wa CCM wakati akizungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo mkoani Iringa ambao ni wanachama cha CCM.
Alisema kuwa kuna watu wanabeza mabadiliko yaliyofanywa na chama hicho hivi karibuni mjini Dodoma na kuongeza kuwa mabadiliko hayo yanalenga kuboresha utendaji ndani ya chama.
Viongozi wa CCM wa kata na matawi pamoja na wananchi mbalimbali waliohudhuria mkutano huo uliyofanyika mjini Iringa juzi.
Lubinga alisema kuwa viongozi walioteuliwa na rais ambao wameondolewa kwenye nyadhifa mbalimbali kuacha kupiga kelele na hivyo kutaka walioondolewa kuyakubali mabadiliko ya mfumo, huku akiwataka walioondolewa kuheshimu busara za Ikulu kwa maamuzi hayo.
“Rais anapoteuwa viongozi wake kuwapa dhamana anaona kwamba wewe anakuhitaji katika nafasi hiyo na mazingira yaliyopo yanakuhitaji unaweza kuyamudu, lakini inapofika wakati anakuondoa ujue kwamba mazingira yale huwezi kuyamudu na anakuokoa ili usipate laana.”alisema Lubinga.
Alisema kuwa busara za Ikulu ziheshimewe na zisijadiliwe kwamba na hasitoke mtu akasma sijapata kwa sababu baadhi ya viongozi wameondolewa madarakani lakini wamebaki wakilalamika mitaani hovyo.
Lubinga alisema chama hicho kimejipanga kimkakati kuhakikisha kinajenga nidhamu na uwajibikaji ndani ya serikali na kuwaondoa watendaji wote ambao wanaonekana kuwa kikwazo katika utekelezaji wa mipango ya serikali ya kujenga uchumi imara kupitia sekta ya viwanda na uzalishaji.
Alisema kuwa chama wakati kinafanya mabadiliko kilichukua hatua ya kuona wapi kinakwama na nani anakikwamisha kwa kula rushwa au kwa kuwa mnafiki.
Kanali Lubinga alisema kuwa hatua iliyochukuliwa kwa kuona kwamba kinafanya kitu chenye uhakika kikaona kwamba watu waovu waondolewe ndani ya chama.
“Maoni yalikuja kila mtu aliitwa na kujieleza na alipojieleza alitolewa ushahidi wa kutosha kwamba wewe… unakubali au unakataa na ndio hao wameondolewa kwa kuona walikisaliti chama.”alisema Lubinga.
Katika hatua nyingine alisema kuwa waliosababisha jimbo la Iringa mjini kupotea sio wananchi wapiga kura bali ni viongozi wake.
“Iringa mmeona viongozi wa juu walitupa matatizo, Iringa bado kuna shida kidogo, kuna vita vya ndani kwa ndani, bado kuna maadui wadogowadogo na mkiamua mtayamaliza, lakini kiukweli waliosababisha kupoteza jimbo la Iringa kupotea sio wananchi wapiga kura waliwapa kura vizuri kabisa bali ni viongozi wake ndio waliofanya mkalipoteza sasa jengeni Iringa Mpya.
Alisema kuwa kusudio la CCM kufanya mabadiliko ya kuwaondoa watu waovu ni kusudio zuri na wale ambao kama wapo wengine wajiandae.
“Tunalalamika rushwa mmeona madhara ya rushwa katika shughuli zenu za kila siku na ninyi wananchi mmeona matatizo yenu ambayo yanatokana na rushwa sasa hao watu wa nini ndani ya chama?alihoji Lubinga.
Pia alisema kuwa chama kimemua kufanya mabadiliko ili kuendana na hitaji,jamii yoyote duniani inayo utaratibu wake wa kutimiza wajibu wake ili iweze kuendana na hitaji liliopo mabadiliko katika uongozi na mabadiliko katika utendaji.
Aidha aliongeza kuwa CCM katika kujifanyia kujitathimini chenyewe kimeamua kupunguza idadi ya vikao ndani ya chama, kupunguza idadi ya wajumbe kwa baadhi ya vikao na kurudisha madaraka chini kwa wananchi ili mambo yaende vizuri.
Kwa upande wao katibu wa (UVCCM) Mkoa wa Iringa Abdulikarim Halanga na Marko Mbanga ambaye ni katibu wa CCM wilaya ya Iringa waliwataka wana CCM hao kuwa waadilifu na wazalendo kwa sababu mbadiliko hayo ni ya kukijenga chama kuwa CCM mpya na Tanzania mpya.
Subscribe to:
Posts (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
The most deadly form of tuberculosis is one that lies in wait inside the body for years, attacking at the first sign of weakness. Abou...