Thursday, 8 February 2018

MAKAMU WA RAIS KUFANYA ZIARA YA SIKU TANO MKOANI IRINGA





MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya kikazi katika Mkoa wa Iringa kesho Ijumaa, ambapo atatembelea wilaya za Iringa, kilolo na Mufindi. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alisema ziara hiyo ya siku tano (5) itaanza kesho tarehe 09/02/2019 hadi tarehe 13/02/2018. 

Alisema kuwa katika ziara hiyo, Makamu wa Rais anatarajia kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo zinazotekelezwa mkoani hapa na serikali pamoja na sekta binafsi, na kufanya mikutano ya hadhara. 

Masenza alisema kuwa makamu wa rais atafungua wodi katika zahanati ya Kijiji cha Kising’a wilayani Iringa, kukagua upanuzi wa kiwanda cha Ivori kilichopo manispaa ya Iringa na kiwanda cha kufungashaji mazao ya mbogamboga. 

Aidha, makamu wa rais atazindua jengo la utawala katika shule ya sekondari Kilolo, kuweka jiwe la msingi kwenye maabara ya shule ya sekondari Mgololo, kufugua zahanati ya Mtili na atakagua kiwanda cha utengenezaji mkaa Mafinga. 

Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa tarehe 12/02/2018, makamu wa rais akiwa mkoani Iringa atazindua mradi wa kuendeleza utalii ukanda wa kusini (REGROW) ambapo mkoa wa Iringa ni kitovu cha Utalii. 

Alisema uzinduzi huo utafanyika eneo la Kihesa Kilolo na baadaye kufanya mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Mwembetogwa katika Manispaa ya Iringa. 







No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...