Sunday, 21 May 2017
Six Civil Servants Of Iringa Municipality Dismissed For Absenteeism
IRINGA: The Council of councilors in the Municipal Council of Iringa, Iringa Region has dismissed six civil servants from work and restoring back one (Lucy Mtafwa) to work for various charges, including absenteeism.
Iringa Municipality Mayor Alex Kimbe, who is also the chairman of the council of councillors mentioned the staff affected by the penalties for absenteeism that is Glory Ngowi, Anzawe Mvena, Francis Mtenge, Paul Sanga, Mkombozi Gendagenda and Tumaini Sanga.
Kimbe told a session of the House of Councilors of Iringa Municipal Council yesterday (Saturday) that the staff six (6) has been dismissed due to absence from their work stations without any notice.
"Staff were absent from work for more than two years and have been dismissed due to lack of work for more than two years without the permission of his employer contrary to the Code of Civil service of the year 2003, and from today on 20 May, 2017 the above staff are no longer workers of Iringa Municipality Council, "said Kimbe.
In addition, the Chairman of the House of Councilors said that the committee has bring back Lucy Mtafwa to work after ratification of the committee that she had committed no errors in service and will eventually be returned to work has suggested by the council.
Meanwhile, Iringa Municipal Council has collected more than 400 million shillings (400m / -) tax revenue for March 2017.
Iringa Municipality Mayor Alex Kimbe to recognize the contribution of the management of tax collection he gave compliments and conferred the certificates of revenue collection within the council to some civil servants in charge the exercise.
During the session of the council of councillors of the third quarter of the year 2016/2017, the mayor said revenues are due to tariff posters and licenses.
The session of councilors in Iringa Municipality of the third quarter of the year 2016/2017, sat and discussed many issues including development projects including the firing of six civil servants for various charges, including absenteeism at work.
Watumishi Sita Manispaa Ya Iringa Wafukuzwa Kazi Kwa Utoro
Meya wa
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Alex Kimbe akifungua kikao cha baraza la
madiwani cha robo ya tatu ya mwaka 2016/2017 wa halmashauri hiyo leo
unaofanyika katika Ukumbi wa Manispaa ya Iringa jana. (Picha na Friday Simbaya)
Meya wa
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Alex Kimbe akimkabidhi mmoja ya watumishi wa
halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Musa Mwaihojo (kulia) cheti cha pongezi ya
ukusanyaji wa mapato ya ndani ya halmashauri hiyo, ikiwa ni pamoja na ushuru wa
mabango na leseni wakati wa kikao cha baraza la madiwani cha robo ya tatu
ya mwaka 2016/2017 wa halmashauri hiyo leo unaofanyika katika Ukumbi wa
Manispaa ya Iringa jana. (Picha na Friday Simbaya)
BARAZA la Madiwani katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, mkoani Iringa limewafukuza kazi watumishi wake sita na kumrudisha kazini mmoja kwa tuhuma mbalimbali, ikiwemo utoro kazini.
Meya wa Manispaa ya Iringa Alex Kimbe, ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la madiwani aliwataja watumishi hao waliokumbwa na adhabu hiyo kwa utoro kazini kuwa ni Glory Ngowi, Anzawe Mvena, Francis Mtenge, Paul Sanga, Mkombozi Gendagenda na Tumaini Sanga.
Kimbe alikiambia kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Iringa jana (Jumamosi) kuwa watumishi hao sita (6) wamefukuzwa kazi kutokana na kutokuwepo kwenye vituo vyao vya kazi bila taarifa yoyote.
“Watumishi hawakuwepo kazini kwa zaidi ya miaka miwili na wamefukuzwa kutokana na kutokuwepo kazini kwa zaidi ya miaka miwili bila ruhusa ya mwajiri wake kinyume na Kanuni za Utumishi wa umma za mwaka 2003, na kuanzia leo tarehe 20 mwezi Mei, mwaka 2017 watajwa hapo juu sio watumishi wa halmashauri ya Manispaa ya Iringa,” alisema Kimbe.
Aidha, Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani huyo alisema kuwa halmashauri hiyo imemrudisha kazini Lucy Mtafwa baada ya kamati kuridhia kuwa hakutenda makosa ya kiutumishi na hatimaye baraza lilipendekeza mtumishi huyo arudishwe kazini.
Wakati huo huo, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imekusanya zaidi ya shilingi milioni 400 (400m/-) kodi ya mapato kwa mwezi Machi mwaka 2017.
Meya wa Manispaa ya Iringa Alex Kimbe kwa kutambua mchango wa usimamizi wa ukusanyaji kodi aliwatunuku vyeti vya pongezi vya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya halmashauri baadhi ya watumishi waliosimamia zoezi hilo.
Akiongea wakati wa kikao cha baraza la madiwani cha robo ya tatu ya mwaka 2016/2017, meya huyo alisema mapato hayo ni kutokana na ushuru wa mabango na leseni.
Kikao cha baraza la madiwani halmashauri ya Manispaa ya Iringa cha robo ya tatu ya mwaka 2016/2017, kilikaa na kujadili taarifa mbalimbali za miradi ya maendeleo pamoja kuwafukuza kazi watumishi sita kwa tuhuma mbalimbali, ikiwemo utoro kazinina kumrudhi mmoja kazini.
Subscribe to:
Posts (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
The most deadly form of tuberculosis is one that lies in wait inside the body for years, attacking at the first sign of weakness. Abou...