PICHA NA FRIDAY SIMBAYA |
Akiwa amesimama nje ya ofisi ya kinyozi iliyopo mtaa wa posta mjini Iringa, mkoani Iringa, akitanzama kuzama kwa jua Msanii wa sanaa ya maigizo mainispaa ya Iringa, Erasto kilowoko (pichani) maarufu kama ‘magumashi’ametangaza kuuza figo yako moja kwa shilingi milioni 25.
Kilowoko alisema akipata fedha hizo atatumia kugharamia utengenezaji wa filamu mpya anayopanga kuiandaa mwaka huu kwa ajilli kueleisha vijana kuhusu masuala ya uzalendo na uwajibikaji.
“Nimekuwa nikiomba viongozi na makampuni mbalimbali wanisaisie kutimiza ndoto zangu za kuwa kioo cha jamii kwa kutoa elimu kwa njia ya filamu,” alisikika akisema msanii huyo.
Akizungumza jana na nipashe magumashi alisema kuwa anataka kuuza figo ili aweze kutimiza ndoto ya muda mrefu, lakini anashindwa kufanikisha hilo baada ya wadau mbalimbali waliowafuata kuomba msaada kutomsaidia.
Msanii huyo ambaye kwa sasa anajishughulisha kama kinyozi mjini Iringa alisema kuwa kati ya hizo 25,000,000/- anazotarajia kuzipata baada ya kuuza figo sehemu atalipata kodi kama mtanzania kusaidia watoto yatima.
Akizumhuzia kuhusu soko la filamu kwa sasa nchini, kilowoko alisema ana Imani kubwa ka serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais dk john pombe magufuli kutokana na juhudi zinazochukuliwa kupamban na biashara haramu ya kazi ya wasanii.