Wednesday, 5 January 2011
MWANAMKE AZAA MTOTO WA KWANZA BAADA YA MIAKA 20 KWENYE NDOA
Otilinda Mambi (38), mkazi wa Kijiji cha Milongi Kata ya Lusewa Wilayani Namtumbo, ni mmoja wa wazazi saba waliojifungua siku ya mkesha wa Mwaka Mpya katika Hospitali ya St. Joseph Mission Hospital Peramiho, Mkoani Ruvuma.
Watoto saba waliyozaliwa siku ya mkesha wa Mwaka Mpya katika Hospitali ya Misheni ya Mtakatifu Joseph ya Peramiho mkoani Ruvuma, wakiwemo wakike wanne na wakiume watatu ni pamoja na mama mwenye umri wa miaka 38 ambaye ameishi katika ndoa zaidi miaka 20.
Mambi aliolewa tangu mwaka 1990 na mume wake Winfred Ngonyani katika Kijiji cha Milongi kata ya Lusewa wilayani Namtumbo lakini hawakubahati ka kupata mtoto hata mmoja, hali ambayo ilipelekea majirani kuwanyoshea vidole kuwa ni watu wasio zaa.
Lakini kabla sijaendelea na kisa hiki, hebu tuangalie tafsiri ya maana ya ndoa ni nini? Ndoa ni chombo cha mume na mke chakufanya kazi za ustawi wa ujamii na uimarishaji wa familia. Kudumu kwa ndoa hutegemea jinsi mume na mke wanavyokiendesha na kukitunza chombo hicho.
Katika mtazamo wetu wa kiafrika ndoa maana yake ni kuwa na watoto na ndoa bila watoto haiheshimiki na jamii inayoizunguka, na vile vile inakuwa kama gundu au mkosi.
Naam, Otilinda Mambi alikaa kwenye ndoa miaka yote na kuvumilia matusi yote na kejeri za watu za kusema yeye ni mgumba, wengine walidiriki kumuita maneno kama sio raia wa Tanzania na mambo mengi….. lakini mgumba sasa amezaa!
“Tumehangaika na mume wangu kwa miaka mingi sana na tulionana wataalamu mbalimabali kuhusu maisha yetu ya ndoa na mume wangu bila mafanikio yoyote, tumeenda kwa waganga wa jadi nako kulikuwa hakuna kitu…. Tumezunguka hospitali huku na kule bila ya mafanikio lakini kudra za Mwenyezi Mungu imewezakana,” amesema mama huyo.
Amesema alivumilia hali hiyo kwa miaka yote aliyoishi kwenye ndoa yake mpaka ilifikia hatua ndugu wa mume wake wakawa wanamshauri achane na yeye (Otilinda) kwa vile hazai, ili akatafute mwanamke mwingine anayeweza kumzalia watoto.
Mume wangu Winfred Ngonyani aliupokea ushauri wa ndugu zake na kuamua kuoa wanamke mwingine ambaye hata hivyo mwanamke huyo hakubahatika kuzaa naye ….yaani bila mafankio.
Mumewe hakuwahi kumtesa pamoja mambo yote hayo kwa vile nilimpatia ruksa ya kuoa mwanake mwingine ili akajaribu pengine naweza kubahatika kupata mtoto, ila shida ilikuwa kwa ndugu za mumewe. Hali iliendea kuwa hivyo na mume wake akihangaika huku na kule mwishowe akabahatika kupata watoto wawili kutoka kwa mwanamke mwingine na watoto wanaishi nao mpaka hivi sasa.
Amesema ,” Mama huyo mwenye watoto wawili huwa anakuja kuwasalimia watoto wake pale nyumbani bila shida yoyote”
“Mnamo Machi mwaka jana 2010, nilianza kuhisi mabadiliko mwilini na nikamwambia mume wangu anisindikize nikapime mimba. Tulipofika hospitali na kupata vipimo niliambiwa kuwa nina ujauzito, sikuaamini macho yangu mpaka hadi leo nimepata mtoto siku hii mkesha wa mwaka mpya… mwaka huu kwa kweli umekuja na neema”
Aidha, amesema kuwa mara nyingi wanawake wanakuja kujifungulia katika hospitali ya St. Joseph Mission Hospital Peramiho kwa vile kuna huduma mzuri sana za afya …Mungu awabariki madaktari wa hospitali hii kwa vile nimejifungua mtoto wangu wa kwanza wa kiume ijapo kwa njia ya opresheni.
“Nilipofika siku chache kabla ya kujifungua niliwaza kwamba itakuwaje….nilikuwa mbishi nilitaka nijifungulie hospitali ya huko kijiji nyumbani kwanza kwa njia ya kawaida lakini wazo likanijia la kwenda hospitali ndiyo ni kaamua kwenda Peramiho na sikutaka kujifungulia pale Kituo cha cha nyumbani kwa sababu ya maneno ya watu pale kijijini. Nilipofika hospitalini madaktari waliniomba nifanyiwe upasuaji kwa sababu mtoto hakukaa vizuri tumboni kwa hiyo ni bora nikafanyiwa upasuaji ilikuokoa maisha ya mtoto na mimi mwenyewe pia”
“Sasa watu pale kijijini kwetu wanamsumbua mume wangu kila mara wanamuuliza ntarudi lini kutoka hospitali ili wanifanyie sherehe kwa kuhakikisha kama kweli nimezaa mtoto au laa, pamoja na kunipa pongezi kwa vile nimekaa muda mrefu kwenye ndoa bila kupata mtoto. Nasikia wananiimbia wimbo ule wimbo uliyozoeleka wa kwamba mgumba sasa amezaa, Hayawi hayawi sasa yameshakuwa……..” alielezea kwa mwandishi hapo hospitalini alipolazwa.
Hata hivyo, Otilinda Mambi amewaomba wanandoa wenye matatizo kama yake wasikate tamaa ila waendelee kumuomba Mungu kwa kila jambo kwa sababu Mungu Mwenyezi nimuweza wa yote.
Kwa upande wao madaktari pale Hospitali ya Peramiho, wamesema si ajabu kumuona mtu mwenye umri kama wa Otilinda kuzaa kawaida baada ya miaka mingi bila kuzaa isipokuwa ina shauriwa watu kama hao wafanyiwe upasuaji kama ni uzao wa kwanza na kwamba mtu kama huyo anatafuta kitu kinachoitwa ‘Precious Baby’, kwa hiyo njia salama ni kumfanyia opresheni kwa sababu kuna asilimia kubwa ya kuweza kumpata mtoto salama.
Subscribe to:
Posts (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
Habari ndugu msomaji wetu wa blog, Natumaini unaendelea vyema. Leo tutaanza kujifunza kilimo cha bora cha nyanya, na tutaanza kufahamu vit...