Saturday, 30 January 2016
Dkt. Kigwangalla awapa funzo watumishi wa sekta ya afya, awataka kuwa wabunifu
Licha ya juhudi zinazofanywa na serikali kuboresha sekta ya afya nchini, watumishi wa sekta ya afya wametakiwa kuwa wabunifu ili kuweza kutoa huduma kwa watu wote hususani wenye kipato cha juu.
Licha ya kutembelea wodi mbalimbali za wagonjwa, Dkt. Kigwangwala alitembelea maabara ya hospitali hiyo na kuridhika na vifaa vilivyopo kwenye hospitali, kushoto ni mtaalamu wa viwango vya maabara, Felix Zelote akimpatia maelezo waziri huyo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akibadilishana mawazo na wataalamu wa hospitali hiyo kwenye chumba cha upasuaji
Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati akitembelea Hospitali ya Mount Meru iliyopo mkoani Arusha.
Amesema hospitali zinatakiwa kusimama zenyewe kwa ukusanyaji wa mapato,hivyo upo ulazima wa kujenga au kukarabati majengo ambayo wanaweza kufanya wodi za kulipia ambazo zitakua zenye ubora ambao unaweza kuwashawishi watu wenye pesa kuja kupata huduma kwenye hospitali za umma kuliko hivi sasa wanakimbilia hospitali binafsi.
"Hii itaifanya serikali kupata pesa ambazo sehemu kubwa zitatumika kuwahudumia watu wenye kipato cha chini hospitalini hapa,” alisema Dkt. Kigwangalla.
Hata hivyo Naibu Waziri huyo alisema wateja wengi wanapokuja kupata huduma kwenye vituo vya huduma ya serikali,wanakata tamaa kwakuwa wanakuta hakuna watoa huduma, dawa wala vifaa tiba hivyo wanakimbilia huko kwenye hospitali binafsi.
"Lengo letu sio kuua hospitali binafsi bali tunataka muimarishe huduma za kulipia ili tupate pesa za kuwahudumia wasio na uwezo na ninyi watoa huduma wa serikali mpate sehemu yenu ili muweze kufanya kazi kwa ufanisi,” alisema Dkt. Kingwangalla.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akibadilishana mawazo na wataalamu wa hospitali hiyo kwenye chumba cha upasuaji
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangwala akiwa amembeba mtoto mchanga (bado hajapatiwa huduma) na mama wa mtoto huyo Bi. Jamila Petro alipotembelea wodi ya wazazi hospitalini hapo
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akimuangalia mtoto huyo
RAIS MAGUFULI AMUONGEZEA MUDA WA KUSTAAFU JENERALI MWAMUNYANGE
RAIS John Magufuli amemwongeza muda wa mwaka mmoja, Mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini,J enerali David Mwamunyange, ambaye alitakiwa kustaafu leo baada ya kutimiza umri kwa mujibu wa katiba na sheria.
Anaadika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Akizungumza na waandishi wa habari,leo mapema kwenye Makao makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)yaliyopo Upanga jijini Dar es salaam,Jenerali Mwamunyange amesema leo alitakiwa kuungana na Brigedia wanne wa Jeshi ya ulinzi nchini pamoja na Meneja Jenerali wawili, ambapo wote kwa pamoja kwa pamoja wamestaa ndani ya Jeshi kwa mujibu wa sheria ya jeshi hilo.
“Mimi mwenyewe ilikuwa nistaafu kazi leo , lakini Rais na Amri Jeshi mkuu ameamua kunibakiza katika utumishi jeshini kwa mwaka mmoja kuazia leo hadi tarehe 31 Januari 2017,”amesema Jenerali Mwamunyange
eneral Mwamunyage amesema sababu iliyomfanya Rais Magufuli kumwongezea mda huo,imetokana na Rais kutopata mtu sahihi wa kujaza nafasi hiyo aliyonayo tena.
Hata hivyo, Jenerali Mwamunyange amesema Rais Magufuli amemteua Luteni Jenerali Venance Mabeyo kuwa mnadhimu mkuu wa Jeshi la ulinzi la wananchi,
Sanajari na huyo,Jeneral Mwanunyange amesema pia,Rais Magufuli , amefanya uteuzi mkubwa ndani ya Jeshi hilo ili baada ya kuteua watu kushikanyadhifa mbali mbali ndani ya jeshi hilo,
Jenerali Mwamunyange ametaja walioteuliwa na Rais, ni Meja Jenerali James Aliois Mwakibolwa kuwa Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la nchi Kavu,ambaye amechukua nafasi ya meja Jenerali Salum Mustafa Kijuu anayestaaafu kazi leo baada ya kufikisha umri wa kustaafu kisheria,ambapo Meja Mwakibolwa alikuwa ni mkuu wa tawi la utendaji wa kivita na mafunzo makao mkuu ya jeshi.
Jeneral Mwamunyange alimtaja pia aliyeteuliwa na Rais,ni -Meja Jenerali-Yakub Sirakwi kuwa Mkuu wa chuo cha ulinzi wa Taifa (Commandant NDC) - kuchukua nafasi ya Meja Jenerali Gaudence Milanzi ambaye ameteuliwa na Rais kuwa Katibu mkuu wa wizara ya Maliasilia na utalii,Meja Jenerali Sirakwi alikuwa mratibu msaidizi mkuu baraza la usalama wa Taifa- BUT.
Mwengine ni aliyeteliwa na Rais Magufuli ni -Brigedia Jenerali George William Ingram, kuwa Mkuu wa Kamandi ya jeshi la Anga, ambaye aliyechukua nafasi ya Meja Jenerali Joseph Pwani aliyestaafu leo kisheria baada ya kufikia umri wa kustaafu,Bregedua Jenerali Ingram alikuwa Afisa Mnadhimu katika mako makuu ya kamandi ya Jeshi la Anga.
Pia Rais Magufuli alimteua Bregedia Jeneralio M.W Isamuhyo kuwa Mkuu wa jeshi la Kujenga Taifa-,kuchukua nafasi ya Meja Jenerali Raphael Muhuga anayestaafu kazi leo, baada ya kufikisha umri wa kustaafu kazi kisheria,kabla ya uteuzi Bregedia Isamuhyo alikuwa mkurugenzi makao mkuu ya jeshi.
Vilevile Rais Magufuli amemteua Bregedia Jenerali Jacob Kingu kuwa mkuu wa shirika la mzinga-,kuchukua nafasi ya Meja Jenerali Charles Muzanila anayestaafu leo kisheria baada ya kufikisha umrii,Brigedia Jeneral Kingu alikuwa mkuu wa utawala na mafunzo katika makao mkuu ya jeshi la kujenga Taifa.
Hata Hivyo,Rais Magufuli amemteua Bregedia Jenerali Robison Mwanjela, kuwa mkuu wa chuo cha Tiba Lugalo (MCMS)- kuchukua nafasi ya Brigedia Jenerali Msangi anatestaafu leo kazi,baada ya kufikisha umri kustaafu kisheria,Kabla ya uteuzi Brigedia Jeneral Mwanjela alikuwa mkuu wa Tiba Hopsitali kuu ya Jeshi Lugalo.
Aidha,Rais Magufuli amemteua Brigedia Jeneral George Msongole kuwa Kamanda wa Brigedia ya Tembo,- kuchukua nafasi ya Brigedia Jeneral J.M Chacha ambaye anastaafu leo baada kisheria baada ya kufikisha umri wa kustaafu, Bregedia Jenerali Msongole kabla ya kustaafu alikuwa bAfusa Mnadhimu makao makuu wa Jeshii.
Rais Magufulia pia amemteua Bregedia Jenerali Sylevesta M.Mijna kuwa mkuu wa chuo cha ukamanda kuchukua nafasi ya Meja Jenerali Ezekiel Kyunga ambaye anastaafu kzai leo baada ya kufikisha umri wa kustaafu kisheria,ambapo kabya ya uteuzi,Bregedia Jenerali Minja alikuwa mkuu wa utawala katika chuo cha Ulinzii wa Taifa –NDC.
WATUMISHI WA HOSPITAL YA SEKOUR TOURE, HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA NA CHUO CHA IFM WASHIRIKI ZOEZI LA USAFI LA KILA MWEZI
Dkt.Magreth William Magambo ambae ni Daktari Bingwa wa Mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure akitoa ufafanuzi juu ya Ushiriki wa Watumishi wa Hospitali hiyo la kushiriki Usafi wa Mazingira la Kila Jumamosi ya Kila Mwisho wa Mwezi lililofanyika hii leo January 30,2016.
Amesisitiza wananchi kuwa na desturi ya kufanya Usafi wa mara kwa mara (Kila Siku) katika mazingira yao ili kuepukana na hatari ya kupata magonjwa ya kuambukiza ikiwemo kipindupi huku akikumbusha zaidi pia wanajamii kuzingatia kanuni za usafi katika maeneo muhimu kama vile vyooni. Kunawa mikono kwa maji safi na sabuni baada ya kutoka chooni.
Dkt.Peter Maziku ambae ni Daktari katika kitengo cha CTC katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure akizungumza wakati wa zoezi la usafi la kila mwisho wa mwezi lililofanyika hii leo Jijini Mwanza.
Anasema watoa huduma mbalimbali (Madaktari, Waalimu, Wafanyabiashara nk) katika jamii lazima wawe mfano wa kuigwa katika kuwajibika kuweka mazingira katika hali ya usafi ili kuwezesha wananchi wengine kuiga mfano huo.
Baadhi ya Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure wakishiriki zoezi la Usafi wa Mazingira la Kila Jumamosi ya Kila Mwisho wa Mwezi lililofanyika hii leo January 30,2016.
Baadhi ya Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure wakishiriki zoezi la Usafi wa Mazingira la Kila Jumamosi ya Kila Mwisho wa Mwezi lililofanyika hii leo January 30,2016.
Kulia ni Dkt.Peter Maziku ambae ni Daktari katika kitengo cha CTC katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure akiwa pamoja na Dkt.Charles Ludibuka ambae ni Mfamasia katika Hospitali hiyo Sekour Toure walishiriki zoezi la usafi katika Mazingira ya Hospitali hiyo.
Katika picha wakichoma uchafu baada ya usafi.
Baadhi ya Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure wakishiriki zoezi la Usafi wa Mazingira la Kila Jumamosi ya Kila Mwisho wa Mwezi lililofanyika hii leo January 30,2016.
Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, wakishiriki zoezi la Usafi wa Mazingira la Kila Jumamosi ya Kila Mwisho wa Mwezi lililofanyika hii leo January 30,2016.
Hapa wakiwa katika barabara ya Machemba Jijini Mwanza ambayo inatoka na kuingia katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sour Toure.
Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, wakishiriki zoezi la Usafi wa Mazingira la Kila Jumamosi ya Kila Mwisho wa Mwezi lililofanyika hii leo January 30,2016.
Hapa wakiwa katika barabara ya Machemba Jirani na Kituo cha mafunzo ya Lugha mbalimbali cha International Language Training Centre Jijini Mwanza ambayo inatoka na kuingia katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sour Toure.
Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, wakishiriki zoezi la Usafi wa Mazingira la Kila Jumamosi ya Kila Mwisho wa Mwezi lililofanyika hii leo January 30,2016.
Hapa wakiwa katika barabara ya Machemba Jirani na Kituo cha mafunzo ya Lugha mbalimbali cha International Language Training Centre Jijini Mwanza ambayo inatoka na kuingia katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sour Toure.
Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, wakishiriki zoezi la Usafi wa Mazingira la Kila Jumamosi ya Kila Mwisho wa Mwezi lililofanyika hii leo January 30,2016.
Hapa wakiwa katika barabara ya Machemba Jirani na Kituo cha mafunzo ya Lugha mbalimbali cha International Language Training Centre Jijini Mwanza ambayo inatoka na kuingia katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sour Toure.
Wanafunzi pamoja na Watumishi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM tawi la Mwanza, pia nao walishiriki zoezi la Usafi wa Mazingira la Kila Jumamosi ya Kila Mwisho wa Mwezi lililofanyika hii leo January 30,2016.
Subscribe to:
Posts (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
The most deadly form of tuberculosis is one that lies in wait inside the body for years, attacking at the first sign of weakness. Abou...