HALMSHAURI ya Mji wa Mafinga mkoani Iringa yakopesha jumla vikundi 60 vya kina mama na vijana kutoka kila kata jumla ya 121,121,300/= ambapo vikundi arobaini (40) ni kina mama na vikundi ishirini (20) ni vijana.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Mafinga Saada Mwaruka alisema jana kuwa katika kuendelea kutekeleza maagizo mbalimbali ya Serikali halmashauri ya Mji wa Mafinga imeweza kukopesha jumla vikundi 60 vya kina mama na vijana kwa kipindi cha mwezi mmoja.
Alisema kuwa Halmshauri ya Mji wa Mafinga ilianza kutoa mkopo wa 50,500,000/= kwa vikundi arobaini vya kina mama na 25,500,000/= kwa vikundi ishirini vya vijana na mara baada ya vikundi vyote kufanya marejesho vizuri na kupata faida ya kupata faida fedha taslimu 31,121,300/= na kufikia 107, 121,300/=.
Mwaruka alisema Halmashauri ya Mji Mafinga imeongeza tena jumla ya fedha 14, 000,000/= na hivyo kufanya jumla kuu ya mikopo yote iliyotolewa kufikia 121,121,300/=.
Halmashauri ya Mji Mafinga ni moja kati ya Halmshauri zilizopo mkoa wa Iringa,halmashauri ina jumla ya kata tisa (9) na mitaa thalathini.
Katika kuendelea kutekeleza maagizo mbalimbali ya Serikali halmashauri ya Mji wa Mafinga imeweza kukopesha jumla vikundi 60 vya kina mama na vijana kutoka kila kata jumla ya 121,121,300/= kwa kipindi cha mwezi mmoja ambapo vikundi arobaini (40) ni kina mama na vikundi ishirini (20) ni vijana.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Mafinga Bi.Saada Mwaruka amesema halmashauri inatarajia tena kutoa mkopo wa awamu ya pili wakati wowote kuanzi a sasa.