Monday, 6 February 2017

WALIOGOMEA MAITI HOSPITALI YA AMANA KWENDA KWA WAZIRI WA AFYA



Mama wa mtoto huyo, Julieth Daudi 





Na Dotto Mwaibale

SAKATA la Julieth Daudi (19) mkazi wa Tabata Relini pamoja na ndugu zake kususia kuchukua mwili wa mtoto aliyejifungua kwa madai kuwa mtoto huyo hakuwa wake baada ya kubadilishiwa na wauguzi wa Hospitali ya Amana katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam baada ya kujifungua limechua sura mpya kufuatia wazazi hao kutaka kwenda kumuona Waziri wa Afya kufikisha kilio chao.

Akizungumza na Jambo Leo nyumbani kwao Dar es Salaam jana, Daudi alisema tunahitaji kwenda kumuona Waziri waAfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kwa hatua zaidi kutokana na kitendo hicho walichofanyiwa na wauuguzi hao.

"Mimi pamoja na ndugu zangu tutakwenda kumuona waziri ili kumpelekea malalamiko yetu" alisema Daudi.

Akizungumzia mkasa huo Daudi alisema alifika Hospitalini hapo Februari 2 jioni akiwa amesindikizwa na mama yake Veronica Lucas na shangazi yake Judith Christopher.

"Nilipofika daktari aliponipima aliniambia kuwa hasikii mapigo ya mtoto isipokuwa ya kwangu hivyo alishauri siku iliyofuata nipate kipimo cha utrasaund lakini kabla ya kipimo hicho nilijisia uchungu na kujifungua" alisema Daudi.

Daudi alisema baada ya kupita muda kidogo muuguzi aliyemzalisha alimfuata na kumueleza kuwa mtoto wake alikuwa amefariki na alipomuuliza alikuwa wa jinsia gani muuguzi huyo alimweleza kuwa alikuwa hajui kama alikuwa wa kiume au wa kike.

Aliongeza kuwa wakati yupo wodini alimuona kijana mmoja aliyevalia koti la hospitali akiwa amembeba mtoto ambaye hakujua alikokuwa amempeleka.

Alisema baada ya kuambiwa mtoto wake amefariki aliomba aonyeshwe lakini hakuoneshwa tangu saa tatu asubuhi ambapo alilazimika kwenda kuomba simu kwa mlinzi wa hospitali hiyo na kuwajulisha ndugu zake walipofika nao waliomba kuonyeshwa mwili wa mtoto huyo bila mafanikio.

Shangazi wa Julieth Judith Christopher alisema baada ya kutokea tukio hilo walikwenda kumuona Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ambaye aliitisha kikao baina ya ndugu pamoja na maofisa wengine wa hospitali hiyo ambacho hakikufikia muafaka baada ya ndugu hao kukataa kuuchukua mwili wa mtoto huyo wakidai si wa kwao.

Aliongeza kuwa mganga mkuu huyo aliwaeleza kuwa mtoto huyo alikuwa amefia tumboni baada ya mimba hiyo kuharibika na ndiyo sababu mtoto huyo alizaliwa akiwa mfu.

"Wanafamilia tumegoma kuuchukua mwili wa mtoto huyo na maamuzi yaliyofikiwa ni kufanyika kipimo cha DNA" alisema Christopher.

Alipopigiwa simu Muuguzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Beauty Mwambebule alisema hawezi kulizungumzia tukio hilo kwenye simu njia ya simu badala yake alimtaka mwandishi wetu kwenda hospitali kupata undani wa jambo hilo.

Mayrose pamoja na Baadhi ya Watanzania Waishio Marekani Katika Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa 2017



Mtaalam wa Maendeleo ya Watu Mayrose Kavura Majinge akieleza umuhimu wa Kanuni ya Dhahabu "The Golden Rule" Katika kuondoa Ufisadi na maovu mbalimbali katika jamii yetu. Fuatilia Habari kamili: maadilikitaifa.blogspot.com




Profesa Nicholls Boas wa Chuo Kikuu Maryland Marekani akiwa miongoni mwa wadau Watanzania waishio Marekani akifurahia jambo wakati wa Siku Maalum ya Kuwezesha Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa iliyofanyika Katika ukumbi wa Quality One Care, Maryland Marekani.



Baadhi ya wadau wa Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa kutoka maeneo mbalimbali nchini Marekani wakifuatilia kwa makini Maudhui ya Siku Maalum ya Kuwezesha Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa iliyofanyika Katika ukumbi wa Quality One Care Silver Spring, Maryland Nchini Marekani




Baadhi ya wadau wa Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa kutoka maeneo mbalimbali nchini Marekani wakifuatilia kwa makini Maudhui ya Siku Maalum ya Kuwezesha Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa iliyofanyika Katika ukumbi wa Quality One Care Silver Spring, Maryland Nchini Marekani.

NDUGU WAGOMEA MAITI YA MTOTO HOSPITALI YA AMANA




Mzazi Julieth Daudi (19) mkazi wa Tabata Relini, akiwa Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam, alipozungumza na mwanahabari akidai amebadilishiwa mtoto aliyejifungua. 




Mama mzazi wa Julieth, Veronica Lucas akiwa ameshika shavu kwa masikitiko kufuatia tukio hilo.



Shangazi yake Julieth, Judith Christopher akielezea tukio hilo 


kwa mwanahabari.



Julieth Daud (kulia) akiwa na dada yake nje ya wodi ya wazazi katika Hospitali hiyo.





Julieth (aliyekaa kushoto), akiwa na ndugu zake nje ya 
wodi ya wazazi katika Hospitali hiyo. 


Na Dotto Mwaibale

MZAZI Julieth Daudi (19) mkazi wa Tabata Relini pamoja na ndugu zake wamegoma kuchukua mwili wa mtoto kwa madai kuwa mtoto huyo hakuwa wake kutokana na kubadilishiwa na wauguzi wa Hospitali ya Amana katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kujifungua.

Akizungumza kwa masikitiko nje ya viwanja vya hospitali hiyo Dar es Salaam jana, Daudi alisema kitendo alichofanyiwa kimemuumiza sana pamoja na ndugu zake wengine.

Alisema alifika Hospitalini hapo Februari 2 jioni akiwa amesindikizwa na mama yake Veronica Lucas na shangazi yake Judith Christopher.

"Nilipofika daktari aliponipima aliniambia kuwa hasikii mapigo ya mtoto isipokuwa ya kwangu hivyo alishauri siku iliyofuata nipate kipimo cha utrasaund lakini kabla ya kipimo hicho nilijisia uchungu na kujifungua" alisema Daudi.

Daudi alisema baada ya kupita muda kidogo muuguzi aliyemzalisha alimfuata na kumueleza kuwa mtoto wake alikuwa amefariki na alipomuuliza alikuwa wa jinsia gani muuguzi huyo alimweleza kuwa alikuwa hajui kama alikuwa wa kiume au wa kike.

Aliongeza kuwa wakati yupo wodini alimuona kijana mmoja aliyevalia koti la hospitali akiwa amembeba mtoto ambaye hakujua alikokuwa amempeleka.

Alisema baada ya kuambiwa mtoto wake amefariki aliomba aonyeshwe lakini hakuoneshwa ambapo alilazimika kwenda kuomba simu kwa mlinzi wa hospitali hiyo na kuwajulisha ndugu zake walipofika nao waliomba kuonyeshwa mwili wa mtoto huyo bila mafanikio.

Shangazi wa Julieth Judith Christopher alisema baada ya kutokea tukio hilo walikwenda kumuona Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ambaye aliitisha kikao baina ya ndugu pamoja na maofisa wengine wa hospitali hiyo ambacho hakikufikia muafaka baada ya ndugu hao kukataa kuuchukua mwili wa mtoto huyo wakidai si wa kwao.

Aliongeza kuwa mganga mkuu huyo aliwaeleza kuwa mtoto huyo alikuwa amefia tumboni baada ya mama yake kuiharibu mimba hiyo kwa nia ya kuitoa na ndiyo sababu mtoto huyo alizaliwa akiwa mfu.

"Wanafamilia tumegoma kuuchukua mwili wa mtoto huyo na maamuzi yaliyofikiwa ni kufanyika kipimo cha DNN na ili mama wa mtoto aruhusiwe kutoka hospitali inatakiwa ipelekwe barua ya mwenyekiti wa mtaa wake anakoishi" alisema Christopher.

Muuguzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Beauty Mwambebule alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo hakuwa tayari kuzungumza kwa njia ya simu badala yake alimtaka mwandishi wetu kwenda hospitali kupata undani wa jambo hilo.

Serikali yatangaza ‘Diploma’ ndiyo kigezo cha chini cha elimu kwa waandishi wa habari



Serikali imetangaza kuwa kiwango cha chini cha taaluma anayopaswa kuwa nayo mwandishi wa habri kuwa ni 'Diploma ya Uandishi wa Habari' kwa mujibu wa kanuni za sheria mpya ya hunda za habari zilizokamilika utungaji wake hivi karibuni.


Akizungumza na wana habari leo mjini Dodoma, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo , Nape Nnauye amesema kuwa kanuni zimeshaundwa na zimechapishwa kwenye gazeti la serikali tangu Februari 3 mwaka huu baada ya kupokea maoni ya wadau mbalimbali.


"Tumesoma, tumechambua maoni ya wengi, wapo waliotaka iwe cheti, wengine diploma, wengine digrii, wapo waliotaka PhD na wapo waliotaka iwe mtu yeyote nayejua tu kusoma na kuandika. Serikali imesimama katikati ya maoni hayo. Sifa ya chini kabisa kwa kuanzia itakuwa ni diploma ya uandishi wa habari” Amesema Nape


Waziri Nape amesema pia kuwa sheria hiyo imeshaanza kutumika tangu Desemba 31 mwaka 2016, ambapo yeye kama Waziri mwenye dhamana alishatoa tangazo katika gazeti la serikali.


Aidha kuhusu wasio na sifa hiyo, Waziri Nape amesema kuwa serikali imetoa kipindi cha mpito cha miaka mitano ili waandishi wasiokuwa na sifa hiyo, waliopo sasa na watakaoingia kwenye taaluma hiyo, wakasome ili wawe wamepata sifa hiyo.


Amesema katika utekelezaji wa sheria hiyo, kuna taasisi ambazo tayari zipo, zitaongezewa majukumu au kazi zake kuhuishwa, pia kuna vyombo vipya vitaanzishwa na kuna taratibu mpya za kiutendaji zitaandaliwa.


Kuhusu manufaa ya sheria hiyo, Nape amesema kuanza kutumika kwa sheria hiyo ni jambo muhimu kwa tasnia hiyo kwa kuwa ni ruhusa ya kuanza kwa mchakato wa kuifanya taaluma ya habari kuwa taaluma kamili yenye sifa mahsusi na maadili yaliyokamilika pamoja na kuwa na vyombo vya kusaidia utekelezaji wake.


Sheria hiyo ilisainiwa na Rais Magufuli Novemba 16 mwaka 2016, na siku mbili baadaye ilichapishwa kwenye gazeti la serikali baada ya muswada wake kupitishwa na Mkutano wa 5 wa bunge mwezi Novemba 2016.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...