Tuesday, 13 October 2015

Mdahalo wa wagombea ubunge Jimbo la Iringa Mjini washindwa kufika mwisho...!


Msigwa

Mwakalebela

Kisinini

Masasi

Washiriki

washiriki

Viongozi wa vyama vilivyoshiriki

Waansdishi wa habari (Picha zote na Friday Simbaya)


Mdahalo wa wagombea ubunge katika Jimbo la Iringa Mjini, jana ulishindwa kufikia tamati kutokana na wafuasi wa wagombea wa vyama hasa CCM na Chadema kuanzisha fujo zinazotokana na ushabiki.

Mdahalo huo ulianza saa 6:30 na ulikuwa umalizike saa 9:00 jioni lakini ulilazimika kumalizika saa 8:40 baada ya hali ya hewa kuchafuka kutokana na wafuasi wa Mgombea wa CCM Frederick Mwakalebela na wa Chadema Mchungaji Peter Msigwa kukamiana na kuanza kurushiana maneno ya kejeri na vijembe.

Hatua hiyo ilianza mara baada ya washiriki kutakiwa kuuliza maswali yanayolenga maendeleo ya wana Iringa wote bila kujali itikadi zao za vyama na ambayo yangejibiwa na wagombea wote sita wa ubunge katika jimbo hilo, lakini wafuasi wa vyama hivyo viwili hasimu hawakuzuia hisia zao kwa kuuliza maswali yanayolenga kumshambulia mgombea aidha wa Chadema au CCM na hivyo kuzua hali ya kuzozana.

Mdahalo huo ulikuwa umeandaliwa na Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa (IPC) kwa kushirikiana na Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC), ambapo Mwenyekiti wake Frank Leonard anasema malengo ya kuandaa mdahalo huo ni kutoa fursa kwa wananchi wa Iringa Mjini kusikiliza sera za wagombea wao na kuwauliza maswali namna watakavyotatua changamoto zinazowakabili wananchi. 

Pamoja na Msigwa na Mwakalebela wagombea wengine walioshiriki mdahalo huo Daud Masasi wa chama cha ADC na Robert Kisinini wa DP, huku Chiku Abwao wa ACT-Wazalendo na Paulina Mgimwa wa Chusta wakishindwa kushiriki.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...