Wednesday, 10 May 2017

SHIRIKA LA WOTESAWA LAZIDI KUSAMBAZA ELIMU YA KUTETEA HAKI ZA WATOTO WAFANYAKAZI



Mwanasheria na Msimamizi wa Mradi wa Uwezeshaji Shirikishi kwa watoto wafanyakazi wa nyumbani nchini Tanzania, Jackline Ngallo, akiwasilisha mada kwenye semina kwa Viongozi wa serikali za mitaa kutoka wilaya za Nyamagana na Ilemela mkoani Mwanza.




Semina hiyo ya siku tatu, kuanzia jana Mei 09 imewashirikisha Madiwani, Watendaji wa Kata, Maafisa Maendeleo na Ustawi wa Jamii, Wenyeviti wa Mitaa na dawati la jinsia kutoka jeshi la polisi imelenga kuwajengea uwezo viongozi hao ili kusaidia kutetea na kulinda maslahi ya mtoto mfanyakazi wa nyumbani na kumuepusha na utumikishwaji wa kazi ngumu na maslahi duni.

#BMGHabari


Mwanasheria wa Shirika la WOTESAWA, Jackline Ngallo, akiwasilisha mada kwenye semina hiyo ambapo pia ameelezea juu ya umuhimu wa viongozi hao kuitambua Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004 ambayo inakataza mtoto chini ya umri wa miaka 14 kuajiriwa huku wale walio juu ya umri huo wakipaswa kuajiriwa kufanya kazi zisizo hatarishi.




Aidha amekumbusha juu ya kuutambua Waraka wa Mishahara wa mwaka 2013 ambao unaelekeza kwamba mfanyakazi wa kazi za nyumbani anapaswa kulipwa kiwango cha chini cha mshahara ambacho ni shingili 150,000 iwapo mwajiri ni balozi ama mfanyabiashara mkubwa, elfu 80,000 ikiwa mwajiriwa haishi kwenye nyumba ya mwajiri wake, elfu 40,000 ikiwa mwajiriwa anaishi kwenye nyumba ya mwajiri wake na shilingi 130,000 ikiwa mwajiri ni rai wakigeni.


Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiwasilisha maoni yao baada ya majadiliano katika makundi


Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiwasilisha maoni yao baada ya majadiliano katika makundi


Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akichangia mada


Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiwasilisha maoni yao baada ya majadiliano katika makundi


Baadhi ya washiriki wa semina hiyo


Semina hiyo ilianza jana Mei 09,2017 na inatamatika kesho Mei 11,2017 Jijini Mwanza


Waraka wa Mishahara wa mwaka 2013 kwa wafanyakazi wa nyumbani


Afisa kutoka shirika la WOTESAWA akiwa kwenye semina hiyo


Diwani wa Kata ya Buhongwa Jijini Mwanza, John Kabadi, amesema semina hiyo itwasaidia katika kutetea maslahi ya watoto wafanyakazi wa nyumbani ikiwemo kuwaepusha na utumikishwaji pamoja na ujira duni.


Gloria Shindika kutoka dawati la jinsia, kituo cha polisi Igogo Jijini Mwanza, amesema semina imewaongezea mbinu zaidi za namna ya kuwasaidia watoto wafanyakazi wa nyumbani watakaokuwa wakikumbwa na aina yoyote ya utumikishwaji.


Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyamanoro Kaskazini, Kata ya Ibungilo Manispaa ya Ilemela, ameeleza kutumia elimu aliyoipata kwenye semina hiyo katika kuwaelimisha wananchi wa mtaa wake katika kuhakikisha maslahi na haki za mtoto yanalindwa


Mwanasheria wa Shirika la WOTESAWA, Jackline Ngallo, akizungumza na Lake Fm Mwanza


Shirika la WOTESAWA linawahimiza wanajamii kwamba bado watoto wafanyakazi wa nyumbani wanayo haki ya kupata elimu hivyo ni vyema haki hiyo ikazingatiwa.


DOROTHY SEMU ATEULIWA KUWA KATIBU MKUU ACT WAZALENDO



KAMATI Kuu ya Act Wazalendo imemuidhinisha Ndugu Dorothy Jonas Semu(pichani), kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo.

Kabla ya uteuzi huu Ndugu Dorothy Semu amewahi kushika nafasi za ukatibu wa Kamati za Sera, Mipango na Utafiti na Kamati ya Fedha na Miradi.

Kwa mujibu wa Kiongozi wa ACT-Wazalendo Mhe. Zitto Kabwe, kupitiaukurasa wake wa Facebook amesema, Ndugu Dorothy Semu ametoa mchango mkubwa kwa chama hasa kwenye uandaaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu, 2015 na masuala mengi ya kiutafiti juu ya sera na mikakati ya Chama.

Ndugu Semu ni mtaalamu wa masuala ya Fiziotherapia mwenye shahada mbili za eneo hilo kutoka Chuo Kikuu cha Western Cape, Afrika ya Kusini. Ana uzoefu wa zaidi ya miaka 16 wa kufanya kazi kwenye nafasi mbalimbali serikalini na kwenye Asasi za kiraia ikiwemo Mratibu wa kuzuia ulemavu kwenye Programu ya Taifa ya Kupambana na Kifua Kikuu na Ukoma.

Tunamtakia kila la heri Ndugu Dorothy Semu kwenye utekelezaji wa majukumu yake.

RAIS MAGUFULI AWAPA MAGARI YA WAGONJWA WABUNGE



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa magari mapya matatu ya kubebea wagonjwa kwa Wabunge watatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuwasaidia wananchi wa maeneo yao ya ubunge.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amekabidhi magari hayo aina ya Land Cruiser Hardtop kwa niaba ya Rais Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa Mbunge wa Nkasi Kaskazini Mkoa wa Rukwa Mhe. Ally Keissy, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa waTabora Mhe. Munde Tambwe na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga.


Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Balozi Kijazi amesema Mhe. Rais Magufuli ametoa magari hayo baada ya kuguswa na kilio cha muda mrefu cha Wabunge hao waliokuwa wakiomba wananchi wao wapatiwe magari ya wagonjwa.


“Mhe. Rais ameamua kuwakabidhi nyinyi haya magari kutokana na vilio vyenu ambavyo amekuwa akivisikia mara kwa mara, Mhe. Keissy umekuwa hata ukitafuta miadi ya kuja kumuona Mhe. Rais kwa suala hili, Waheshimiwa Wabunge wamekuwa wakiyazungumza haya kwa muda mrefu.


“Tunafahamu kila Mbunge katika jimbo lake anahitaji kupata huduma kama hii, na huduma kama hii ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, kwa hiyo sisi Serikali kila tunapopata uwezo basi tunasaidia pale tunapoweza kufikia kwa wakati ule, tulishatoa magari mengine matatu kama haya Chalinze na vituo vingine vya Morogoro.”Amesema Balozi Kijazi


Balozi Kijazi amewapongeza Wabunge hao kwa kupata magari hayo kwa ajili ya wananchi wao na amewasihi kuhakikisha yanatunzwa vizuri ili yadumu muda mrefu na yawahudumie wananchi wote bila kujali dini, kabila, itikadi zao za kisiasa wala makundi.


Kwa upande wao Mhe. Ally Keissy, Mhe. Munde Tambwe na Mhe. Lucy Mayenga wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuitikia kilio chao cha kuwasaidia wananchi magari ya kubebea wagonjwa, na wamempongeza kwa kazi nzuri ya kuwapigania Watanzania wote hasa wenye shida na pia kwa juhudi kubwa za kuleta maendeleo.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
09 Mei, 2017

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi (kati) akiwa na Katibu Mkuu Ikulu Mhe. Alphayo Kidata (Kushoto) na Mkurugenzi wa Huduma Ikulu Bw. Charles Mwankupili (kulia) na Wabunge Mhe Ali Mohamed Kessy (mbunge wa Nkasi Kaskazini) Mhe. Munde tambwe na Mhe Lucy Mayenga (wabunge viti maalumu) baada ya kuwakabidhi magari la kubebea wagonjwa waliyopewa msaada na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 9, 2017

ZIMWI LA AJALI LAZIDI KULITESA TAIFA




Basi la Ally's lililokuwa likitokea Mwanza kuelekea Tabora limegongana na Coaster ya Isanzu uso kwa uso iliyokuwa linaelekea Mwanza kutoka Kahama


Ajali imetokea saa mbili asubuhi eneo la Samuye barabara ya Shinyanga.Hali ya dereva wa Coaster ya Isanzu si nzuri.

Kamanda wa polisi mkoani hapa, Muliro Jumanne amesema chanzo cha ajali hiyo ni basi la kampuni ya Ally's kuwa kwenye mwendo kasi.

Jumanne amesema kuwa abiria waliokuwa kwenye magari hayo ni zaidi ya 70 lakini waliojeruhiwa ni 35 ambao ndiyo wamelazwa hospitali ya mkoa wa Shinyanga.

Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Dk Rashid Mfaume amesema amepokea majeruhi 35 wa ajali hiyo wakiwemo watoto wawili na kwamba kati ya majeruhi hao wenye hali mbaya ni wawili.

BUNGE LATHIBITISHA KUPATA MAJINA KUWANIA UBUNGE EALA KUTOKA CHADEMA



1.Tarehe 4 Aprili, 2017 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilifanya Uchaguzi wa kuwachagua Wajumbe Tisa (9) wa Bunge la Afrika Mashariki watakaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Bunge hilo. Katika Uchaguzi huo, Wajumbe Sita (6) kutoka Chama cha Mapinduzi na Mjumbe mmoja (1) kutoka Chama cha Wananchi (CUF) walichaguliwa. Wagombea wawili kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)walikosa kura za kutosha kuwapatia ushindi.

2.Hivyo, Bunge linapaswa kufanya uchaguzi kwa mara ya pili ili kuwapata wawakilishi Wawili (2) kutoka katika Kundi la Vyama vya Upinzani ambapo Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ndicho chenye hakiya kujaza nafasihizo.


3.Katika mazingira hayo na kwa kuzingatia masharti ya Sheria na Kanuni zinazotawala Uchaguzi huo, na kwa mamlaka niliyonayo kama Msimamizi wa Uchaguzi nilitoa TAARIFA ya Siku ya Uteuzi na Siku ya Uchaguzi kwenye Gazeti la Serikali Na. 537 la tarehe 21Aprili,2017. Taarifa hiyo ilitaja Sikuya Uteuzi(nominationday) wa Wagombea kuwa ni tarehe 03 Mei, 2017 Saa Kumi Kamili (10:00) Jioni na Siku ya Uchaguzi(electionday) kuwa nitarehe 10 Mei, 2017.


Hata hivyo, tarehe 28 Aprili, 2017 Chama cha CHADEMA kiliandikia barua na kuiwasilisha kwangu siku ya tarehe 2 Mei, 2017 Jioni. Barua hiyo ilitoa maelezo kwamba muda waliopewa kuwasilisha majina ya wagombea kupitia kwenye Taarifa hiyo ni finyu kutokana na kuathiriwa na kuwepo kwa siku za mapumziko ya mwisho wa wiki pamoja na Sikukuu ya Mei Mosi iliyoanguakia siku ya Jumatatu hivyo, kuwepo kwa ugumu wa kufanya vikao vyao.


5.Kutokana na sababu hiyo, Chama hicho kiliomba kuongezewa muda usiopungua wiki mbili ili kiweze kukamilisha mchakato wa uteuzi wa wagombea, kupata uthibitisho wa uraia kutoka Idara ya Uhamiaji na uthibitisho wa sifa za kugombea kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa mujibu wa Ibara ya 50 (2) ya Mkataba ikisomwa pamoja na Ibara ya 67 ya Katiba ya Jamhuriya Muungano wa Tanzania,1977.


6.Kutokana na sababu zilizotolewa, niliongeza muda wa siku 4 kuanzia tarehe 3 hadi tarehe 7 Mei, 2017 ili kukiwezesha Chama hicho kukamilisha taratibu hizo za kisheria na hivyo kukitaka kuwasilisha kwangu majina na nyaraka za wagombea waliowateua tarehe 8 Mei, 2017 kabla ya Saa Kumi Kamili (10:00) Jioni ambayo ni Siku ya Uteuzi wa Wagombea(nomination day).


7.Kupitia taarifa hii, napenda kuujulisha umma kwamba Chama cha CHADEMA kimewasilisha kwangu majina sita (6) ya Wagombea wa nafasi mbili za ujumbe wa Bunge la Afrika Mashariki. Kati ya wagombea hao wanne (4) ni wanaume na wagombea wawili (2) ni wanawake.Majina hayo yamewasilishwa kwangu jana tarehe 8 Mei, 2017 kabla ya mudawaSaa 10 Jionikama nilivyokuwa nimeelekeza.


8.Baada ya hatua hiyo,nilifanya uchambuzi wa Nyaraka zilizowasilishwa ili kujiridhisha na uzingatiwaji wa masharti ya uteuzi wa Wagombea kwa mujibu Ibara ya 50 (2) ya Mkataba, Ibara ya 67 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, Kifungu cha 4 (4) cha Sheria ya Uchaguzi wa Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki na Kanuni 5 (2),(3) na Kanuni ya 6 ya Nyongeza ya Tatu ya Kanuni za Kudumu za Bunge,ToleolaJanuari,2016.


Matokeo ya uzingatiwaji wa masharti hayo yameainishwa katika Jedwali lifuatalo:
TANBIHI:


√-Maana yake sharti husika limetimizwa


10.Uchambuzi huo umebainisha kuwa Wagombea wote wamekidhi vigezo na masharti yanayotakiwa kwa mujibu wa Sheria. Hivyo, napenda kutoa TAARIFA na KUWATANGAZA wafuatao kuwa Wagombea katika Uchaguzi wa Wajumbe Wawili (2) kupitia Kundi la Vyama vya Upinzani kutoka Chama cha CHADEMA uliopangwa kufanyika tarehe10 Mei,2017:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...