Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mufindi (DED), Saada Malunde (mwenye hijabu) akipata maelezo kutoka kwa mtaalum wa uzalishaji miche, Prosper Wilbright (pili kulia) ya jinsi Kampuni ya Green Resources Ltd hiyo inavyozalisha miche ya miti kitaalamu alipotembelea bustani hiyo ya kuzalisha miche mbalimbali iliyopo katika Kijiji cha Mabaoni wilayani Mufindi, Mkoa wa Iringa jana. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Mabaoni, Sailas Ndenga (kushoto) akipekea akipokea funguo ya jengo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Green Resources Ltd, Anthony Kisondella wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika Kijiji cha Mabaoni, wilayani Mufindi, mkoani Iringa jana. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)
Green Resources Ltd (GRL) imegawa zaidi ya miche milioni tano (5,000,000) kwa wananchi wa vijiji pamoja na kupatiwa mafunzo ya namna ya utunzaji na upandaji wa misitu.
Kaimu Mkurugenzi wa GRL, Anthony Kisondella kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Roselyne Mariki, alisema kuwa hekta zinazokadiriwa kufikia 20,000 zimepandwa miti katika mashamba binafsi ya wanavijiji.
Alitoa rai wakati wa kukabidhi jengo la ukumbi na ofisi kwa Kijiji cha Mabaoni, Kata ya Makungu katika Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa jana.