Tumaini Msowoya,
Iringa
VITENDO vya wabunge wa CCM kuhamisha samani na vitu vingine kwenye ofisi za wabunge majimboni, jana liliibukia Iringa Mjini ambako mbunge mpya kwa tiketi ya Chadema, Peter Msigwa amedai kuikuta ofisi ikiwa imeondolewa kila kitu, ikiwa ni pamoja na kung'olewa kwa mapazia.
Msigwa anadai kuwa vitu hivyo vimeondolewa na mbunge aliyemaliza muda wake, Monica Mbega, ambaye alianguka vibaya kwenye uchaguzi wa mwaka huu baada ya kuliongoza jimbo hilo kwa miaka kumi.
Kitendo hicho kimeibuliwa siku chache baada ya taarifa za kuondolewa thamani na vitasa kwenye ofisi ya mbunge wa Jimbo la Nyamagana. Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha ndiye aliyeng'oa samani hizo baada ya kushindwa na mgombea wa Chadema, Ezekiel Wenje.
Akizungumza na wanahabari ofisini kwake jana, Msigwa ambaye alianza kazi Jumatatu, alidai aliikuta ofisi hiyo ikiwa katika hali ya uchafu huku ikiwa haina mapazia, kompyuta, simu, nyaraka wala faili za kuhifadhia taarifa muhimu licha ya kuwa ilikuwa ikitumika katika kipindi kilichopita.
Alisema kuwa kutokana hali ya uchafu, alilazimika kupaka rangi ofisi hiyo iliyo katika jengo la
Halmshauri ya Manispaa ya Iringa na kisha kufunga simu mpya baada ya ile iliyokuwepo kuonekana imenyofolewa.
“Ofisi nimeikuta katika hali ya uchafu sana; haina simu wala nyaraka yoyote inayoonyesha kama ofisi hii ilikuwa ikifanya kazi katika kipindi kilichopita. Hali hii ni hatari ikiwa kweli, viongozi tuna nia ya kuwatumikia wananchi,” alisema Mchungaji Msigwa.
Alisema kuwa hakuna makabidhiano mazuri ambayo yamefanyika katika ofisi hiyo na kwamba amelazimika kuanza na kutengeneza vitasa ambavyo vilikuwa vimeharibika, ili kuhakikisha ofisi hiyo inakuwa katika hali ya usalama.
Alisema alipotaka kujua sababu ya ofisi kuwa katika hali hiyo, alidai kujibiwa kuwa vifaa vilivyokuwemo vilinunuliwa na Monica Mbega na kwamba kwa kuwa amemaliza muda wake, amelazimika kuondoka na kila kitu ambacho alinunua kwa ajili ya kulitumikia jimbo hilo.
“Nimeuliza kwa nini ofisi hii haina kitendea kazi wala nyaraka yoyote inayoonyesha kwamba ilikuwa ikifanya kazi, jibu nililopewa ni kwamba Mama Mbega andiye aliyenunua hivyo kwa hiyo ni vitu vyake na ameamua kuondoka navyo,” alisema.
Alipopigiwa simu na Mwananchi ili azungumei madai hayo, Mbega alikata simu mara baada ya mwandishi kujitambulisha kuwa anatoka gazeti hili.
Pia simu hiyo iliendelea kukatwa pale mbunge huyo wa zamani alipopigiwa mara ya pili na ya tatu na baada ya hapo ilikuwa ikiita bila majibu.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Theresia Mahongo alisema licha ya kwamba ofisi hiyo ipo kwenye jengo la halmashauri hiyo, inahudumiwa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Hata hivyo, katibu tawala wa Wilaya ya Iringa, Gidion Mwinami alisema ofisi yake haijawahi kufanya tathmini kujua ndani ya ofisi hiyo kulikuwa na nini hivyo ikiwa kweli, Mbega alinunua vifaa hivyo, ana haki ya kuondoka navyo.
“Sifahamu kulikuwa na nini, na sisi hapa hatujaletewa oda kwamba ofisi ya mbunge inahitaji kuwa na nini. Kama kweli vifaa vilivyokuwepo alinunu mbunge aliyepita, ni haki yake,” alisema.
Alisema kuwa anachofahamu yeye ni kwamba ofisi hiyo ya mbunge inapaswa kuhudumiwa na serikali na kwamba meza moja sambamba na makochi ndivyo vilivyokuwepo, lakini hajui kama kulikuwa na kitu kingine zaidi ya hivyo.
“Kulalamika ni hulka ya mtu, nyie mmefika na kuona kuwa hapo kuna upungufu wa kitu gani; kama pazia pisi ngapi hazipo? Sisi hatujafanya tathmini kubaini hili ila tutafanya hivo,” alisema
Msigwa alisema kutokana na ukweli kwamba, uongozi wa jimbo ni wa kupokezana kwa kuzingatia ridhaa ya wananchi, ni vyema mbunge anayekuwa madarakani akajitahidi kuhifadhi nyaraka ili mbunge anayeanza ajue kilichofanyika, na wananchi gani walihudumiwa tofauti na hali ilivyo katika ofisi hiyo.
Hata hivyo, alisema kuwa yupo katika mchakato wa awali wa kuajiri mwanasheria kwa ajili ya kusikiliza matatizo ya wananchi wanaohitaji msaada wa kisheria ambao wamekuwa wakikosa haki zao kwa kutojua sheria.
Subscribe to:
Posts (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
The most deadly form of tuberculosis is one that lies in wait inside the body for years, attacking at the first sign of weakness. Abou...