Peramiho
Ijumaa ya tarehe 19 Novemba ya mwaka 2010 Chuo cha Ufundi cha Peramiho (Peramiho Vocational Training Center) kilichopo Jimbo la Songea, mkoani Ruvuma, kilifanya mahafali yake ya 79 ambapo jumla ya wahitimu 23 walitunikiwa vyeti vya kumaliza mafunzo katika fani mbalimbali.
Katika mahafali hayo jumla ya wahitimu 23 walitunukiwa vyeti vya kumaliza mafunzo katika fani ya ushonaji, ufundi magari na useremala ambapo vijana waliohitimu wanakamilisha idadi ya wahitimu jumla 1,718 katika chuo hiki tangu kuanzishwa kwake mwaka 1928.
Chuo cha ufundi Peramiho kilipata usajili kwa mujibu wa sheria za nchi kwa kuendasha mafunzo chini ya uratibu na muongozo wa VETA ambao ni waratibu wakuu wa mafunzo ya ufundi stadi nchini Tanzania.
Mahafali hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Mtakatifu Benediktini hapa Peramiho na kuhudhulia na wageni mbalimbali kutoka taasisi mbalimbali za hapa Peramiho (Shule ya Wasichana Peramiho, Sekondari ya Sili, Sekondari Maposeni, Daraja Mbili, Chuo cha Uuguzi, Hospitali Peramiho, Seminari Kuu Peramiho na Masista Tutzing).
Awali, Mkuu wa Chuo cha Ufundi Peramiho Bro. Joseph Mukasa alitoa taarifa ya mafunzo kwa mgeni rasmi ambaye alitarajiwa kuwa ni mkurugenzi wa kanda za juu –VETA, katika Mahafali ya 79 Peramiho VTC, lakini kwa niaba yake alimuagiza Mkuu wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) cha Songea Bw. Afridon Mkhomoi.
Bw. Mukasa alisema kuwa chuo chake kia jumla ya wanachuo 116 ambapo wasichana 44 na wavulana 72. Aidha, idadi ya wanachuo katika mwaka ujao (2011) itaongezeka kutoka wanafunzi 116 hadi kufikia idadi ya 160, ilikuenda sambamba na uboreshaji na uongazaji wa miundombinu hususani mabweni ya wasichana.
Alisema kuwa vijana waliyohitimu mafunzo walitoka katika fani zifuatazo: ushonaji nguo za kike na za kiume walikuwa 12(wavulana 4 wasichana 8), ufundi magari(MV Mechanics) walikuwa wavulana 6 na msichana 1 na useremala walikuwa wavulana 4 na kufanya jumla ya wahitimu wote 23.
BAADHI YA CHANGAMOTO WANAZOKABILIANA NAZO
Mahali penye mafanikio hapakosi kuwepo na changamoto, Chuo Cha Ufundi cha Peramiho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali lakini kubwa zaidi ni lile la kupungua kwa misaada kwa chuo siku hadi siku pamoja na kupanda kwa gharama ya za maisha.
Chuo hiki sasa kina umri wa miaka 82 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1928, umri huu si mdogo una changamoto zake katika uendeshaji wake wakati huu wa ulimwengu wa sayansi na teknolojia.
• Uchakavu wa miundo mbinu kama vile vitendea kazi na mitambo, ambapo kwa kiasi kikubwa imepitwa na wakati.
• Uchakavu na uchache wa nyumba za watumishi.
• Mabweni ya wasichana kwa ajili ya wasichana hayatoshi na hii inasababisha chuo kipokee idadi ndogo ya wasichana kwa ajili ya mafunzo.
• Kitengo cha komputa hakina komputa za kutosha ili kukidhi uwiano wa 1:1.
Pamoja na changamoto wazokabiliwa nazo kama chuo ipo pia mikakati waliojiwekea kwa kipindi kijacho kuanzai mwaka 2011.
1. Kuannzisha fani mpya ya Printing Press’ inayounganishwa na ‘Computer Application’.
2. Kuanshia shule ya mafunzo ya udereva kwa kozi fupi fupi (Driving School).
3. Kuendelea na zoezi la kuwajengea uwezo wakufunzi wetu kwa kuwepeleka Chuo Cha Ualimu Morogoro au Off Campus Songea.
4. Kukarabati majengo ya Mruma Center kwa ajili ya hostel ya wasichana.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika nasaha za zake Bw. Afridon Mkhomoi kwa nia ya mkurugenzi wa kanda nyanda za juu-VETA, alikipongeza chuo kwa mafaniko makubwa ya chuo hicho likiwemo swala la kutoa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana.
Alisema kuwa vjiana wakiwezeshwa wanaweza kujiajiri na kujitegemea wenyewe kwa kuanzisha miradi mbalimbali hatimaye kupunguza umasikini.
Pamoja na pongezi hizo mgeni rasmi ambaye pia ni Mkuu wa Chuo cha Ufundi Stadi VETA cha Songea, aliusihi uongozi wa chuo cha peramiho kuanzisha kuotoa fani ngazi ya diploma kutokana na chuo hicho kuwa kikongwe an kuwa waanzilishi wauutoaji mafunzo ya ufundi stadi nchini.
Alisema kuwa kutokana na umri wa chuo hicho kinastahili kabisa kuanzisha program za diploma.
Aidha, mkuu wa chuo cha Songea alihaidi kuwa VETA katika mwaka fedha wa bajeti ujao watasaidia Chuo Cha Peramiho katiak masuala mazima ya vifaa ilikiweza angalau kusonga mbele.
Baba Abate,[Mkuu wa shirika la wabenedictini]Abasia Peramiho, Anastasius Reizer ,ambaye ni abate wa nne tangu kuanzishwa shirika hapa Peramiho, naye ni mtu anayejali na kufuatilia kwa karibu ufanisia katika Nyanja ya elimu hapa Abasiani, kwani ndiye mfadhili mkuu kwa kukiwezesha chuo zaidi ya thelusi mbili ya gharama za uendeshaji wa chuo hicho.
Kwa kweli anatakiwa pongezi za pekee na bila kuficha ni mfano wa kuigwa na wengine.
Baba Abate Anastasius Reiser (OSB-Mkuu wa Shirika la wabeneditini ) Abasia Peramiho
Mkuu wa Chuo cha Ufundi Peramiho Br. Joseph Mukasa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake hivi karibuni.