Saturday, 20 August 2016

WANAOWAPA MIMBA WATOTO WA SHULE NA KUWAOA HATA MAGEREZA YAKIJAA WATAENDELEA KUKAMATWA




Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (wa pili kulia), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa kukusanya nguvu za pamoja kulinda haki za wasichana nchini Tanzania awamu ya pili Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi kutoka Shirika la CDF, Kashuma Mtengeti, Mwakilishi wa Shirika la Comic Relief Uk, DFID, Jane Miller na Mwenyekiti wa Bodi ya Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF), Foturnata Temu.



Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.



Mwakilishi wa Shirika la Comic Relief Uk, DFID, Jane Miller, akizungumza katika mkutano huo wakati akimkaribisha Wazir Ummy Mwalimu (kulia)



Mwenyekiti wa Bodi ya Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF), Foturnata Temu (kulia), akizungumza katika hafla hiyo wakati akitoa taarifa ya mradi huo.





Na Dotto Mwaibale


SERIKALI imesema hata magereza zikijaa itaendelea kuwakamata na kuwachukulia sheria kali wanaume wote wataka0 bainika kuwaoa au kuwapa mimba wanafunzi.


Hayo yalisema na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati akizindua mradi wa kukusanya nguvu za pamoja kulinda haki za wasichana nchini Tanzania awamu ya pili Dar es Salaam leo.

Mwalimu alisema kuwa hata magereza yakijaa kwa kiasi gani serikali haitasita kuwakamata watuhumiwa hao bila ya kuwaonea huruma bila ya kujali mtuhumiwa ni mtu wa namna gani.


"Nawaagiza maofisa Ustawi wa Jamii wote katika ngazi ya mikoa, wilaya na Kata kuhakikisha haki za mtoto zinalindwa nchini kote hususan mtoto wa kike. Ninataka wahakikishe wale wote wanao wapa watoto wa shule mimba na wanao waozesha au kuoza wanakamatwa na kuchukuliwa hatua haraka kwani sheria za kuwalinda watoto zipo, kinachotakiwa sasa ni utekelezaji" alisema Mwalimu.


Waziri Mwalimu alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye kiwango cha juu cha ndoa za utotoni ambapo taarifa ya Demografia na Afya ya mwaka 2010 zimeonesha kuwa kwa wastani wanawake 2 kati ya watano Tanzania wa umri wa miaka 15-49 waliolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka 18.


Aliongeza kuwa utafiti wa hali ya afya ya uzazi, mtoto na malaria wa mwaka 2015/16 unaonesha kuwa idadi ya wasichana wanaopata watoto katika umri wa miaka 15-19 imeongezeka kufikia asilimia 27 mwaka 2015 kutoka asilimia 23 mwaka 2010 na kuwa tatizo hilo lipo zaidi katika mikoa ya Katavi kwa asilimia 36.8, Tabora, asilimia 36.5, Simiyu asilimia 32.1, Geita asilimia 31.6 na Shinyanga kwa asilimia 31.2.


Mwenyekiti wa Bodi ya Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF), Foturnata Temu alisema katika kudumisha harakati za kupambana dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia na mimba za utotoni vinavyoendelea kuwakumba wasichana nchini Tanzania, CDF, Chama cha Uzazi na Malezi (Umati) na Kituo cha Wadada Centre wameamua kuzindua mradi huo kwa pamoja ili kulinda haki za wasichana hapa nchini.

MLIMBWENDE WA TAJI LA MISS MWANZA 2016 APATIKANA


Usiku wa jana Ijumaa Agost 19,2016 kuamkia leo Jumamosi Agost 20,2016, kulikuwa na mtifuano mkali wa kumtafuta mlimbwende wa taji la MISS MWANZA 2016 ambapo warembo 16 kutoka wilaya mbalimbali mkoani Mwanza walijitosa kusaka taji hilo.




Ilikuwa ni furaha kubwa kwa mrembo, Mary Peter (katikati), pale alipotangazwa kuwa MISS MWANZA 2016. Pia mwendelezo wa furaha uliwaendea warembo, Victoria Boniphace (kushoto) aliyetangazwa Miss Mwanza nambari mbili na Winnie Shayo (kulia), aliyetangazwa Miss Mwanza nambari tatu.




Kinyang'anyiro cha Miss Mwanza 2016, kiliandaliwa na Kampuni ya "Big D Entertainment" na baada ya kinyang'anyiro hicho, unafuata mtifuano wa MISS LAKE ZONE 2016 utakaofanyika Septemba 10,2016 ambapo washiriki wa Miss Mwanza 2016 waliongia nafasi tano bora, wanashiriki moja kwa moja kwenye shindano hilo.

Na BMG


Miss Mwanza 2015, Donny Roberty (kushoto), akimkabidhi taji Miss Mwanza 2016, Mary Peter (kulia) baada ya kuibuka mshindi wa shindano hilo.


Washiriki wa Miss Mwanza, walioingia nafasi tano bora



WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...