Monday, 25 July 2011
WAKAZI WA LUNDUSI
Wakazi wa Kijiji cha Lundusi Kata ya Peramiho wilayani Songea, Mkoani Ruvuma wakisaidiana Bi. Clementina Mlowe (mwenye Khanga nyekundi na kilemba)kupukuchua na kujaza mahindi kwenye mifuko. Mkazi huyo wa Lundusi amebahatika kuvuna gunia 80 za mahindi.
BUMPER HARVEST IN RUVUMA REGION
Na Friday Simbaya,
Songea
Wakati mikoa ya Arusha na Kilimanjaro inakabiliwa na uhaba wa chakula kutokana na mvua za masika na vuli kutonyesha vizuri katika msimu wa kilimo mwaka huu, Mkoa wa Ruvuma unasemekana kuwa na chakula cha ziada kutokana na mavuno mzuri ya chakula msimu huu.
Wakati huohuo, wakazi wa vijiji vya Lundusi na Maposeni Wilayani Songea Mkoani Ruvuma wameipongeza serikali kwa mpango kabambe wake wa ‘Kilimo Kwanza’ wa vocha ya ruzuku ya pembejeo uliyowapelekea wananchi wengi kupata mavuno kabambe katika msimu wa mavuno ya mwaka huu.
Wakiongea na Nipashe jana katika nyakati tofauti, wakazi hao walisema kuwa ni jambo la busara sana kwa serikali kwa kuwawezesha wakulima kupata mavuno mazuri msimu huu kutokana na mkakati mzuri wa vocha za ruzuku ya pembejeo.
Walisema kuwa katika maeneo mengi wa Mkoa wa Ruvuma, wakulima wamepata mavuno ya chakula mazuri hasa mahindi, kwa kutumia vyema mvua za masika na zile za vuli, zilizonyesha vizuri msimu huu.
Katika kuhakikisha kuwa zoezi la kilimo na mkakati wa taifa wa ‘Kilimo Kwanza’ unakwenda vizuri, serikali ilijitahidi kurekebisha lile lililojitokeza miaka iliyopita, kwamba pembejeo zinawahi na kuwafikia wakulima walengwa wakati mwafaka.
Utaratibu uliyowekwa na serikali unalenga kuhakikisha kwamba mnufaika na vocha, anakuwa mwananchi mkulima wa kawaida ili kusudi aweze kuboresha uzalishaji na kuondokana na baa la njaa na kuongeza kipato kidogo.
Clementina Mlowe makazi wa Kijiji cha Lundusi alisema kuwa hapo zamani walikuwa wanalima kutumia mbegu za kawaida na kupata mavuno kidogo, lakini tangu serikali ianzishe mpango wa vocha za ruzuku ya pembejeo, mavuno yameongezeka na kuimarika sana.
Alisema kuwa mwaka huu amebahatikia kuvuno magunia 80 ya mahindi akilinganisha na miaka ya nyuma kabla ya mpango wa serikali wa vocha za ruzuku ya pembejeo.
“Kwa kweli sisi wakulima wadogo wadogo tumenufaika na mkakati wa serikali wa Kilimo Kwanza unakwenda vizuri cha msingi pembejeo ziwafikie walengwa msimu wa kilimo ukiwa umeanza,” alisisitiza Bi. Clementina.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Maposeni, Bw. Deo Jordan Komba alisema hali ya mavuno ya chakula katika kijiji chake msimu huu nzuri, karibu maeneo mengi wananchi wamepata mahindi, na kuongeza kwa asilimia kubwa wamevuna mahindi mengi na kupelekea kijiji hicho kuwa na ziada ya chakula.
“Lakini, pamoja na kuwa mavuno kambambe, ni rai yangu kwa wananchi wote wa Kijiji cha Maposeni wahifadhi chakula vizuri ili kuepukana na baa la njaa baadae, kwa sababu kuna mikoa mingine hali ya mavuno haikuwa nzuri sana,” alsema mwenyekiti.
Mkoa wa Ruvuma ni mmoja katika ya mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ijulikanayo kama ‘The Big Five’ yenye mavuno mazuri ya chakula cha mahindi msimu huu.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa pamoja na kuwepo mavuno mazuri ya mahindi katika maeneo mengi ipo haja kwa wananchi kutunza mahindi vizuri, katu wasiuze mahindi yote.
Mwananchi mwingine wa Mtaa wa Ujamaa katika Kijiji cha Maposeni alisema kuwa suala la pembejeo za ruzuku zimesaidia sana kuongeza mavuno ya chakula katika maeneo mengi nchini, lakini mpango mzima unatakiwa kuangaliwa upya kutokana na kasoro ndogo ndogo zinazojitokeza, unaosababisha na baadhi ya watendaji na viongozi wa vijiji katika kugawa vocha hizo.
“Lengo la serikali la kuwawesha wakulima wadogo wadogo kupitia mpango wa vocha za ruzuku ya pembeojeo za kilimo ni mzuri sana, lakini baadhi watendaji wa vijiji wanaharibu kwa kuwabagua wakulima na wakati mwingine rushwa inatumika,” alisema mwananchi huyo kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini.
Kijiji cha Maposeni kianzishwa tangu mwaka 1974 wakati wa opresheni ya sogeza vijiji iliyofanywa na serikali wakati hao, lakini Shule ya Msingi ya Maposeni ilianzishwa mwaka 1947 enzi za wakoloni.
Katika upande wa elimu, Kijiji cha Maposeni kina Shule ya Sekondari moja tu ya Daraja Mbili na shule za msingi mbili ya Maposeni na Namakinga. Shule ya Msingi ya Maposeni kwa sasa inakabiliwa upungufu mkubwa wa walimu.
Shule ya Sekondari ya Daraja Mbili inakabilikwa pia tatizo la walimu hasa katika masomo ya sayansi pamoja na uhaba wa vifaa vya maabara.
Mwanafunzi wa Kidato cha Tatu, katika Shule ya Sekondari Daraja Mbili ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, aliambia Nipashe kuwa tangu shule ianzishwe mwaka 2007, wanasomo masomo ya sayansi kinatharia kutokana na uhaba wa vifaa vya maabara na maabara yenyewe.
“Huwa na tunasikia tu Bunsen burner, test tube, beaker n.k, lakini hutujawahi kuviona vitu hivyo, huwa tunasimuliwa tu na mwalimu kwa mdomo, na pengine kuchorwa ubaoni tu,” alisema mwanafunzi huyo.
Aliongeza kuwa kuna jengo la maabara linaendea kujengwa hapo shuleni, lakini linachukuwa muda mrefu kukamilika kupitia mpango wa TASAF II.
Kijiji cha Maposeni kina wakazi zaidi 2,280 kutokana Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2000, visima nane vya pampu, zahanati moja yenye wauguzi watatu tu. Wakati mwingi wananchi asilimia kubwa na tumia visima vya jadi.
Tatizo la maji nalo ni kubwa katika kijiji cha Maposeni kwani asilimia kubwa ya wakazi wa kijiji hicho hutumia maji ya visima vya jadi, ambayo maji yake si safi na salama sana.
Mwisho
Subscribe to:
Posts (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
The most deadly form of tuberculosis is one that lies in wait inside the body for years, attacking at the first sign of weakness. Abou...