Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akipozi na bango la picha lenye rangi mbalimbali zinazowakilisha malengo ya dunia 17 kwa Maendeleo Endelevu wakati wa mdahalo kwenye juma la Umoja wa Mataifa ambalo linamalizika leo katika maadhimisho ya miaka 70 tangu kuundwa kwa umoja huo. Mdahalo huo umefanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jana. (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Na Mwandishi wetu
RAIS Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa ametoa wito wa kufanyika kwa mabadiliko katika mfumo wa uendeshaji wa Umoja wa Mataifa ili kukidhi mahitaji ya sasa ya dunia.
Mkapa alisema hayo jana katika mdahalo kwenye juma la Umoja wa Mataifa ambalo linamalizika leo katika maadhimisho ya miaka 70 tangu kuundwa kwa umoja huo. Mdahalo huo umefanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jana.
Mkapa ambaye alichukua muda wake mwingi kuelezea na kuangalia maslahi ya Umoja wa Mataifa kwa dunia na changamoto inazokabiliana nazo, alisema kwa muda sasa dunia inataka mabadiliko katika uendeshaji wa Umoja huo lakini wanaonufaika na mfumo wa sasa wamekuwa wagumu kukubali mabadiliko.
Alisema kuna mambo sasa yanatokea yanayohatarisha usalama wa mataifa, lakini hatua zinazopendekezwa zinashindwa kuchukuliwa kutokana na kuendelea kuwapo kwa tabia ya vita baridi kati ya mataifa makubwa yenye kura ya veto katika umoja huo.
Alisema yeye anaungana na watu wengine duniani wanaotaka mabadilio katika Umoja huo yatakayozingatia jiografia za kisiasa duniani zinazoweza kusaidia kuinua uwezo wa utekelezaji wa Vyombo vya Umoja wa Mataifa likiwemo baraza Kuu na Baraza la Usalama.
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akipozi na Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mh. Fionnuala Gilsenan.
Alisema kwamba yapo baadhi ya mataifa na wakazi wa dunia hii ambao wanataka kuondolewa kwa kura ya turufu inayomilikiwa na mataifa kadha kutokana na makubaliano ya vita kuu ya pili ya dunia.
Alisema anafahamu kwamba Afrika inakubaliana na suala hilo kimsingi ingawa lina changamoto yake kwamba nini kitatokea kama kura hiyo ya turufu itaondolewa.
Hata hivyo, Mkapa alisema kwamba masuala ya usalama wa dunia ni nyeti sana kubaki katika mikono ya watu wachache na kutaka uwezo huo kupewa dunia kwa kuiwekeza katika sheria ya kimataifa inayotaka uwajibikaji wa pamoja katika masuala ya usalama.
Alisema katika kongamano hilo la vijana kwamba Afrika imepitisha azimio la pamoja Machi 8,2005 la kutaka mabadiliko makubwa katika vyombo vya Umoja wa Mataifa na umoja wenyewe.
Mapendekezo hayo yaliyotambulika kama makubaliano ya Ezulwini yanataka mabadiliko makubwa katika uendeshaji wa vyombo vyote vikubwa vya Umoja wa Mataifa ikiwamo baraza la Usalama, baraza Kuu na ECOSOC.
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez na Balozi wa Ujerumani nchini, Mh. Egon Kochanke.
Alisema anaomba Mungu mabadiliko hayo yaje kwa kuelewana lakini si kwa sababu iliyoanzisha Umoja huo na vyombo vyake, vita kuu ya pili ya Dunia.
Alisema hali bora ya baadae ya dunia kimsingi inategemea ushirikiano wa mataifa huru kama ilivyoelezwa katika nadharaia zenye uhalisia kamili.
Alisema pamoja na kwamba kunachangamoto nyingi Umoja huo umekuwa jukwaa jema la kuangalia mustakabali wa dunia na wakazi wake.
“Umoja wa Mataifa umefanyakazi njema kabisa katika maeneo ya misaada ya kiutu, utunzaji wa mazingira na maendeleo ya jamii na uchumi” alisema na kuongeza kuwa anasikitishwa na watu wanaoitazama UN katika upande wa siasa pekee na kulalamikia.
Alisema Umoja wa Mataifa na mashirika yake wamekuwa wakifanyakazi kubwa na shughuli zao kwa kipindi kikubwa zimekuwa zikienda vyema kwa kutoingiliwa na siasa za Baraza la Usalama.
Mkapa alisema akiwa mwafrika ambaye nchi yake ilishawahi kusimamiwa na Umoja huo na sasa ina miaka 54 ya Uhuru atakosa shukurani kwa jinsi umoja huo ulivyohangaika kuondoa ukoloni barani Afrika.
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez katika picha ya pamojan na Naibu Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Kwacha Chisiza.
Alisema kwamba UN imekuwa ikifanya vyema kuandaa mataifa hayo kujitawala.
Aidha alimpongeza Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon kwa juhudi zake na hasa hotuba yake aliyoitoa Malabo, Equatorial Guinea Juni mwaka jana wakati alipozindua sherehe za miaka 70 za Umoja wa Mataifa.
Alisema katika miaka 70 Umoja huo umefanikiwa kutokomeza ubaguzi wa Rangi barani Afrika, kukabiliana na maradhi na kupambana kutengeneza amani na kuzuia vita.
Alisema pamoja na mafanikio hayo miradi na mipango ya maendeleo ambayo yameweka dunia katika mstari mmoja kama malengo ya millennia na sasa malengo ya maendeleo endelevu yamefanya dunia kuwa na sauti moja katika kukabili umaskini na kulinda dunia iwe mahali bora pa kuishi.
Alisema kutokana na malengo ya millennia watu wanaoishi katika umaskni wamepungua kwa zaidi ya nusu kutoka watu bilioni 1.9 kwa mwaka 1990 hadi watu milioni 836 kwa mwaka 2015.
Aidha mdondoko wa wanafunzi umepungua kwa asilimia 43 kutoka watoto milioni 100 kwa mwaka 2000 hadi watoto 57 kufikia mwaka 2015 na kupunguza pengo la wasiojua kusoma miongoni mwa wanawake na wanaume.
Aidha alisema changamoto za vifo na uzazi na uharibiofu wa mazingira kwa sasa ndio zinazotakiwa kushughulikiwa wakati dunia inaadhimisha miaka 70 ya uwapo wa Umoja wa Mataifa.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Awa Dabo akipozi na lengo namba 8 kati ya malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia.
Awali akimkaribisha rais mstaafu kuzungumza, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe alisema wakati umefika kwa vijana kujua muskabali wa dunia na maendeleo yake.
Alisema vijana ambao kwa sasa ndio wengi wanapaswa kushirikishwa katika kubuni na kutekeleza mikakati ya kimaendeleo.
Naye Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez pamoja na kumshukuru rais Mstaafu kwa kukubali kuzungumza na vijana katika maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja huo amesema hoja alizotoa rais huyo wa zamani ni za msingi na zinazostahili kuangaliwa.
Alisema amefurahishwa na jinsi Kiongozi huyo wa zamani alivyouzungumzia Umoja wa Mataifa kwa kuangalia mwanzo wake na maazimio ya awali ya kwanini umoja huo ni muhimu hasa katika suala la amani na usalama.
Naibu Mkurugenzi Mkazi, Oparesheni wa UNDP, Bw. Titus Osundina.
Alisema hoja aliyozungumza Mkapa ya kuwajibika kwa pamoja kwa amani na usalama wa dunia na hivyo kushughulikia masuala yenye kuleta tishio kama mabadiliko ya tabia nchi, umaskini na kuondoa baa la njaa, rais huyo amegusa vionjo muhimu vinavyotakiwa kuangaliwa.
Aidha alisema mabadiliko aliyokuwa akizungumzia rais Mkapa ya Umoja huo ambayo yanatakiwa kuzingatia usalama wa dunia yanawezekana kutokana na jinsi nchi zinavyowajibika.
Aidha alimshukuru kwa kuzungumzia maendeleo kwanza ya millennia na yale endelevu.
Mratibu huyo alisema kwamba Umoja wa Mataifa utaendelea kufanyakazi na serikali ya Tanzania kuhakikiksha kwamba malengo yaliyowekwa ya uwapo wake yanafanikiwa na watanzania wanaendelea kufaidi program zinazoendeshwa kwa pamoja kwa manufaa ya ustawi wa nchi.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem na Mwakilishi Msaidizi wa Shirika hilo, Christine Kwayu wakipozi na mabango yanayowakilisha kati ya malengo ya dunia 17 kwa Maendeleo Endelevu.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Joyce Mends-Cole pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy.
Kutoka kushoto ni Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mindi Kasiga pamoja na Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu wakipozi na bango la picha lenye rangi mbalimbali zinazowakilisha malengo ya dunia 17 kwa Maendeleo Endelevu.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Awa Dabo (katikati) akipozi na vijana kutoka vyuo mbalimbali walioshiriki mdahalo huo ulioendeshwa na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jana.
Vijana wakiendelea kupozi na namba mbalimbali kati Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (katikati) na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez (kushoto) wakimlaki Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa alipowasili katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jana jijini Dar.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa akisaini kitabu cha wageni katika chumba maalum kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jana jijini Dar. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe akiongozana na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mh. Benjamin William Mkapa kuingia kwenye ukumbi wa mikutano. Nyuma yao ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez wakibadilishana mawazo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Rais mstaafu Benjamin Mkapa kuzungumza na hadhira iliyoshiriki Kongamano la Umoja wa Mataifa lililofanyika jana jijini Dar.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mh. Benjamin William Mkapa akimshukuru Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe kwa ukaribisho.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin Mkapa akizungumza Kongamano la Umoja wa Mataifa lililofanyika jana jijini Dar es salaam katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere.
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez (kulia) akimpongeza Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin Mkapa kwa hotuba nzuri. Kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim akifuatiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe.
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akitoa salamu za Umoja wa Mataifa kwenye kongamano hilo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akitoa neno la shukrani kwa washiriki.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe akisoma maneno yaliyoandikwa kwenye tuzo aliyokabidhi Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa. Kushoto ni Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Alvaro Rodriguez akijianda kukabidhi tuzo hiyo.
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Alvaro Rodriguez (kushoto) akimkabidhi Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin William Mkapa tuzo ya Umoja Mataifa kwa kutambua mchango wake katika malengo ya millennia (MDGs) na kuwezesha Mashirika ya Umoja wa Mataifa kutoa huduma kama taasisi moja. Anayeshuhudia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe wakati wa Kongamano la Umoja wa Mataifa lililofanyika jana jijini Dar es salaam katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere.
Mtandao wa vijana wanaopambana uharibufu wa mazingira (Youth Climate Activists Network), Fadhili Meta akiuliza swali Je Serikali inamikakati gani ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi?
Mwanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Blesira Mukandala akitoa maoni yake kwa Umoja wa Mataifa ambapo aliuomba Umoja huo kuwatazama Walemavu kwa jicho la pili kama makundi mengine yanayofaidika na msaada wa mashirika ya Umoja huo.
Pichani juu na chini ni Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania viongozi wa serikali, wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa pamoja na wadau wa maendeleo wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mdahalo huo.
Vijana pamoja na wanavyuo kutoka vyuo mbalimbali nchini wakifuatilia majadiliano yaliyokuwa yakiendelea kwenye mdahalo huo.
Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania pamoja na wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa pamoja na wadau wa maendeleo wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mdahalo huo.
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali za sekondari nchini walioshiriki mdahalo huo.
Ukumbi ukiwa umefurika wanafunzi, mabalozi, viongozi wa serikali, wanafunzi na wadau wa maendeleo wakati wa mdahalo kwenye juma la Umoja wa Mataifa ambalo linamalizika leo katika maadhimisho ya miaka 70 tangu kuundwa kwa umoja huo. Mdahalo huo umefanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jana.
Maafisa kutoka UNESCO wakifuatilia mijadala mbambali iliyokuwa ikiendelea ukumbini hapo Kulia ni Nancy Kaizilege na Rehema Sudi (katikati).
Maafisa habari na mawasiliano wa mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania Jacqueline Namfua na Sawiche Wamunza wakifurahi jambo ukumbini hapo.
Meza kuu katika picha ya pamoja na mabalozi waalikwa pamoja na wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania.
Meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya makundi ya vijana walioshiriki kongamano hilo.
Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na Wizara ya Mambo ya Nje.