Saturday, 20 January 2018

SHILINGI MILIONI 100 ZAKOPESHWA KWA WANAWAKE NA VIJANA MUFINDI

Sehemu ya Viongozi wa Makundi 37 ya Wanawake na Vijana wakiwa ndani ya ukumbi wa Halmashauri kupokea hundi za Vikundi vyao.


Viongozi katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Vikundi wakiwa wameshika hundi zilizoambatishwa na Vocha.


Jumla ya s
hilingi Milioni 100, zimetolewa kwa sharti la Mkopo kwa vikundi vya Wanawake na Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, ikiwa ni utekelezaji wa takwa la sheria inayozitaka mamlaka za Serikali za mitaa nchini kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa lengo la kuwakopesha vijana na Wanawake ili wajiajiri kupitia shughuli za kijasirimali hivyo kuboresha maisha yao.

Akisoma taarifa ya Mikopo hiyo, Mkuu wa Idara ya maendeleo ya jamii Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Bw. Hatibu Bwashehe, ametanabaisha kuwa, kati ya vikundi hivyo, vikundi 22 vya wanawake vimekopeshwa jumla ya shilingi Milioni 62, wakati vikundi 15 vya Vijana vimenufaika na Mkopo huo kwa kupata shilingi Milioni 38.

Akizungumza kabla ya kukabidhi hundi kwa walengwa, mgeni wa heshima katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mh. Jamhuri William, amevitaka vikundi hivyo vielewe kuwa, fedha wanazopokea ni Mkopo hivyo, zitumike kulingana na maandiko waliyowasilisha badala ya kuzitumia kwa malengo tofauti kama vile kuchangia harusi au kununua mavazi ya kifahari na kuongeza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa kutorejesha fedha za Serikali.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mh. Festo Ngina, amepongeza mwenendo mzuri ya urejeshaji Mikopo kwa vikundi vilivyokopeshwa kiasi cha shilingi Milioni 300 kwa mwaka wa fedha uliopita wa 2016 – 2017 na akaongeza kuwa ili hali ya urejeshaji izidi kuwa bora zaidi, Watendaji wa kata na Vijiji watahusika kufuatilia marejesho hayo kama ambavyo wanahusishwa kwenye chakato kusajili vikundi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mtendaji wa wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Profesa Riziki Shemdoe, amewahimiza Vijana na Wanawake wa Halmashauri hiyo kuendelea kuwasilisha maombi kwa kuwa Halmashauri yake tayari imetenga fedha nyingine kiasi cha shilingi Milioni 140 ambazo watazikopesha baadaye mwezi ujao mara baada ya kukamilisha uchambuzi wa maandiko ambayo yatakuwa yanalenga kuanzisha viwanda Vidogo.

Aidha, wanufaika wa Mkopo huo ambao ni Wanawake na Vijana, wameipongeza Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais John Pombe Magufuli, kwa kuwathamini na kuwapatia mikopo hiyo huku wakiahidi kuzitumia kwa malengo na kurejesha kwa wakati.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...