Saturday, 5 September 2015

MWIGULU NCHEMBA MGENI RASMI UZINDUZI WA KAMPENI JIMBO LA IRINGA MJINI


Kesho, CCM JIMBO LA IRINGA MJINI kutafanyika uzinduzi Rasmi wa kuanza rasmi kwa kampeni za ubunge na madiwani utakaofanyika katika VIWANJA VYA MWEMBETOGWA .
Mgombea Ubunge kwa ticket ya CCM ni FREDRICK MWAKALEBELA atambulishwa rasmi kupeperusha bendera ya chama na mgeni rasmi MWIGULU NCHEMBA.

Maandalizi ya uzinduzi huo yameshakamilika na yatawekwa nakshi na wasanii mbalimbali kama......JB, ANT EZEKIEL, IRENE UWOYA,WEMA SEPETU na pia YAMOTO BAND, TWANGA PEPETA nk watakuwepo kesho kwenye uzinduzi huo.

Pia viongozi mbalimbali wa chama watakuwepo na wageni waalikwa kama LIVINGSTONE LUDINDE, MWIGULU NCHEMBA nk

Bila kuwasahau wenyeji wote hasa wale waliokuwapo kwenye kinyang'anyiro cha kumtafuta mgombea ubunge kwa ticket ya CCM wakiongozwa na MADAM JESCA, MADENGE, KIBIKI, WEEKEND nk.

Sherehe hizi za uzinduzi zitaanza rasmi saa 6 kamili mchana hapa hapa Iringa mjin ktk viwanja vya mwembetogwa. KARIBUNI SANA. (Hapa kazi tu)

A+E NETWORKS(R) KURUSHA DOKUMENTARI YA OJ SIMPSON



Mkuu wa vipindi channel ya A & E Networks, Racheal Job akizungumza na waandishi wa habari kutoka nchi za Afrika waliokusanyika kwenye jukwaa kubwa la kuonesha vitu mbalimbali vinavyoburudisha katika chaneli za DStv na GoTv kupitia MultiChoice nchini Mauritius. Katikati ni Mkurugenzi wa Kanda channel ya A & E Networks, Anthea Petersen na kushoto ni Mkuu wa Mawasiliano channel ya A & E Networks, Sarah Williams-Robbins.



Mkuu wa Mawasiliano channel ya A & E Networks, Sarah Williams-Robbins akifafanua jambo kwenye jukwaa lililowakutanisha waandishi wa habari (hawapo pichani) kutoka nchi mbalimbali za Afrika nchini Mauritius.



Ebenezer Donkoh kutoka YFM Ghana akiuliza swali katika mkutano wa waandishi wa habari ulionadaliwa na MultiChoice Africa.



Philip Mwaniki kutoka Nairobi, Kenya akiuliza swali kwenye jukwaa hilo lililowakutanisha waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali za Afrika.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...