Monday, 15 October 2012

MASHINDANO YA MGOSI CUP 2012

PASCAL MGOSI MDHAMINI


TIMU YA RED STARS WAKISHANGILIA GOLI

MASHABIKI WA TIMU YA RUWAWAZI AKIMURUSHA JUU KIPA WA TIMU RUWAWAZI BAADAYA KUIBUKA MABINGWA KOMBE LA MGOSI


MWENYEKITI WA SORUFA, HAMDANI HAMDANI KITANGAZA UTARATIBU WA KUTOA ZAWADI MBALIMBALI

SHABIKI

TIMU YA RED STARS ALIVAA JEZI YA JANO NA RUWAWAZI WALIVAA JEZI YA BLUU



PENALTI


PENALTI




Na Friday Simbaya, Peramiho


TIMU ya Ruwawazi kutoka Kata ya Lilambo imeibuka mabingwa baada ya.kuichapa Timu ya Red Stars ya Kata ya Peramiho mabao 6-5 kwa njia ya mikwaju ya penalti katika fainali ya Mashindano ya Kombe la Mgosi (Mgosi Cup 2012) yaliyofanyika Peramiho jana, Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.

Awali timu hizo zilitoka sare ya kufungana mabao 2-2 katika ndani ya dakika 90 na baadaye kuijia moja kwa moja kipindi cha mikwaju, ambapo Red Stars ilikosa penalti mbili wakati Timu ya Ruwawazi ilipata penati zote.

Katika kipindi cha kwanza Timu ya Ruwawazi walipata bao la kwanza kupitia mshambuaji mchachali Geradi Steven dakika 21. Hadi kipindi cha kwanza kuisha Ruwawazi ilikuwa inaongoza 1-0.

Kipindi cha pili timu ya Red Stars ilirudisha goli mapema kupitia mshambuaji wake Basil dakika 58 na baadaye sana kuongeza goli la pili katika dakika 85 kupitia mshambuaji Edu. Kabla Red Star nao hawajakaa sawa sawa Ruwawazi walirudisha goli pili kupitia mshambuaji machachali Mobi Kangaluka dakika 87 kabla mpira kiisha.

Mwamuzi wa mechi ya fanali hiyo ya mashindano ya mgosi walikuwa ni Bw.Alfons Luoga wakati makamsaa walikuwa ni Bw. Milinga akisaidina na Bw. Mukoba.

Mashindano hayo yalianza mnamo tarehe 14.08.2012 na kumalizika 14.10.2012 na kushirikisha timu 10 kutoka kata za Peramiho na Lilambo, wilayani Songea, Mkoa wa Ruvuma, ambapo mdhamini wa mashindano hayo alikuwa mfanyabiashara mmoja wa Peramiho, Bw. Pascal Mgosi.


Akiongea na gazeti la mwenge mdhamini wa mashindano, Pascal Mgosi aliomba wadau wa mpira wa miguu pamoja na michezo mingine kujitoka na kudhamini michezo katika maeneo haya ili kuweza kukuza kiwango cha michezo na kuibua vipaji.

Aliongeza kuwa akiwa kama mfanyabiashara mdogo wameweza kudhamini mashindano hayo kwa nini isiwezekane hata kwa wadu wengine?, alihoji Mgosi.


Hata hivyo Bw. Mgosi aliseam kuwa malengo ya mashindano hayo ni pamoja na kukuza na kuboresa michezo kwa vijana wa kiume na wakike, kupunguza uzururaji, kupunguza tabia mbaya hasa za maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) yanayotokana ulevi wa kupidukia, kudumisha undugu na umoja na kuongeza kipato kupitia biashara ndogondogo wakati wa mashindano.

Kwa upande wa zawadi, mshindi wa kwanza aliibuka na kitita cha shilingi laki mbili (200,000/-) ambao ni Timu ya Ruwawazi FC, mshindi wa pili alijipatia shilingi laki na nusu (150,000/-) ambao ni timu ya Red Stars na ushindi wa watatu ulikwenda kwa Timu ya Mwanamonga FC kutoka pia Kata ya Lilambo, kwa kupata kifuta jasho cha 50,000/-.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...