Thursday, 26 October 2017

MPANGO WA KKK WAPATA MAFANKIO

Teacher in Kenya leads a reading lesson



Muwezeshaji wa ushiriki wa jamii katika elimu (CEF)Sarah Dotto ambaye pia mratibu mradi wa Tusome Pamoja wilaya ya iringa, mkoani iringa akitoa maelekezo kwa wajumbe katika kikao cha mrejesho cha kuwakilisha mipango ya shule zao uliofanyika katika shule ya wasichana ya Ifunda hivi karibuni. (Picha na Friday Simbaya)


Baadhi ya wajumbe kutoka vijiji mbalimbali katika wilaya ya iringa, mkoani iringa wakifuatilia mkutano wa mrejesho wakati wenzao wa kiwakilisha mipango ya shule zao uliofanyika katika shule ya wasichana ya ifunda hivi karibuni. (Picha na Friday Simbaya)

Na Friday Simbaya, Iringa

Wadau mbalimbali wa sekta ya elimu mkoani Iringa wamesifu mradi ya ‘USAID Tusomo Pamoja’ unaolenga kuongeza umahiri katika kujua kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK).

Wakiongea kwa nyakati tofauti wadau hao walisema kuwa mradi huo umeleta ufansi katika shule za msingi mkoani hapa hasa shule ambazo zipo kwenye mradi.

Walisema kuwa wanafunzi wamejengewe uwezo wakiwa darasa la kwanza hadi la nne katika stadi za KKK, katika lugha ya mazungumzo, misingi ya kuandika na utambuzi wa dhana ya namba.

Hayo yameelezwa hivi karibuni katika mikutano ya marejesho ya mipango ya rahisi kutoka katika shule zao iliyofanyika katika wilaya ya iringa na kilolo mkoani iringa hivi karibuni.

Kaimu Ofisa Elimu Wilaya Kilolo Antony Makwaya ambaye pia ni mratibu wa mradi wa Tusome Pamoja wilayani Kilolo, mkoani Iringa alisema katika kutimaza malengo kadhaa ya elimu ikiwemo kukuza stadi za KKK, serikali imekuwa ikiwa ikifanya kazi na wadau kadhaa zikiwemo taasisi binafsi za kimataifa na kitaifa.

Alisema kuwa wazazi sasa wameanza kushirikiana na walimu katika kujua maendeleo ya watoto wao na kutokana na juhudi hii, watoto wanasoma sababu wanaelewa wazazi wao wapo karibu na wanafuatilia maendeleo yao shuleni,’’ anaongeza kusema.

Makwaya alisema malengo makuu ya mradi ni kuunga mkono jitihada za Serikali ili kuweza kufikia lengo la kuondoa kabisa tatizo la wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika kwa darasa la kwanza na la pili ifikapo mwaka 2021.

“Lengo jingine ni kuisaidia Serikali kwa kuwapatia walimu mbinu za ufundishaji pamoja na vifaa vya kujifunzia ili kuinua kiwango cha elimu nchini,’’ anasema.

Kwa upande, mratibu wa mradi Wilaya ya Iringa Sara Dotto alisema kwa USAID Tusome Pamoja ni mradi wa elimu wa miaka mitano unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Watu wa Marekani (USAID). 

Mradi huu unalenga kusaidia kuboresha stadi za ufundishaji na kujifunza kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK) katika shule za awali na madarasa ya chini ya shule za msingi (1-4), katika mikoa minne ya Tanzania bara (Iringa, Morogoro, Mtwara na Ruvuma) pamoja na shule zote za serikali Zanzibar. 

Dotto alisema kuwa Pamoja na kutoa mafunzo kwa walimu , vitabu kwa wanafunzi, malengo zaidi ya mradi wa USAID Tusome Pamoja ni kuimarisha ushiriki wa wazazi na jamii kwenye elimu kupitia kamati za shule, Ushirikiano wa Wazazi na Waalimu ( UWAWA) na jamii yote kwa ujumla.

Hivi Karibuni, USAID Tusome Pamoja ikishirikiana na serikali katika mikoa huu, iliendesha mafunzo ya mpango jamii wa uhamasishaji na utekelezaji elimu (MJUUE) wenye lengo la kuhamasisha jamii katika kubaini changamoto katika sekta ya elimu zinazo athiri ubora wa elimu na ufaulu; Kubaini rasilimali na utatuzi wa changamoto hizo.

Pia mafunzo haya yalilenga (kusaidia jamii ishiriki katika kuandaa mipango ya elimu kwa ajili ya watoto wao hivyo kuimarisha ushiriki wa jamii katika kuboresha utoaji wa elimu.

Naye Winston ambaye ni mratibu wa mradi Wilaya ya Kilolo alisema kupitia mpango huo USAID Tusome Pamoja ilitoa mafunzo ya siku tatu kwa Wawezeshaji Jamii Elimu 968 kutoka shule 481 za msingi za serikali mkoani Iringa.

Kwa sababu hii, shirika la Misaada la Marekani (USAID), limeanzisha mkakati uitwao Tusome Pamoja ambao pamoja na mambo mengine unalenga kutoa mafunzo kwa walimu wanaofundisha madarasa ya chini, msisitizo ukiwa stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu.

Alisema kuwa pamoja na mambo mengine wameweza kusaidia kuongoza uandaaji wa dira na mipango kazi ya muda mfupi ya shule zao za msingi na mipango hiyo kuridhiwa na jamii, Wahamasishaji hawa baada ya kupata mafunzo.

“Kupitia mafunzo haya tumeanza kuona mafanikio ya wanafunzi wanaoingia darasa la tatu, huku wakijua kusoma kuandika na hisabati kwa sababu ya uwingi wa vifaa vya kufundishia hasa vitabu pamoja na elimu waliyoipata walimu hawa,”alisema Winston.

Pia wanafanya kazi ya kujitolea ya kuhamasishaji jamii kushiriki katika shughuli zote zinazohusu elimu katika shule zao.

“leo hii wamekuja wilayani kutoa mrejesho kwa ofisi ya halmashauri ya wilaya juu ya mipango waliyojipangia na yale mambo watakayofanya kutelekeza mipango yao na baadhi ya mipango yao itajumuishwa kwenye mpango wa serikali ya mwaka ujao wa fedha,” alisema Winston.

Ukiondoa Iringa, alisema mradi huo unafanyika pia katika mikoa ya Mtwara, Ruvuma, Morogoro na Zanzibar.

Baadhi ya wazazi na walezi pia mradi wa tusome pamoja umesaidia kuondelea dhana kuwa shule ni mali ya mwalimu mkuu au walimu isipokuwa shule ni mali ya jamii.

Walisema kuwa baadhi ya changamoto katika shule zimeanza kupungua kama vile masuala ya chakula mashuleni wazazi wamekuwa na muamko wa kuchangia.

Hata hivyo, watekelezaji wa mradi Research Triangle Institute (RTI) kwa shirikiana na Plan International, idara aa elimu na maendeleo ya jamii.


WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...